Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, November 27, 2012

MUIGIZAJI SHARO MILLIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI, KUZIKWA KESHO JUMATANO KIJIJINI KWAO LUSANGA

Sharo Milionea katika moja ya pozi zake za Kimilionea enzi za uhai wake.
TANGA, Tanzania

Msiba wa Milionea unakuja siku chache tangu msanii mwingine John Maganga afariki siku tatu zilizopita. Aidha tasnia ya sanaa pia hivi karibuni imempoteza muigizaji kundi la Kaole Sanaa Group Mlopelo, wiki chache baada ya kifo cha mwimbaji mahiri wa taarabu nchini Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ wa TOT

NYOTA wa filamu za vichekesho na Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Hussein Ramadhani Mkiety ‘aka’ Sharo Milionea amefariki dunia jana usiku kwa ajali ya gari, imethibitishwa.

Taarifa rasmi kutoka kwa ndugu wa karibu wa Sharo Milionea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Constatine Masawe, zimethibitisha kutokea kwa  kifo cha Sharo, kilichosababishwa na ajali ya gari katika kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga  ambako ndio nyumbani kwao.......

Taarifa zilizoifikia Habari Mseto kutoka kwa ndugu wa Sharo Milionea, aliyetambulika kwa jina la Snura Mushi, zimepasha kuwa, nyota huyo alikuwa safarini kuytoka SDar es Salaam kwenda kijijini kwao Lusaanga, Muheza mkoani Tanga, kwa ajili ya kusalimia wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.

“Ni kweli Sharo Milionea amefariki dunia jana saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera, Muheza. Alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR, ambalo liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, ambapo mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali Teule ya wilaya ya Muheza.”

Habari Mseto imezipokea taarifa za kifo cha Sharo Milionea kwa masikitiko makubwa, kutokana na mwangaza halisi alioanza kuupata nyota huyo katika tasnia ya filamu na muziki nchini, alikotamba na filamu kadhaa, na nyimbo kali za Bongo Flava ukiwamo wa Chuki Bure aliomshirikisha Dully Sykess.

Msiba wa Milionea unakuja siku chache tangu kufariki kwa msanii mwingine John Maganga, aliyefariki siku tatu zilizopita. Aidha tasnia ya sanaa hiyo pia hivi karibuni imempoteza muigizaji kundi la Kaole Sanaa Group Mlopelo, wiki chache baada ya kifo cha mwimbaji mahiri wa taarabu nchini Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ wa TOT.

Habari zaidi zinapasha kuwa, baadhi ya wasanii waliokuwa nyumbani kwa marehemu Maganga, wakishamaliza kumzika nyota huyo, watasafiri kwa mabasi mawili maalum yaliyotolewa na mdhamini mmoja kuelekea Lusanga kwa ajili ya mazishi ya Sharo yanayotarajiwa kufanyika kesho.

Inna Lillah Wainna Ilaiyh Rajiuuuuun. Mungu ailaze roho ya marehemu Sharo Milionea mahali pema Peponi. Ameen.

Wednesday, November 21, 2012

A DAY TO REMEMBER # NAWASHUKURU SANA WAPIGA KURA WANGU KWA KUFANIKISHA YOTE.

karibu kuendekea kuona picha za matukio mbali mbali ambayo yalifanyika moshi katika chaguzi tofauti za ndani ya chama.
nikiwa miongoni mwa wagombea wa nafasi ya uwakilishi wa UWT kwenda vijana ambapo niliibuka mshindi kwa kishindo sina budi kuwapa shukurani za dhati na za kipekee wapiga kura woote ninacho ahidi ni kuwa nimeamua sasa kazi ni moja wataona kwa matendo na sio maneno.

MKUTANO UKIENDELEA

POZI NIKIWA NA MH BETTY MACHANGU (MB)

 KUJADILI NI MUHIMU SANA HASA KATIKA CHAGUZI MBALI MBALI
 KIONGOZI WANGU
 WAPIGA KURA WANGU

 SIKU MUHIMU SANA YA KUKUMBUKWA

 MMH NAMSHUKURU MUNGU KWA KILA HATUA
 WAPIGA KURA WAKIJADILI
 HAPO SASA
 MAMA YANGU HAKUWA MBALI NA MIE KWA FURAHA KABISA ALINIUNGA MKONO
 ASANTE SANA DADA NA KIONGOZI WANGU PIA KWENYE CHAMA DUME
 WATU TULICHEZA IYENA IYENA WEWEEEE

 MH BETI MACHANGU AKIJADILI JAMBO

 KATIBU WANGU WA UWT DA YUSTA
 MIE NA DADA YUSTER


KIONGOZI WANGU KATIKA POZI.

