Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, October 22, 2012

Zuma akadhibisha madai ya gazeti la Economist

Zuma akadhibisha madai ya gazeti la Economist
Rais wa Afrika Kusini amekadhibisha habari kuhusu uchumi wa nchi hiyo zilizochapishwa na gazeti la kila wiki la Economist la huko Uingereza. Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini ametoa radiamali katika kujibu taarifa zilizoandikwa na gazeti la Economist la Uingereza kwamba ufisadi na uongozi mbaya unatawala katika safu ya uongozi wa Afrika Kusini.  Rais Zuma amesema madai ya gazeti hilo ni ya urongo na kwamba hayana usahihi wowote. Rais wa Afrika Kusini amesisitiza kuwa habari iliyoandikwa na gazeti la Economist kuwa uchumi wa Afrika Kusini unaporomoka kwa sababu ya ufisadi na uongozi mbovu miongoni mwa viongozi wa nchi hiyo si sahihi.

kwa hisani ya Iran radio.

Friday, October 12, 2012

Wanawake kurithi Mali Botswana


Wanawake wamekuwa wakinyimwa nafasi ya kurithi Botswana
Mahakama kuu nchini Botswana imebatilisha sheria ya kitamaduni ambayo iliwazuia wanawake kurithi mali nyumbani.

Mahakama imesema kuwa kanuni hiyo ya kitamaduni inakiuka sheria ya katiba inayosisitiza usawa kwa wanaume na wanawake.

Mwandishi wa BBC mjini Gaborone, anasema kuwa uamuzi wa jaji Key Dingake, sasa inaileta katika safu moja sheria ya utamaduni na katiba ya nchi.

Alisema kuwa lazima pawepo usawa kati ya wanawake na wanaume kuhusiana na swala urithi.

Thursday, October 11, 2012

TCCIA) mkoa wa Pwani yakabiliwa na changamoto ya wafanyabiashara wake kukosa masoko ya kuuzia bidhaa.

CHAMA cha wafanyabiashara,Wenye viwanda na wakulima (TCCIA) mkoa wa Pwani kinakabiliwa na changamoto ya wafanyabiashara wake kukosa masoko ya kuuzia bidhaa zao hali inayosababisha kushindwa kulipa ada kwa wakati na kusababisha chama hicho kuyumba.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mkutano mkuu wa chama hicho ,Mwenyekiti wa Chemba hiyo ya TCCIA Mkoa,Bi Kasa Mlonja amesema ukosefu wa soko la uhakika unapelekea wafanyabiashara hao kushindwa kuuza bidhaa zao kwa uhakika.

Alisema wapo wafanyabiashara wao ambao wamefanikiwa katika soko lakini kati ya hao ni wale waliopata nafasi ya kuuza bidhaa zao nchi jirani na katika maonyesho mbalimbali.

"Mji wa kibaha upo njiani lakini malighafi zimekuwa zikipatikana Jijini Dar es salaam hali inayosababisha kutumia kipato kikubwa katika usafirishaji," alisema Bi Mlonja.

Aidha alisema japo hali ya kimapato haikidhi mahitaji ya wanachama wake lakini haina budi kuwaomba wanachama hao kulipia ada kwa wakati ili chemba hiyo iweze kusimama .

Hata hivyo Bi Mlonja alisema serikali mkoani humo imewahakikishia kuwepo kwa soko la kisasa hivi karibuni ingawa muda wa utekelezaji wa soko hilo haujawekwa wazi.

Akizungumzia suala la hisa amewaomba wanachama hao kijumla kununua hisa za TCCIA Investment Company ili hali kukuza mitaji yao .
Uongozi wa chama hicho unamaliza uongozi wake hivyo wanachama wamewekwa sawa kujipanga tayari kwa uchaguzi utakaofanyika April mwaka 2013.

 
Na John Gagarini,Kibaha

SIKU YA MAAFA KUADHIMISHWA OCTOBER 12/ 2012.‏ WAZIRI MKUU KUTOA TAMKO.

