Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Saturday, December 31, 2011

mambo yote ni Lidaz Club leo mpaka kuchwee na tamasha la bongo 50 katika mkesha wa mwaka mpya



AIRTEL 50 na mkesha wa mwaka mpya katika viwanja vya lidaz Club hapa jijini Dar Es saalam ndio mambo yameanza sasa ni wakati wako unaambiwa kujisogeza Taratiibu katika kuja kufurahi na kuburudika tukusubiri kuuanza vyema mwaka mpya.




 uwanjani tayari kabisa Exta Bongo Next Level waiongozwa na Alichoki wameanza kutoa dozi ya burudani na airtel 50. bado ni muendelezo wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Tanzania.








Gari mpya ya kurushia matangazo ya Clouds Tv ( OB VAN)   tayari kabisa ikiwa imesha paki sehemu maalum ya kuweza kurusha live Tamasha la Bongo 50 linarushawa  live na Clouds Fm na Clouds Tv pande za lidaz Club leo 


Meneja  uhusiano wa kampuni ya simu za mkononi ya  Airtel bwana Jackson Mbando  akiwa na baadhi ya waandaaji wa tamasha la funga mwaka wakigawa CD zenye nyimbo za wasanii mbalimbali .

Friday, December 30, 2011

KIDUMU(2011's1st east African artist)TOUR, BELGIUM, SWEDEN, SWISS


Jean Piere Nyimbona AKA Kidum Kibido mmoja kati ya artiest wa Sk Entertainment akisongesha mbele
 keep it up Kidum
hiki ndio kinacho takiwa kwa mwanamuziki wa ukweli uwezo wakupiga vyombo vyote na kuimba vizuri pasipo kutetereka kama ulikuwa ufahamu basi fahamu sifa moja wapo ya kidumu ni uwezo mkubwa alionao katika kupiga drums huku akiimba live bila kukosea kitu ambacho kwa wanamuziki wengine imekuwa Ngumu kuweza hilo.

tumsuport Teddy Kalonga Haight binti wa kitanzania anaependa Maendeleo kaja na Lotion yake sasa


Huyu ndie binti mrembo

Teddy Kalonga Haight


 
Ambae kwa sasa amekuja na bidhaa yake mpya ni lotion hebu soma maelezo pichani chini na jinsi ya kuweza kumsuport siku zote kuwa naamini ma binti wa kibongo wakali , wanakili na tunaweza  kwa lolote ni wajasiri na wapambanaji haya sasa kazi ni kwako BUY MY LOTION ya TK.




Sasa ni wakati wa kupata ile ngozi yako nyororo asilia unayoitaka! 

MyLotion ni lotion asilia itakayofanya ngozi yako kuwa na mwonekano mmoja asili na wenye kuvutia. MyLotion pia inakuja na scents 2, Limao na Vanilla. Karibu kujaribu MyLotion!!


Bei:
  • $45 Small 8oz
  • $65 Regular 16oz
  • $110 Large 32oz 
Jumlisha pesa ya kutuma: 
  • $10 United States
  • $15 International (kama ukinunua kupitia PayPal itakuchaji $10 tu. Raha eh!?...)

Kuagiza:
  • Purchase using a credit card with PayPal

AU
  • Waweza tumia Western Union, au Money Gram kwa kutuma malipo kwa anwani hii:  Teddy Haight, Los Angeles, CA 90028. 
  • Kisha tuma email ya maelezo ya kupokea hayo malipo kupitia email hii=>  "getmylotion at gmail.com" . Bila kusahau anwani yako utakayotaka lotion ikufikie.


Kama una swali lolote husisite kunipigia simu moja kwa moja ukaongea na mimi +1(323) 325-1772

Nawapenda woooo't
~TK 


Haijarishi huko wapi, MyLotion itakufikia popote pale ulipo. India, Africa, Ulaya ndani ndani, Asia, na Marekani bila shaka.

Thursday, December 29, 2011

BOZI BOZIANA na MASHUJAA BAND show ya pamoja kesho IJUMAA 30


BOZI BOZIANA na MASHUJAA BAND show ya pamoja kesho IJUMAA 30 December katika ukumbi wa BUSINESS PARK-GREEN ACRES HOUSE victoria kijitonyama

Mama land ilipotua yatua kinshasa kushuhudia Papa wemba akirecord na mashujaa muzica

hii ndio studio kubwa na ya kisasa huko Kinshasa ambayo wanamuziki wengi wakongwe huko Kongo wamekuwa wakiitumia kufanyia kazi zao akiwamo, papa wemba, bozi boziana, werasoin, Jb mpiana na wegine ni studio gani na inaitwaje live katika new season ya Mama land.