Tuesday, November 20, 2012

Picha: Aunt Ezekiel na mume wake kwenye harusi ya Dubai


Aunt Ezekiel na mume wake Demonte
Apparently, Aunt Ezekiel aka Rahma amefunga ndoa rasmi huko Dubai. aunt na mume wake huyo aitwaye Demonte.  Hongera Aunt.


Just got married!

Chanzo: Leo bongo 5

Friday, November 16, 2012

Ngisi wa kukaanga

Mahitaji Gramu 250 za ngisi waliolowekwa, gramu 500 za mafuta yaliyopikwa, vitunguu maji, tangawizi, vitungu saumu, chumvi, M.S.G., mvinyo wa kupikia, wanga wa maji na vipande vichache vya matango.   Njia 1. Osha ngisi waliokwishalowekwa, ondoa ngozi, wapasue vipande viwiliviwili kutoka kichwani hadi mkiani. Watandaze kifudifudi kwenye ubao wa kukatia mboga na uwakate katika umbo la fungu la ngano(acha upana wa mm.3 baina ya mikato, kina cha mkato kiwe 3/4 ya maki ya nyama, halafu kata mikato ya mshadhari), na mwisho wakate vipande vyenye urefu wa sm.4 na upana wa sm.2.   2. Pitisha vipande hivyo vya ngisi ndani ya maji yanayochemka na uvitoe kwa mkupuo mmoja ili viviringike.   3. Pasha moto mafuta mpaka yawe na joto la asilimia 80 hivi, tumbukiza vipande vya ngisi ndani ya mafuta na kuvitoa nje mara moja, la sivyo nyama itakuwa ngumu.   4. Tia mafuta kidogo ndani ya sufuria, kisha yapashe moto, mimina mchuzi wenye mchanganyiko wa vitunguu maji, tangawizi, vitunguu saumu, chumvi, M.S.G., mvinyo wa kupikia, wanga wa maji na matango, baada ya mchuzi kuchemka, tia vipande vya ngisi, iepue na iandae tayari kwa kuliwa.

Thursday, November 15, 2012

WATU WAWILI WAFA KWA EBOLA NCHINI UGANDA.

Virusi wa Ebola

Virusi wa Ebola

Wizara ya afya nchini Uganda imesema kuwa watu wawili wameaga dunia kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola.

Waziri wa afya Christine Ondoa amesema, watu wawili kutoka jamii moja waliaga dunia mwishoni mwa juma lililopita, katika wilaya moja viungani mwa mji mkuu Kampala.
Inakadiriwa kuwa watu 17 waliaga dunia magharibi mwa Uganda, kutokana na ugonjwa huo mwezi Julai mwaka huu.

Kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka la Medecins Sans Frontieres (MSF), hakuna maafa yoyote yaliyoripotiwa kuhusiana na ugonjwa huo hatari tangu mwezi Agosti.
Waziri huyo wa Afya ameliambia shirika la habari la AFP, kuwa uchunguzi uliofanywa umethibitisha kuwa watu hao waliaga dunia kutokana na ugonjwa huo wa Ebola katika eneo la Luwero, takriban kilomita sitini kutoka mki mkuu Kampala.

Lakini amesema mwanaume mmoja kutoka eneo hilo, pia aliaga dunia mwezi uliopita, kutokana na kile kilionekana kuwa dalili za ugonjwa huo, lakini hakuna uchunguzi uliofanyika kuhusiana na kifo hicho.
Watu watano ambao ni jamaa wa karibu wa walioaga dunia, wanaendelea kuchunguzwa na madaktari. Wawili kati yao wamelazwa katika chumba maalum katika hospital kuu ya kitaifa ya Mulago mjini Kampala.

Hakuna tiba maalum inayojulikana ambayo inaweza kutumika kutibu ugonjwa huo, lakini wagonjwa hupewa dawa za kawaida za kinga pamoja na zile za kupunguza maumivu na kutibu Malaria ili kuongeza kinga mwilini.

Asilimia Tisini ya watu wanaogunduliwa kuwa na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo wa Ebola huaga dunia, na katika kipindi cha miaka Kumi na mbili iliyopita kumekuwa na visa kadhaa vya mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda.