 

Tarehe 12 Oktoba, 2012 ni Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji wa Athari za Maafa (International Day for Disaster Reduction). Siku hii huadhimishwa tarehe 13 Oktoba ya kila mwaka.
Hata hivyo, kwa mwaka huu Sekretariati ya Kupunguza Athari za Maafa ya Umoja wa Mataifa, imeelekeza kuwa siku hii iadhimishwe siku ya Ijumaa Oktoba 12, 2012.

Kama ilivyo kwa miaka yote tangu siku hiyo ilipoanzishwa katika miaka ya 1990, Sekretarieti hiyo hutoa Kaulimbiu ya mwaka husika. Kaulimbiu ya mwaka huu inasema, WANAWAKE NA WASICHANA – NGUVU ISIYOONEKANA KATIKA KINGA DHIDI YA MAAFA” (WOMEN AND GIRLS –THE INVISIBLE FORCE OF RESILIENCE).
Siku ya Kimataifa ya Upunguzaji wa Athari za Maafa kwa mwaka huu imewalenga Wanawake na Wasichana kwa lengo la kutambua na kukubali mchango unaotolewa katika jamii na mamilioni ya Wanawake na Wasichana katika kukabili athari za maafa na Mabadiliko ya tabia nchi na hivyo kuleta manufaa katika shughuli za maendeleo na uwekezaji.

PAKA AWA MEYA KWA ZAIDI YA MIAKA 15 HUKO ALASKA.



kuna mji mmoja nchini Alaska ambao umemfanya paka kuwa MEYA wa Mji huo kwa miaka 15.

cat mayor
paka huyo aliepewa jina la Stubbs amekuwa MEYA wa Talkeetna, huko Alaska kwa takriban muda wa maisha yake yote  na hii sio utani.


Imekuwa ni kwa zaidi ya muongo sasa katika mji mdogo wa utalii wenye wakazi takriban 900.
 
paka huyo alipewa uheshimiwa huo wa UMEYA mara baada tu ya kuzaliwa kwake na mpaka sasa wananchi wa eneo hilo wanafahamu fika kuwa paka aitwae "Stubbs  huyo ndio MEYA.



"paka huyo amekuwa akiandikwa katika  majarida kadhaa huko Alaska, na amekuwa featured katika mambo kadhaa tofauti," alisema Lauri STEC, ambaye anafanya kazi katika Hifadhiya Nagley na ni Mkuu katika hifadhi ya Talkeetna, ambapo Stubbs ndipo anapoishi .

ilikuwa kama hadhithi ambapo, miaka 15 iliyopita wakazi wa mji huo hawakupenda wagombea ambapo inadaiwa kuwa watu wengi walikuwa  wanakimbia kwa meya wa Talkeetna, hivyo kama utani utani tu wakachoshw ana tabia hizo na kuhamasishana watu na kweli , wakahamasika vya kutosha na kisha  kumchagua Stubbs paka kama  awe mgombea  na kweli lengo likatimia na yeye kweli paka huyo  alishinda.

kwa Sasa, zimekuw ani shukurani kw amji huo kwakuwa  meya paka Stubbs, amekuwa akipata viongozi mbali mbali nna wageni ambao wamekuwa wakitembelea eneo hilo hasa majira ya joto kufurahi na  kujione ilivyo.

Wednesday, October 10, 2012

A picture is worth a thousand words.











NOTHING TO SAY BUT I LOVE THE CAR I WISH TO HAVE THIS ONE ONE DAY YES.

MAUAJI TANGA YAMKOSESHA MKUU WA MKOA USINGIZI‏

SERIKALI ya Mkoa wa Tanga imesema kwamba itafanya kila liwezekanalo kuhakikisha inakomesha vitendo vya mauaji ya raia vinayoendelea kutokea katika jiji la Tanga kutokana na imani za kishirikina, wivu wa kimapenzi pamoja na ujambazi .
 