Next season Mama land ilitua kinshasa live utashuhudia papa wemba akipiga vocal katika wimbo alioshirikishwa na Mashujaa Musica wataalam wa muziki wa hapa Bongo .



lakini pia utapata kushuhudia live Werrasoin akiingiza vocal kwa ajili ya single zake mpya kama unavyo muona pichani
Bozi Boziana pia usikosee katika Mama land new season.

Kimora Lee Simmons alivyo sherehekea Christmas paoja na wanae & mumewe huko St. Barts



Kimora Lee Simmons akifurahiaChristmas pamoja na familia yake .  TV star  huyo alionekana pamoja na mumewe mwanamitindo Djimon Hounsou na mwanae wa kiume mwenye miaka 2-aliejulikana kwa jina la Kenzohuko St. Barts siku ya  (December 25).
Familia nzima akiwemo ,  Ming Lee, 11, a  Aoki Lee, 9 ( watoto Kimora’aliezaa na mumewe wa kwanza walietalikiana bwana  Russell Simmons) waliitumia wiki yooe vizuri kabisa  kwenye ufukwe wa Flamands .

Kim Kardashian bila make-up...



hapa bi dada mrembo anae tikisa huko Hollywood kwa urembo. akiwa hana Make up duh!!! ukizingatia hapa Bongo wadada kibao ndio wanaoongoza kwa kumuiga kweli wanawake wa afrika ni Wazuri duh kwa namna hii Mbona tunawafunika mbaya sana ho kina Kim K.


sasa hapo Binti kashaficha makovu kwa make up za ukweli watu woote wanachanganyikiwa @ ndio binti anaetikisa Majuu kwa uzuri jamani kweli tembea uyaone ya malimwengu.

Radio RFI inakutakieni Heri ya Kris masi na Mwaka Mpya


"Kwa marafiki na wasikilizaji wetu barani Afrika na duniani kote kwa
ujumla, Wafanyakazi wote wa Idhaa ya Kiswahili ya Radio France
Internationale iliyoko Dar Es Salaam – Tanzania, wanakutakia Heri ya
Kris masi na Mwaka Mpya wa 2012 wenye fanaka."

--
RFI Kiswahili
c/o TBC Broadcasting House
Nyerere Road
P.O.Box 69077
Dar es Salaam
Tanzania
www.rfikiswahili.com

Grooveback New Year's Eve Party!!

Wadau Nyote mnakaribishwa Tuanze mwaka...2012 Pamoja...

Wednesday, December 28, 2011

huyu ndie rafiki wa kweli hata ulale bila nguo hasemi


Anae kataa na aseme leo kwamba huyu sie Rafiki wakweli !!!!!!??? (KITANDA)
umewahi kujiuliza ni mambo magapi umeyafanya ukiwa Nyumbani tena kitandani kwako chumbani na hata sikumoja kitanda hicho A.K. A BED hakijawahi kukusaliti au kukusema vibaya nje ya hapo au hata kumweleza mgeni wako kwamba jana ulifanya nn??????!!! ha ha ha ha ha nacheka maana nimegundua kuwa huyu ndie Rafiki wa kweli maana hata ulale bila nguo kitanda chako hakiwezi kusema kwa yeoyote au kikasema  lolote  kamwe hakitakusaliti. anaebisha aseme.

RAHA YA KIJIJINI KWETU

Tukio hili naweza sema hufanyika Mara moja tu kwa mwaka ambapo wana familia wengi tunakutana kujumuika na kufanya mambo mbali mbali ya kifamili kwa kuwa kwa mwaka mzima huwa tunakuwa katika mikoa mbali mbali wenzetu wa mjini hutania wachaga wakidai kuwa tumeenda kuhesabiwa, Sensa ya kufunga mwaka ha ha ha ha Basi na mie mwaka huu nikajichangana na wachaga wenzangu haya ndio nilioyaona na kujikumbusha mengi ambayo niliyakosa kwa muda mrefu jumuika nami

Marangu moja hiyoo Gree Land

kichumi kina kuwa kisafiii, kwa wachaga wanelewa nikisema kichumi namaanisha ni kale kanjia ka kuingilia Nyumbani ni utamaduni kwa wachaga wengi huwa hawakosi kanjia hako  hicho ndio  kichumi na nilazima kifagiliwe kila siku saa 12 alfajiri inapendeza sana
unapofika kijijini kwa wachaga wa marangu basi utapokelewa na kitochi ( mbege ) ni pombe ya asili ambayo hupikwa kwa ndizi mbivu na ulezi  nili enjoy sana maana ni muda mrefu sikuwa nimeipata


Marangau kuna vivutio vingi sana kuanzia mazingira tu kwa usafi na mengine mengi


Maji ya chemichemi ambayo ni masafi kuliko kawaida


wazee wa familia wanapokutana kujadili mambo



straw Bell mjini huuzwa bei mbaya sana ila kwetumarangu zimejaa kibao wenyewe wanita MAWERO bureee wala hununui.




