Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Sunday, March 15, 2015

Maadhimisho ya 27 ya Wiki ya Maji Kitaifa

Wizara ya Maji yaadhimisha Maonesho ya 27 ya Wiki ya Maji Kitaifa yatakayofanyika kuanzia tarehe 16-22 March, 2015 katika Viwanja vya Mkendo mjini Musoma. Kauli mbiu ni "Maji kwa Maendeleo Endelevu"

TUBURUDIKE NA WIMBO WA LOKUA KANZA AKIWA NA FALLY IPUPA

Miongoni mwa wanamuziki wanao heshimika na kupendwa sana barani Afrika Lokua Kanza akimshirikisha Fally Ipupa katika wimbo huu hebu tazama.

SHABIKI NAMBA MOJA WA KOFII OLOMIDE MWANAMAMA KISI NDJORA WAKATI ALIPOACHIWA HURU.



Hatimae KISI NDJORA yuu huru baada yakupewa msaada kutoka kwa mawakili wa koffi olomide.
JB MPIANA ndie aliekua wakwanza kumfungulia mashitaka kisi ndjora kwakosa la kumpakazia mambo yasiokua na ukweli wowote, baada ya kutafakari, jb mpiana kupitia mawakili wake, kaiomba mahakama jijini kinshasa imfutie kisi ndjora kesi.

Wakati akiachiwa huru kutokana na kesi ya JB MPIANA, fally ipupa kwaupande wake, kaja pia kumfungulia mashitaka kisi ndjora,kashutumiwa kosa la kumtukana , kumtishia maisha fally ipupa…

Izingatiwe yakwamba katika mzozo ulioko kati YA JB MPIANA na KOFFI OLOMIDE, kisi ndjora yeye ni mpambe namba moja wa koffi olomide, kwakutaka kumuumiza zaidi jb mpiana, kamtupia khashfa mbaya kwakusema, alimuharibu mmoja kati ya wanenguaji wake na kumpa mimba , binti anaejulikana kwa jina la ” mwanatsuka ” ambae kiumri bado mdogo chini ya miaka 16.


Ingawa kisi ndjora anao muonekano wakiume, bali ni mwanamke na anaishi na mwanaume, ana watoto hadi wajukuu!!!
Kwa hisani ya sport na starehe. By Pius

ASANTE KWA MIAKA 10 YA UTUMISHI # AMBULANCE ALIYOITOA MBUNGE ZITTO KABWE MARCH 14 JIMBONI KWAKE.

691ztkbwMbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe leo March 14 ametoa gari mpya ya kubebea wagonjwa (Ambulance)kama moja ya ahadi zake alipokuwa kwenye kampeni ambapo aliahidi kabla ya kumaliza kipindi cha uongozi wake atatoa gari hiyo.
679ztkbwWakipokea msaada huo Michael Mwandezi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kigoma pamoja na Hamis Said Betese ambaye naye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambapo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Nyarubanda ambao ndio msaada huo wamemshukuru sana Mbunge Zitto Kabwe.
688ztkbwHata hivyo kabla ya kuelekea kukabidhi Gari hiyo ya kubebea wagonjwa,Zitto Kabwe aliwatembelea Wanachama wa Chama cha Ushirika Rumaco ambao wanajishughulisha na kilimo cha Kahawa kutoka kijiji cha Matyazo Kigoma Kaskazini.
656ztkbw
532ztkbw
452ztkbw
449ztkbw
419ztkbw
447ztkbw
387ztkbw
356ztkbw
39ztkbw
71ztkbw
120ztkbw
203ztkbw
88ztkbw
 PICHA NA HABARI KW AHISANI YA MILLARD AYO BLOG.

Thursday, March 12, 2015

WATOTO, VIJANA, WATU WAZIMA NA HATA WAZEE WAKO HATARINI KUKUMBWA NA TATIZO LA FIGO



Ni wakati wa jioni wanaonekana Vijana zaidi ya Watano wakisikiliza Redio, mara linasikika tangazo linalohamasisha upimaji wa afya zao, wote wanapuuza na mmoja wao anabadilisha kabisa stesheni na kutafuta nyingine.


Baada ya wiki kupita mmoja wa Vijana hao ghafla hali ya mwili wake inaanza kubadilika anahisi uchovu muda wote, na miguu yake kuvimba hivyo wanalazimika kumkimbiza hospitali.

Kutokana na kutojenga utamaduni wa kupima afya zao, mara baada ya vipimo anabainika kuwa na tatizo la figo lakini kibaya zaidi Daktari anawajuza kuwa tatizo la rafiki yao ni kubwa zaidi kutokana na kuchelewa kubainika.
Hali hiyo ndiyo inayoelezwa kuwakumba Wagonjwa wengi wanapelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi… 

Tatizo la figo linaelezwa kuendelea kuwa kubwa nchini ambapo kwa wiki katika Hospitali hiyo pekee wanapokea wagonjwa kuanzia 8 hadi 10.
Watoto, Vijana, watu wazima na hata Wazee wako hatarini kukumbwa na tatizo hilo.

Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), idadi ya vifo vitokanavyo na magonjwa ya figo nchini imefikia 4533 sawa na asilimia1.03  ya vifo vyote, wakati kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa figo kimeripotiwa kuwa asilimia 14 .

TAASISI YA LISHE TANZANIA YASHITUSHWA NA UDUMAVU MKUBWA WA WATOTO SIMIYU



Taasisi ya lishe tanzania imeshitushwa  na asilimia 42 za  takwimu
za udumavu  kwa watoto walio chini ya miaka mitano na hivyo ni sababu mojawapo inayochangia baadhi ya watahiniwa wa darasa la saba kutofanya vizuri katika  mtihani wa taifa mkoani simiyu.  

Akitoa elimu ya uhamasishaji ,kwa wawakilishi wa wakurugenzi wa halmashauri   ,maafisa mipango na waganga wakuu mkoani simiyu , afisa lishe wa mkoa wa iringa ambaye ni mwezeshaji mshauri kwa viongozi ngazi ya mikoa  na halmashauri mwita waibe amesema kuwa huu ni   mkakati wa kitaifa wa utoaji  elimu nchi nzima,ikiwa ni kutekeleza agizo la rais jakaya kikwete ambalo kimsingi alitoa agizo kuwa ,viongozi wote wapewe elimu ya lishe ili kuwajengea uelewa wa namna ya kusukuma masuala ya lishe ambayo yanaliathiri taifa ambapo   kati ya watu ,100,42 wamedumaa.

Katika mjadala huo wa lishe mganga mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa bariadi dr godfrey MPANGALE akazitupia lawama mamlaka ya chakula na dawa TFDA NA shirika la viwango Tanzania tbs kwa kushindwa kudhibiti bidhaa ambazo hazina na ubora na kuleta madhara kwa watumiaji bidhaa hizo.

Naye katibu tawala wa mkoa wa simiyu mwamvua jirumbi amewataka watendaji kuwajibikaji kwa kila mmoja kwa nafasi yake ili kuweza kulitokomeza tatizo la udumavu lililofikia asilimia 42 .