Jumla ya watu 11 wameripotiwa kuuwawa kikatili katika kipindi cha kuanzia Septemba moja hadi 28 mwaka huu kufuatia imani za kishirikina,kujichukulia sheria mkononi, vivu wa kimapenzi pamoja na ujambazi.
 
Oktoba 8 mwaka huu mlinzi wa kampuni ya Mult System naye ametekwa na haijulikani alipo hadi sasa wakati akilinda katika ofisi za Halimashauri ya Wilaya ya Mkinga.
 
Baada ya kutekwa majambazi hayo yalifanikiwa kuiba gari aina ya Lendcuiser lenye namba za usajili STK 7446 tukio ambalo lilidhibitishwa na kamanda wa polisi mkoa wa Tanga Bw.Costantine Massawe.
 
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga hakutaka kutaja jina la mlinzi aliyetekwa kwa sababu za kipolisi.
 
 
Akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kukithiri kwa mauaji hayo,Mkuu wa Mkoa wa Tanga Luten Mstaaf Chiku Galawa amesema jeshi la polisi kwa ujumla halijashindwa kukabiliana na mauaji hayo ambayo amesema yanautia doa Mkoa wake.
 
 
Mkuu huyo wa Mkoa amesema ameliagiza jeshi la polisi kuimarisha doria na kushughulikia taarifa za uhalifu zinazotolewa na wananchi ili vitendo vya mauaji viweze kuwa historia badala ya kuendelea kushamiri.
 
Hata hivyo katika kushughulikia swala hilo,ni mtu mmoja tu aliyekamatwa katika tukio linalohusishwa na imani za kishirikina huku wangine wakiendelea kutafutwa na jeshi la polisi ili wachukuliwe hatua za cheria.
 
Wakati huo huo Mkuu huyo wa Mkoa ameagiza watendaji wa serikali wa mkoa huo kuhakikisha wanapiga vita tabia ya baadhi ya jamii inayopenda kushinda vijiweni na kushindwa kushiriki katika shughuli za uzalishaji.