bro akiwa kapozi na yeye kwenye jumba lake la  la joto ha ha ha ha






mauwa mazuri ambayo ukija mjini utauziwa kwa bei ya gali kule yapo yamejiotea tu na unapochuma hata wenyeji hukushangaa kuwa unapeleka wapi yapo tuuuu.



majimbi na mboga aina ya salad mboga mboga hiyo ndogoo iliyo tambaa kwenye Maji ya majani ambayo huota katika maji marangu zipo kibao hizo


PICHA ZAIDI ZINAKUJA NA MATUKIO MEEENGI

Tuesday, December 27, 2011

25 Dec The day to Remember



kila ifikapo tarehe 25 December kwangu huwa ni siku muhimu sana si tu kwakuwa wakristo ulimwenguni kote tuna adhimisha sikukuu ya Christ Mass, bali hunikumbusha kujumuika na Mama yangu mpenzi Salama J mohamed Mama yake na Sophia kessy ambae huadhimisha siku yake ya kuzaliwa akiwa kazaliwa miaka kadhaa iliopita huko Sikonge Tabora Mama wa Kinyamwezi Mwenye asili pia ya Tanga  sina cha kumpa isipokuwa daima nitajitoa kuhakikisha anakaa kwa amani na upendo kama alivyo nilea hiyo ndio ilikuwa ahadi ya zawadi  kwangu kwake mapema juzi alipoadhimisha iku ya kuzaliwa.

Mama nakupenda sana tena sana Happy Birthday wa Mara nyingine tena.
sophia kessy.

HODI HODI WADAU HATIMAE NIMERUDI TENA!!!

BAADA YA KUPOTEA KWA SIKU KADHAA HATIMAE WAPENZI NA WADAU NIMEREJEA TEANA NIKIWA NA AFYA TELE ASANTENI KWA SUPORT NA KWA KUENDELEA KUTEMBELEA BLOG HII BASI SI VIBAYA NIKA SHEAR NA NYIE KILE NILICHOKIONA NILIPOKUWA AMA KUWAFAHAMISHA NINI KILIJIRI ENDELEA KUWA NAMI SOON NAKUDONDOSHEA BURUDANI NA HABARI HUSIKA
SOPHIA KESSY.

Monday, December 19, 2011

wachaga umefika msimu wa kwenda kwetuu


haya kile kipindi ambacho wachaga wengi tuna kipenda ndio hiki na mie sikonyuma naenda kutambika ha ha ha ha ha ha haya wadau ntawanimiss kwa sikuchache lakini nawatakia sikukuu njema ya cristimass na mwaka mpya hakuna kitakacho haribika nikiwa Marangu home sweet home .


nitakudonoshea habari zote nini kinafanyika kuanzia tunapokuwa huko mpaka tunaporejea so tegemea mengi kutoka kwa sophia kessy
nawapenda sana ila tuko pamoja naamini hilo.
daraja ulionalo ndio la mto wenyewe. Njia ya kulia ndio inayoenda Marangu gate (KINAPA) - huko inapoelekea hiyo pickup.

KWA WAPENDA TATOOO

 TATOO ZA AINA MBALI MBALI ZINACHORWA HAPO BLUE PALACE SALOON SINZA MAPAMBANO
 KINA KAKA HAYAAAA KILA MMOJA SIKUHIZI ANAPENDA KUTOKA KIVYAKE NA TATOO ZA AINA YAKE
 HYO JEE WATAALAM WAKUTOSHA TOKA NDANI NA NJE YA NCHI NDIO WANAOFANYA KAZI HIZO
 CHIPEPEO MGUUNI DAH RAHAAAA
 HAYA WEEE
 KAZI NI KWAKO
WANAKOMAJE????!!!!

Sunday, December 18, 2011

TOA UCHAFU NA SUMU KATKA MWILI WAKO

  maji hapo chini katika picha  huweka katika kifaa maalum ambapo mteja hutumbukiza miguu yake na kisha kuanza kusubiri maajabu hayo ambapo maji yale taratibu kabisa huanza kubadilika Rangi kulingana na wingi wa mafuta na uchafu katika mwili wako ,  





uchafu huo hutoka vyema kabisa na kukuacha mwenyefuraha na afya njema lakini pia endapo maji yatakuwa machafu na kuwa ya kijani (green ) bala ya rangi ya njano kama uonavyo katika picha juu basi wataalam hao hukupa ushauri kwakuwa hali yako kiafya inaonyesha kuwa si nzuri sana.
wataalam hao ni Blue Palace saloon walioko sinza mapambano wanafanya urembo wa kila namna mie nimejionea hayo maajabu kazi ni kwako. IPENDE AFYA YAKO NA KWAKUFANYA ZOEZI HILI HUSAIDIA PIA MWILI KUPUNGUA.