African music is on my blood Back to my root Proud to be Africa,be your self #lets talk about African culture,tourism music ,life style, business,technology, money, fashion, Love, Marriage, Health, food, animals,and so on!!!!
Thursday, February 28, 2013
Monday, February 25, 2013
MENO 18 YA TEMBO YAKAMATWA MOROGORO
Vipande 18 vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi milioni ishirini na tisa laki saba sabini na sita elfu vimekamatwa kwa ushirikiano wa jeshi la polisi mkoani Morogoro na hifadhi ya Udzungwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia mwema huku wahusika waliokuwa wakisafirisha nyara hizo kutelekeza gari vilivyokuwamo vipande hivyo
(picha kutoka maktaba)
Akizungumza na Clouds Fm kamanda wa jeshi la polisi mkoani Morogoro Faustine Shilogile amesema kuwa tukio hilo lilitokea februari 23 mwaka huu majira ya saa saaa 11:00 jioni katika eneo la la Mto Mwaya Mang’ula wilayani Kilombero ambapo askari polisi walipata taarifa ya kuwepo gari lenye namba T 557 AYR aina ya Toyota mark II yenye rangi ya kijivu ikiwa na watu wawili ndani iliposimamishwa watu hao walishuka kwenye gari na kukimbilia porini huku wakilitelekeza gari hilo ambalo ndani yalikuwamo meno hayo.
Naye mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Udzungwa Vitalis Uruka amesema kuwa vipande hivyo vya meno ya tembo vinadaiwa kupatikana maeneo ya Ifakara au Mahenge na ni tukio la muda mrefu na kwamba wwatatumia gari hilo lililotelekezwa na watu hao kuwapata wahusika
PICHA ZA MSIBA WA GOLDIE, MUME WAKE NA WENGINE WALIOHUDHURIA.
Wa pili kutoka kushoto ni mtangazaji wa Channel O Denrele Edun ambae alikua rafiki mkubwa wa Goldie na ndioGoldie alifia mikononi mwake akiwa amembeba, huu msiba ulihudhuriwa na watu wachache walioalikwa tu huko Ikoyi Lagos Nigeria.
Imeripotiwa kwamba manenoya mwisho ya Goldie yalikua ni kumuomba baba yake amuombee apone maumivu makali ya kichwa aliyokua nayo ambapo Daily Post wameripoti tena kwamba staa huyo alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali, foleni ya magari siku hiyo ya wapendanao ilichangia kuchelewa kufika hospitali.
Chanzo mojawapo cha kifo chake ni shinikizo la damu na maradhi ya moyo.
HABARI HII KWA HISANI YA MILARD AYO BLOG.
Wednesday, February 20, 2013
IDHAA YA KISWAHILI YA DW YATIMIZA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWAKE.
Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle leo inaadhimisha miaka 50 tangu ilipoanzishwa na kuanza kurusha matangazo yake tarehe 1 Februari 1963 na kusikika katika maeneo ya Afrika Mashariki na Kati.
(Nikiwa pamoja na Adrea Schmidt ambae ni mkuu wa idhaa ya kiswahili wa Radio (DW) Deutshche Welle mara baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo 20/2/2013 katika ukumbi wa umoja house hapa jijini Dar es saalam. )
Deutsche Welle inaadhimisha miaka 50 ya idhaa yake ya Kiswahili
chini ya maudhui ya “Maarifa na Mwamko“ katika hafla maalumu itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Kwa nusu karne, Deutsche Welle (DW) imekuwa ikitangaza taarifa na habari
za uhakika kwa lugha ya Kiswahili kwa ajili ya wasikilizaji kwenye maeneo ya
Mashariki mwa Afrika na eneo la Maziwa Makuu.
Tarehe 22 Februari, saa 9.oo mchana katika jengo la Makumbusho ya Taifa, DW itasherehekea
maadhimisho haya kwa hafla maalumu jijini Dar es Salaam, Tanzania, ikiwaleta
pamoja wachambuzi wanaoheshimika katika mjadala wenye maudhui ya
“ Maarifa na Mwamko kupitia Vyombo vya Habari“.
Hotuba maalumu zitatolewa kwa lugha ya Kiingereza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter Brandes, na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt.
“Idadi kubwa ya wasikilizaji wanaoishi hapa Tanzania, kwa hivyo lilikuwa chaguo la uhakika kwa ajili ya sherehe zetu,“ alisema Andrea
Schmidt. “Kwa miaka 50 iliyopita, DW imejitolea katika utoaji wa habari
zenye uwiano na taarifa za uhakika, ikiwapa watu wa Afrika ya Mashariki
habari na uchambuzi wa kina juu ya masuala yenye uzito mkubwa.“
Uchambuzi utafanywa na jopo la majadiliano lililotayarishwa kwa msaada
wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) ofisi ya Dar es Salaam na
utafanywa kwa lugha ya Kiswahili. Mohammed Khelef wa DW ataongoza
majadiliano hayo akiwa na wataalamu wa vyombo vya habari wanaoheshimika
nchini Tanzania, akiwemo Assah Andrew Mwambene (Mkurugenzi
nikifuatilia kwa umakini kabisa mkutano huo
Tuesday, February 19, 2013
RAIS KIKWETE AKUTANA NA WANACHAMA WA SIMIYU COMMUNITY BANK LEO IKULU
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam, kumwelezea mipango ya kufungua benki hiyo itayoshirikisha jamii katika mkoa huo mpya na ya jirani katika azma ya kumkomboa mjasiriamali na mkulima
mdogo.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na wajumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam
KANISA LA CHOMWA MOTO VIZIWANI ZANZIBAR
SIKU TATU TU ZIMEPITA BAADA YA PADRE KUUWAWA -'KANISA JINGINE LA POOL OF SILOAM LACHOMWA MOTO VISIWANI ZANZIBAR' ( TUNAELEKEA WAPI? AMANI IPO WAPI? WATU WANAOGOPA HATA KUSALI MAKANISANI SIKU HIZI UNAPOTOKA HUNA UHAKIKA WA KURUDI NYUMBANI UKIWA SALAMA EEH MWENYEZI MUNGU TUSAIDIE WAJA WAKO.)
Monday, February 18, 2013
SAFARI YA KISIWANI MBUDYA ILIVYOKUWA
SORRY FRIENDS I HAVE BEEN SO BUSY WITH STUDIES AND WORK NDIO MAANA NACHELEWA KUWEKA PICHA ZA MATUKIO KISIWANI MBUDYA PLZ NAOMBA MNIVUMILIE WHEN I GET TIME SOON WILL PUT MORE PICS NA HABARI ZAIDI LOVE YOU ALL ENJOY.
dogo langu merry kessy na yeye alijumuika na ma single girls kuenjoy kisiwani mbudya
hapa tukielekea kufuata boti kubwa inayoonekana pichani chini
baba jonii hakukosekana Adam Mchomvu na yeye yumo
misosi pia ilikuwepo
aah mie nikapozi kupata upepo
kimodo nae muoga ndani ya life jacket
waliobaki wali lala kisiwani humo
raha jipe mwenyewe ukisubiri kupewa utazeeka bila kuzipata
sitii neno hapo kilaji
kisiwa cha ukweli
mtu na dada yake
PICHA ZAIDI NIKIPATA TU TIME NITAZIWEKA THANKX