SIKU YA MACHO DUNIANI‏

                                          JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII



TAARIFA KWA UMMA
MAADHIMISHO YA SIKU YA AFYA YA MACHO DUNIANI
TAREHE 11 OKTOBA 2012
 

Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inaadhimisha Siku ya Afya ya Macho Duniani ambayo huadhimishwa duniani kote kila Alhamisi ya pili ya mwezi Oktoba ya kila mwaka kwa lengo la kuhamasisha jitihada za kutokomeza upofu unaozuilika duniani.
Mwaka huu siku hii itaadhimishwa tarehe 11 Oktoba 2012 katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
Kauli mbiu ya Siku ya Afya ya Macho Duniani kwa mwaka 2012 ni; “AFYA BORA YA MACHO NA MAENDELEO YA TAIFA” Sambamba na kauli mbiu hii, ujumbe mahususi kwa wadau wa Afya ni; “AMUA KUWEKEZA SASA KATIKA HUDUMA ZA MACHO, UEPUSHE GHARAMA ZA ULEMAVU WA KUONA”
Kauli mbiu hii inatoa msisitizo na kuonyesha umuhimu wa wananchi kuwa na afya bora ya macho, ili waweze kushiriki vema katika shughuli za maendeleo. Aidha, ujumbe mahususi unalenga wadau wa Afya ili waelekeze juhudi zaidi na kutoa kipaumbele katika kuboresha huduma za macho nchini.
Azimio la Dira 2020 ya Kutokomeza Upofu Unaozuilika ifikapo mwaka 2020 na Siku ya Afya ya Macho Duniani
Maamuzi ya kuadhimisha Siku ya Afya ya Macho Duniani yalifikiwa na Lions Club International Foundation mnamo mwaka 1998, na baadae kuungwa mkono na wadau wengine wa Huduma za Macho ambao ni pamoja na Muungano wa mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa, Serikali , wataalamu wa masuala ya afya, taasisi mbalimbali na watu binafsi.
Dira 2020 ni Azimio la Kutokomeza Upofu Unaozuilika Duniani ifikapo mwaka 2020. Azimio hili linasisitiza juu ya upatikanaji wa haki ya kuona kwa kila binadamu duniani.
Serikali ya Tanzania imeungana na mataifa mengine duniani katika azimio hili mnamo tarehe 23 Mei 2003.
Malengo ya Dira 2020 ni pamoja na:-
  • Kuinua uelewa wa wadau juu ya sababu za upofu unaozuilika na njia mbalimbali  zinazoweza kutumika ili kusaidia kutokomeza hayo matatizo ya afya ya jamii zetu.
  • Kuainisha na kuwekeza rasilimali muhimu ulimwenguni zinazohitajika ili kuziongezea uwezo wa programu za kukinga na kutibu magonjwa yaletayo upofu.
  • Kuwezesha Vitengo vya Huduma za Macho kwenye nchi kupanga, kuendeleza na kutekeleza Mikakati mikuu mitatu ya Dira 2020 ambayo ni:
1.Udhibiti wa magonjwa
Mkakati huu unalenga udhibiti na tiba kwa magonjwa makuu yanayoleta upofu
2.Uendelezwaji wa rasilimali watu
Mkakati huu unalenga kuwezesha upatikanaji wa mafunzo kwa madaktari bingwa wa macho na kada nyingine muhimu zinazohusika katika kutoa huduma za macho.
3.Uimarishwaji wa Miundombinu na uendelezwaji wa teknolojia muafaka
Mkakati huu unalenga katika kusaidia kuboresha miundombinu na teknolojia ili kuwezesha upatikanaji wa huduma za macho.
Dira 2020 inaweka msisitizo wa kuongeza kasi ya kutokomeza upofu unaoweza kuzuilika duniani. Utekelezaji wa Dira 2020 unazingatia na kusisitiza ugawanywaji wa jamii kwenye ‘Wilaya za Dira 2020’ yaani jamii yenye wakazi takriban milioni moja, ili kurahisisha uratibu wa shughuli za kutokomeza upofu unaoweza kuzuilika. Kila ‘Wilaya ya Dira 2020’ ambayo hapa nchini ni Mkoa ama Wilaya inatakiwa kuwa na uwezo wa kutoa huduma za macho zilizo endelevu za gharama nafuu, zinazopatikana wakati wote na za kiwango cha juu. Sambamba na huduma hizi, ‘Wilaya ya Dira 2020’ inatakiwa kutoa elimu ya afya ya macho inayolenga kuboresha afya ya macho, kuzuia na kutibu magonjwa ya macho na huduma za utengamao kwa watu wenye ulemavu wa kuona.