Takriban asilimia 50 ya yatu 425 ambao walikuwa wameambukizwa virusi hivyo waliaga dunia mwaka wa 2000.

SOURCE BBC NEWS.

FOREVER YOUNG # MAJANGA ... THANK YOU MY LORD STILL DOING GREAT



ASANTE MUNGU KWA KILA HATUA NINAYOIPIGA KATIKA MAISHA YANGU

Tuesday, November 13, 2012

Punda 200 huchinjwa Nigeria kwa matumizi ya chakula na sasa Soko kuu la punda lafungwa


Muuzaji mkubwa  wa Nyama katika soko kubwa la punda nchini Nigeria ametekwa nyara na watu waliokuwa wamejihami.
Polisi wanasema kuwa kutekwa nyara kwa Al-Haji Salisu Yunusa,kumesababisha kufungwa kwa soko hilo ambalo lilijengwa miaka themanini imepita,mjini Ezamgbo.
Takriban punda 200 huchinjwa kila siku katika soko hilo kwa matumizi ya watu.
Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Sylvester Igbo anasema kuwa juhudi zinaendelea za kumtafuta bwana Yunusa.

Mwandishi wa BBC Abdussalam Ibrahim Ahmed, mjini Enugu, anasema kuwa anaelewa watekaji wanataka dola milioni moja nukta 9 kama kikombozi kabla ya kumwachilia mfanyabiashara huyo.

Soko hilo lilifungwa siku ya Jumatatu huku wauzaji wakiandamana kupinga kutekwa kwake.

Hata hivyo lilifunguliwa baadaye huku wauzaji wakihofia kuwa kufungwa kwake kungezua hali ya wasiwasi na kutatiza harakati za kuweza kuokolewa kwa bwana Yunusa.
Uuzaji na ununuzi wa punda na nyama ya punda kumenawiri kama biashara katika soko hilo tangu kufunguliwa kwake miaka themanini iliyopita.


Takriban malori 20 ya punda huletwa katika soko hilo, kila siku.

ISIKILIZE HAPA SEHEMU YA HOTUBA YA YUSUF MAKAMBA CCM DODOMA MUDA MFUPI ULIOPITA.

.


ASANTE SANA MILARD HAYO KWA KAZI NZURI.

NDANDAA KOSOVO ASEMA YEYE NI MKALI KULIKO FM ACADEMIA ILA WAO WAMEMZIDI KWA MKOROGO NA KUVAA WIGI

MWIMBAJI mwenye asili ya Kikongo mwenye wingi wa vituko, Ndandaa Kosovo amesema yeye ni msanii mkali kuliko yeyote yule ndani ya FM Academia na kwamba hata kimataifa bendi yake ya Watoto wa Tembo iko matawi juu kuliko Wazee wa Ngwasuma.
Akiongea na mtandao wa Salut Ndandaa alisema FM Academia ambayo ni bendi yake ya zamani imemzidi kwa vitu vitatu: Kujichubua, kuvaa wigi na kuiba majina ya wanamuziki maarufu.

habari kwa hisani ya salut

MWIMBAJI MELODY AFARIKI DUNIA

MWIMBAJI nyota wa miondoko ya Taarab, Mariam Khamis “Paka Mapepe” amefariki alfajiri ya leo katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili.
Mariam Khamis ambaye hadi anafariki alikuwa ni mwajiriwa wa TOT Taarab alipelekwa Muhimbili kwa ajili ya uzazi na inasemekana mtoto ametoka salama lakini yeye Mungu amempenda zaidii.
Mtu wa karibu sana na mwimbaji huyo, Thabit Abdul ameithibitishia kwa wana SALUT kuwa ni kweli Mariam Khamis amefariki dunia.
Aidha mwimbaji Isha Ramadhan “Mashauzi” naye akiongea na saluti5 kutoka Muhimbili nae alithibitisha kutokea kwa kifo hicho “Ni kweli Mariam amefariki na hivi tunavyoongea tayari tupo hapa Muhimbili” Alisema Isha.
Mariam Khamis alitamba sana na wimbo wa Mapaka Mapepe alouimba akiwa na Melody, kabla ya kujiunga na Zanzibar Stars, Five Stars na hatimae TOT.
Wimbo wake wa kwanza kurekodi na TOT ni Sidhuriki na lawama ambao unatamba sana hadi leo hii
MAZISHI ya mwimbaji Mariam Khamis aliyefariki leo alfajiri yatafanyika kesho, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Baba Mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Sembuli, alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuombwa na Mkurugenzi wa TOT Kapten Komba kufanya hivyo ili wapate kuhudhuria mazishi ya mfanyakazi mwenzao.