Maadhimisho ya Siku ya Afya ya Macho yanalenga katika kuweka bayana na kuhamasisha wadau wote kuhusu hali halisi ya matatizo ya magonjwa na upofu duniani na huduma za Afya ya Macho ili kuwafanya waelekeze nguvu zaidi katika kukamilisha Azimio la Dira 2020.
Hali ya Ulemavu wa Kuona Duniani:
Inakadiriwa kuwa takriban watu milioni 285 duniani wana matatizo ya kuona. kati ya hao, milioni 39 wana upofu na milioni 246 wana uoni hafifu.Asilimia 80 ya matatizo yote haya ya kuona yanayoikabili dunia yanachangiwa na sababu zile zinazoweza kuzuilika.Idadi kubwa ya watu wenye matatizo ya kuona (asilimia 90) wanaishi katika nchi zinazoendelea.
Matatizo ya upeo mdogo wa macho kuona ambao haujarekebishwa yanaongoza kidunia kama sababu ya matatizo ya kuona wakati mtoto wa jicho anaongoza kama sababu iletayo upofu. Japokuwa matatizo ya upeo mdogo wa macho kuona ni sababu kubwa ya matatizo ya kuona kidunia, mtoto wa jicho anabaki kuwa ni sababu kuu ya matatizo ya kuona katika nchi zinazoendelea.
Asilimia 65 ya watu wenye matatizo ya kuona na 82% ya watu wasioona ni wale wenye umri wa zaidi ya miaka 50, japokuwa watu wenye umri huu ni asilimia 20 tu ya wakaazi wa dunia. Watoto milioni 19 duniani wana matatizo ya kuona.
Hali ya upofu nchini Tanzania
Kulingana na Takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) za hivi karibuni, Tanzania inakadiriwa kuwa na watu 992, 250 (yaani asilimia 3.15) wenye matatizo ya kuona ambapo kati yao, wasioona ni 315,000 (asilimia 0.7 ya  wakaazi wa Tanzania). Watu wenye uoni hafifu wanakadiriwa kuwa 787,500.
Sababu kubwa zinazosababisha upofu unaoweza kuzuilika hapa nchini na dunia kwa ujumla ni:-
·         Mtoto wa jicho (Cataract)
·         Shinikizo la jicho (Glaucoma)
·         Matatizo ya retina ikiwa ni pamoja na yale yatokanayo na ugonjwa wa Kisukari na umri mkubwa
·         Upofu wa utotoni utokanao na upungufu wa Vitamini A, mtoto wa jicho, maambukizi ya surua na maambukizi ya kisonono toka kwa mama kwenda kwa mtoto
·         Makovu kwenye kioo cha jicho
·         Upungufu wa upeo wa Macho kuona na uoni hafifu (Refractive Errors na Low Vision)
·         Trakoma/Vikope (Trachoma)
Huduma za Macho nchini
Hapa nchini Tanzania huduma za macho zinapatikana katika hospitali zote za Wilaya, Hospitali za rufaa za Mikoa, Hospitali za Rufaa za zoni, Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali maalum ya CCBRT. Katika kila Wilaya na Mkoa, yupo mratibu wa huduma za macho ambaye shughuli zake zinaratibiwa na Mratibu wa Kitaifa chini ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
Waratibu hawa ni madaktari bingwa, madaktari wasaidizi ama wauguzi waliosomea fani ya macho. Aidha katika kila hospitali ya Mkoa na Wilaya kuna wauguzi wa macho pamoja na mtaalam wa kupima upeo wa macho kuona na miwani wanaoshirikiana kiutendaji na waratibu hawa.
Huduma zinazotolewa ni pamoja na: elimu ya afya ya macho na mwili kwa ujumla, uchunguzi wa kina, upimaji wa miwani, huduma ya matibabu, huduma za upasuaji wa jicho na huduma za utengemao kwa wale wenye ulemavu wa kuona.
Huduma maalumu za macho kwa watoto zinatolewa katika hospitali za KCMC, Hospitali ya Taifa Muhimbili na Hospitali ya CCBRT.
Aidha, huduma za macho nchini kama ilivyo huduma nyingine za afya hutolewa kwa ushirikiano mkubwa kati ya Serikali na hospitali binafsi pamoja na taasisi za kidini.
Mafanikio na changamoto
Katika miaka 12 iliyopita kumekuwa na mafanikio kadhaa yaliyolenga kutokomeza upofu unaozuilika duniani, lakini bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuyafikia malengo ya dira 2020 ikiwa imebakia miaka 8 tu kufikia mwaka huo wa 2020.
Baadhi ya Mafanikio yaliyokwishapatikana ni pamoja na:-
·         Utetezi unaofanywa na wadau wa macho duniani umeweza kusababisha kuhamasika kwa viongozi na watunga sera katika nchi zote 193 zilizo wanachama wa Shirika la Afya Ulimwenguni.
·         Mpango- kazi wa Udhibiti wa Upofu na Uoni Hafifu umetengenezwa chini ya uratibu wa Shirika la Afya Ulimwenguni ili kusaidia taasisi zinazolenga kutoa huduma bora ya afya ya macho.
·         Nchi 100 zimeshaandaa mpango-kazi wa huduma za macho.
·         Jumla ya nchi 118 ulimwenguni zimefaulu kuanzisha kamati za Taifa za Dira 2020.
·         Takwimu zinaonesha kwamba hadi leo, idadi ya watu wenye upofu imepungua kutoka watu milioni 45 mwaka 1999 hadi watu milioni 39 mwaka 2011.
·         Idadi ya watu wenye matatatizo ya kuona yatokanayo na magonjwa ambukizi kama vile surua imepungua kwa kiasi kikubwa katika miaka 20 iliyopita.
Changamoto zilinazokabili utekelezwaji wa Dira 2020 ya Kutokomeza Upofu Unaoweza Kuzuilika Duniani  kote ni pamoja na:-
·         Kuna upungufu mkubwa wa rasilimali watu katika utoaji wa huduma za macho
·         Kuna ushindani mkubwa wa rasilimali chache zilizopo ukizingatia kuwa kuna matatizo mengineyo makubwa kama vile ukimwi, kifua kikuu na malaria. Hali hii inapelekea huduma za macho kukosa kupewa kipaumbele kinachostahili.
·         Kukosekana kwa miundombinu na teknolojia kwa ajili ya utoaji wa huduma za macho kutokana na ushindani wa rasilimali.
Wito wa kiutendaji:
Ili Tanzania iweze kuchangia katika kufikiwa kwa malengo ya Dira 2020 ya Kutokomeza Upofu Unaoweza Kuzuilika ifikapo mwaka 2020, yafuatayo yanapaswa kuzingatiwa:-
·         Halmashauri na Mikoa iweke nia na kutenga rasilimali kwa ajili ya kuwezesha upatikanaji wa huduma za macho zinazojitosheleza katika hospitali zao.
·         Mashirika ya maendeleo yaunge mkono na kuungana pamoja na Mashirika binafsi ili kuwezesha utekelezwaji wa dhana nzima ya Dira 2020.
·         Wanataaluma wa fani ya Macho wafanye wajibu wao kwa kushirikiana na kufanya kazi kwa pamoja katika kuwezesha upatikanaji wa huduma endelevu za macho ndani ya mfumo mzima wa huduma za afya nchini.