TOT wako Dodoma kwa hivi sasa kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi.
Msiba uko nyumbani kwa baba yake mkubwa Magomeni makuti mtaa wa Ndovu Bar.

Mariam Khamis alifariki kwa uzazi baada ya kupata kifafa cha uzazi muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji. Mtoto ametoka salama.

Monday, November 12, 2012

UCHAGUZI WA MWENYEKITI NA MAKAMU KUFANYIKA KESHO

Kutoka kushoto,Mbunge wa Longido, Michael Lekule Laiza, Mh. Wassira na Aden Rage wakiingia kwenye ukumbi wa mkutano wa Kizota ,Dodoma leo.

 

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kwamba uchaguzi wa Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti Bara na Makamu Mwenyekiti Zanzibar  utafanyika kesho tarehe 13 Novemba 2012.
Katika mkutano wake na Waandishi wa Habari,uliofanyika leo asubuhi Kizota mjini Dodoma,Nape alizungumzia kufanikiwa kwa siku ya jana, baada kila kitu kwenda vizuri kwa mujibu wa ratiba.
Pia alizungumzia ratiba ya leo,ambapo kutakuwa na Taarifa mbali mbali za kazi za chama,Taarifa za utekelezaji za ilani ya uchaguzi (Bara na Zanzibar) itasomwa na Waziri Mkuu Mizengo Kayanda Pinda kwa upande wa Tanzania bara na kwa upande wa Tanzania visiwani itasomwa na na Makamu wa Pili Rais wa Zanzibar Balozi Seif Idd.Taarifa kutoka  Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi pia zitasomwa leo.
Akizungumzia mabadiliko ya Katiba,alisema kumekuwa na mafanikio sana baada ya mapendekezo yote kupitwa bila kupingwa,moja ya mapendekezo ni kuwepo kwa Baraza la Ushauri la Wazee, pamoja kubariki mapendekezo wajumbe wa halmashauri kuu ya Taifa watoke wilayani.
Baada ya uchaguzi kutakuwa na mrejesho wa mijadala na kutoa maazimio ya Mkutano Mkuu.

MATUKIO YA MKUTANO MKUU WA NANE WA CCM KATIKA PICHA

Asha Baraka akiwa ndani ya banda la gazeti la Uhuru kwenye viwanja vya Kizota Dodoma.


Viwanja vya Kizota vikiwa vimefurika wajumbe na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi


Biashara  za aina nyingi zikiwa zimetanda kila kona.


Ukumbi ukiwa umefurika wananchama na wajumbe wa Chama.

Waalikwa kutoka vyama vya upinzani.


Wajasiriamali hawakuwa nyuma kuuza bidhaa zao, Mkutano Mkuu wa nane wa CCM ulioanza leo umefungua fursa pekee kwa wafanyabiashara wadogo wadogo.


Huduma za vyakula vya aina zote zinapatikana Kizota,eneo ambalo CCM inafanya Mkutano Mkuu wa nane.


Wajumbe kutoka Mbeya wakionyesha ukakamavu wao kwenye ukumbi wa Mkutano Kizota leo.

VIONGOZI 5 WA CHADEMA WAHAMIA NCCR MAGEUZI JIMBO LA BUSANDA‏

Chama cha  Demokrasia na maendeleo Chadema Kata ya Katoro Jimbo la Busanda mkoani geita kimepata pigo kubwa  baada ya vigogo 5 kuhamia chama cha NCCR mageuzi  akiwemo mjumbe wa serikali ya kijiji na alie kuwa  mwenyekiti wa jimbo hilo huku wanachama wapya  117 wakijiunga katika chama hicho.
 
Viongozi hao waliokihama chama hicho ni pamoja na Elikana Sono aliekuwa mwenyekiti wa jimbo la Busanda kupitia chama cha Demokrasia na maendeleo  Chadema  kwa kipindi cha mwaka 2009 na 2010,katibu mwenezi kata ya Nyamigota ambae pia alikuwa mjumbe wa serikali ya kijiji cha Chibingo Lugambwa Silva,Khanifa Gervas ambae ni mke wa Diwani wa kata ya Katoro (CHADEMA) wengine ni Evodia Phiribert aliyekuwa mwenyekiti wa akina mama jimbo la Busanda  na Flora Raphael ambae alikuwa  katibu wa  akinamama jimbo la Busanda wote wakitokea chama cha Demokrasia  CHADEMA.
 