“Pamoja tunaweza kutokomeza upofu unaozuilika”


IMETOLEWA NA
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA AFYA NA USTAWI WA JAMII.

Mtetezi wa elimu Pakistan anusurika kifo

Malala Yousafzai,
Madaktari nchini Pakistan wamefanikiwa kutoa risasi kichwani mwa msichana wa miaka 14 mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel, Malala Yousafzai.
Hii ni baada ya msichana huyo kushambuliwa kwa kupigwa risasi hapo jana alipokuwa akitoka shuleni Kaskazini Magharibu mwa eneo la Swat.
Malala alituzwa tuzo la nobel kutokana na juhudi zake za kupigania haki ya elimu kwa wasichana wa Taliban ambao kwa mujibu wa desturi za kitaliban haswa katika eneo la Swat walikuwa hawaruhisiwi kupata elimu
Ndugu yake aliambia BBC kuwa, madaktari,wangali wanatafakari ikiwa wampeleke nje kwa matibabu zaidi.

SOURCE BBC

Tuesday, October 9, 2012

Thank you so much my Friends from Paris Friends Forever


Nitakuwa sina shukurani kama sitawashukuru Marafiki zangu kutoka Paris Ufaransa kwa Mijizawadi kibao ambayo wamkuwa wakinitumia jamani nasema Asante sana Mama Sophie Lob Pius dah I have nothing to say kwa kweli i love the shoe it's really nice what a  good friend ambae umekuwa na Moyo wa kipekee na wa upendo nashukuru sana kwa yote amabayo siezi kuaandika hapa ila unajua always love you.

Papa Soleil Sola from Paris Merci Mingi Vieux I really appreciate Thier Mugle Gift from you thank you.



 Unyunyu kama alijua duh thank you Sola + Hand bag ya designer wa ukweli uuh so in love with hivi vitu .
friends Forever. xo xo xo xo!!