Viongozi hao wametangaza rasmi kukihama chama hicho mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya setelait mjini Katoro,wakati makamu mwenyekiti wa NCCR MAGEUZI Taifa Maltini Danda juju akiwahutubia  mamia ya wananchi wa mji huo majira ya saa kumi jioni.
 
Wakielezea sababu ya kukihama chama hicho viongozi hao wamesema kuwa chama cha Chadema katika kata ya Katoro kwa sasa kinatuhuma kubwa ya ufisadi suala ambalo ni kinyume na katiba ya chama hicho kinachokemea vikali ufisadi, pamoja baadhi ya viongozi kutokukubali kukosolewa na badala yake wanataka kufanya mambo kwa matakwa yao.
 
 
Aidha katika hatua nyingine makamu mwenyekiti wa NCCR mageuzi Juju amewataka wananchi kabla ya kujiunga na chama chochote wanatakiwa kujua historia, kupima sera na itikadi ya chama kwani asilimia kubwa ya wananchi wanaojiunga kwenye vyama mbalimbali hawaangalii mambo hayo ambayo ni ya msingi kwani wakijua nchi ya Tanzania itakuwa na maendeleo makubwa,na ufisadi katika nchi utakuwa ni historia kwa vizazi vijavyo.
 
Pia amekemea vikali tabia ya baadhi ya wanasiasa kununua kura kutoka kwa wanachama mara pale wanapogombea nyadhifa mbalimbali,kwani hali hiyo inalijenga mazingira ya rushwa Taifa hali hiyo ambayo itaendelea vizazi na vizazi.
 
HABARI NA ESTER SUMIRA GEITA.

KAMPENI YA MAMA MISITU YAZINDULIWA PWANI.‏

Kampeni ya mama misitu imezinduliwa rasmi katika kijiji cha Kisanga tarafa ya Sungwi wilayani Kisarawe, ikiwa na lengo la kuhamasisha jamii kuwa na ufahamu kuhusiana na masuala ya utunzaji wa mazingira na umuhimu wake katika kupunguza hewa ukaa.
 
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hizo Mratibu wa BW. YAHYA MTONDA ambaye amesema lengfo kuu la kampeni ya mama misitu, ni kupeleka suala la utawala bora katika suala la uhifadhi wa misitu kwa jamii ili kuweza kuwa shirikishi kwa jamii kushiriki moja kwa moja katika kuilinda na kuitunza misitu ya RUVU Kusini.
 
BW. MTONDA ameongeza kuwa kwa kampeni hiyo ni kuleta mageuzi chanya katika suala uhifadhi wea misitu na kupunguza uvunaji haramu wa mazao ya misitu sawa na kuhakikisha wanajamii wanaoishi maeneo yaliyozunguka misitu wanafaidika kwayo.
 
Amesema katika suala zima la kuwepo kwa utawala bora, halmashauri za wilaya na vyombo vinavyosimamia sherian kwa kuwapatia elumi kuhusiana na utawala bora katika suala zima la uhifadhi wa misitu.
 
BW. MTONDA amebainisha kuwa kampeni hiyo inatekelezwa na washirika wenza 11, ambao wamegawanyika katika makundi mawili ya Taifa na wilaya katika ngazi ya taifa moja wapo ni MJUMITA Trafiki maalum ambao wanakusanya shughuli mbalimbali kuhusiana na suala misitu, POLICY FORUM, LEAT, HEMINA na wengineo.
 
Na katika ngazi ya wilaya utekelezaji unasimamiwa na shirika la kuhifadhi misitu ya asili Tanzania,katika wilaya za Rufiji na Kibaha kwenye msitu wa Ruvu kusini ambapo WSSP wanasimamia misitu ngazi ya wilaya ya Kisarawe, Mradi wea mama misitu unatarajiwa kutekelezwa katika kipindi cha miaka 5.

Sunday, November 11, 2012

CCM yamrudisha tena kwenye medani za siasa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho JAPHET PHILLIP MANGULA

 
 
Hatimaye Chama Cha Mapinduzi CCM kimemrudisha tena kwenye medani za siasa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama hicho  JAPHET PHILLIP MANGULA baada Kamati Kuu ya Chama hicho iliyoketi jana Mjini Dodoma kupitisha jina lake kugombea nafasi ya Makamu wa Mwenyekiti CCM Taifa Bara.
 
Kwa uteuzi huo  MANGULA sasa ataungana na Rais JAKAYA KIKWETE ambaye amepitishwa kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa chama hicho taifa huku Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi DK ALLI MOHAMED SHEIN akipitishwa kuwa makamu Mwenyekiti Zanzibar.
 
Akizungumza Mjini Dodoma Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi amesema, chama chake kimeamua kumrudisha MANGULA ili kukiongezea nguvu huku ikirejea dhana yake ya kuwafikia wakulima na wafanyakazi.


Katika hatua nyingine NAPE ametangaza mabadiliko ya ratiba ambapo kwa sasa uchaguzi wa Halmashauri Kuu ya Taifa viti kumi bara na viti kumi Zanzibar utafanyika leo na mkutano
kutarajiwa kumalizika Novemba 13 mwaka huu.



Mkurugenzi mkuu wa shirika la BBC, George Entwistle, amejiuzulu.

George Entwistle ajiuzulu kama Mkurugenzi BBC

Taarifa hiyo kwa makosa ilimshutumu aliyekuwa Waziri wa Fedha wakati wa serikali ya Conservative , Lord McAlpine, kwamba alihusika katika kashfa ya kudhalilisha watoto.
Tayari shirika la BBC limekuwa likichunguzwa vikali katika kashfa inayomhusu mtangazaji wake wa zamani Jimmy Savile kwa madai ya kuwadhalilisha watoto.

Kipindi hicho cha Newsnight kinadaiwa kuacha kwa makusudi kutangaza habari ya uchnguzi kuhusiana na kashfa ya Bwana Savile.
Wakati wa kutangaza kujiuzulu Jumamosi,usiku Bwana Entwistle alisema "ilikuwa ndilo jambo la heshima kwangu kulifanya".

Akisimama kando yake Mwenyekiti wa BBC Trust, Lord Patten alisema " huu ulikuwa moja wapo ya usiku wa majozi katika maisha yangu ya umma".
"Muhimu kwa BBC ni jukumu lake kama chombo cha habari kinachoaminika"
"Kama Mhariri Mkuu wa shirika hili la habari, kwa heshima kubwa George amehiari kujiuzulu kutokana na makosa yasiokubalika - uanahabari mbovu ambayo umezua malalamiko mengi".

HABARI KWA HISANI YA BBC

Friday, November 9, 2012

President Barak Obama made a surprise visit to campaign HQ yesterday to thank staff & volunteers



na hii ni mara baada ya kuchaguliwa kuwa Rais Barak Obama akafanya ziara ya ghafla kutoa shukurani kwa waliompigia kampeni . unaeza kuacha maoni yako waonaje hii. niwatakie Ijumaa njema na weekend njema

"Rushwa inaitafuna China"

Rais Hu Jintao akitoa hotuba wakati akifungua mkutano wa 18 wa chama tawala cha Kikomunisti siku ya Alhamis, unaotarajiwa kuidhinisha viongozi wapya kwa muongo ujao. Rais wa China anayemaliza muda wake Hu Jintao, ameonya kuwa rushwa inatishia mustakabali wa chama tawala cha kikomunisti na taifa hilo kwa ujumla, huku akiahidi mageuzi wakati akifungua mkutano mkuu wa chama hicho.
 
Mkutano huo wa wiki nzima na unaotizamiwa kutetua viongozi wapya wa chama na taifa, unahudhuriwa na wajumbe elfu mbili waliyokusanyika katika ukumbi wa Cavernous mjini Beijing, na unafanyika huku kukiwa na machafuko ya kijamii na hasira za umma dhidi ya kuongezeka kwa vitendo vya rushwa, na pengo linalozidi kupanuka kati ya walicho nacho na wasiyo nacho.

"Kama tutashindwa kushughulikia suala larushwa vizuri, linaweza kkusababisha kuanguka kwa chama na taifa kwa ujumla. Mageuzi ya mifumo ya kisiasa ya chama ni muhimu kama sehemu ya mageuzi ya ujumla ya China. Laazima tuendelee kufanya juhudi za maksudi kugeuza mfumo wa kisiasa, na kupanua demokrasia kwa vitendo," alisema rais Hu.

habari kwa hisani ya DW