Always Proud to have a beautifully Mama like you Mama Sophie Get well soon my Mama

Najionea fahari na furaha kila wakati napokuwa na Mama mwenye upendo wa dhati kwakweli nina kila sababu ya kumshukuru Mungu kwa Malezi bora upendo na suport ninayoipata toka kwa Mama yangu ambae amekuwa bega kwa bega na mie from day 1 nilipoiona hii dunia na kisha kunilea kwenye maadili ya dini na mila na tamaduni pamoja na heshima zote za kiafrica , Mama Mzaa chema Mama ambae amekuwa benga kwa bega na mie katika kila jambo ambalo nimekuwa nalifanya # siwezi hata kuelezea zaidi Mwenyezi mungu ndie ajuae.. napata shida sana some time naposikia au kuona Mama akiwa Mgonjwa naamini Mungu atakuwekea Mkono wake wa kheri na soon utapona na kurejea katika hali yako ya kawaida always praying for you My Mama Nakupenda sana . naamini soon you will be ok.

Friends please Pray for My Mama Presha inamsumbua sana sijui na uzee nao ila i hope soon she will be ok na kurejea katika harakati zake.  Love you Mama.

Dedication Kwaooo!!! # Living My life No matter what!" On My Own"

NI UJUMBE WANGU KWAKO LEO KAMA UTAKUCHOMA BASI TUSAMEHEANE NA KUHESHIMIANA  HABARI NDO HIYO!!

I'm wiser now
I'm not the foolish girl you used to know
So long ago
I'm stronger now
I've learned from my mistakes which way to go
And I should know
I put myself aside to do it your way
But now I need to do it all alone

And I am not afraid to try it on my own
I don't care if I'm right or wrong
I'll live my life the way I feel
No matter what I'll keep it real you know
Time for me to do it on my own
Yeah yeah, mmm, yeah yeah

It's over now
I can't go back to living through your eyes
Too many lies
And if you don't know by now
I can't go back to being someone else
Not anymore
I never had a chance to do things my way
So now it's time for me to take control

And I am not afraid to try it on my own
I don't care if I'm right or wrong
I'll live my life the way I feel
No matter what I'm gonna keep it real you know
Time for me to do it

Oh I start again go back to one
I'm running things my way
Can't stop me now, I've just begun
Don't even think about it
There ain't no way about it
I'm taking names, the ones of mine
Yes I'm gonna take my turn
It's time for me to finally stand alone, stand alone

I am not afraid to try it on my own
And I don't care if I'm right or wrong
I'll live my life the way I feel
No matter what I'm gonna keep it real you know
It's time for me to do it
See I'm not afraid

NDIO HIVYO LIVING MY LIFE NO MATTER WHAT

Friday, October 5, 2012

RICK ROSS WA BONGO KUMPOKEA AIRPORT RICK ROSS WA MAREKANI

Rick Ross wa Bongo kumpokea airport Rick Ross wa Marekani, ama kweli duniani wa wili wa wili
Rick Ross wa Bongo huyu hapa
Rick Ross Kutoka USA
Rick Ross Ajipange atapokuja Tanzania Tarehe 06 Oct 2012 kukutana na look i like wake....huendi Baba ake alicha mbegu Bongo..lol.

hongera sana Joseph Chintika kwa kushinda vyema



Joseph Chitinka

Alikuwa akigombea nafasi ya -Mjumbe wa mkutano mkuu CCM Taifa 2012-2017 kupitia UVCCM Dodoma

ameshinda kwa kura  215,Fatuma Issa kura 160,Ally Barongo kura 73.

Uzoefu wake katika Uongozi ni
-Mjumbe wa baraza la UVCCM mkoa wa Dodoma 2008-2012
-Mwenyekiti wa Tawi la St Johns University of Tanzania 2007-2010
-mjumbe wa halmashauri kuu ya tawi St johns University of Tanzania

Kazi nyingine anazofanya ni
-Mwenyekiti wa NGOs iitwayo Tanzania youth Capacity building
 

Thursday, October 4, 2012

HBD MY FRIEND ESTER ULAYA AND MY WIFIIIII


Jamani mwezi huu wamezaliwa wengi du.... hongera sana mama cathbert angelo aka mama Ester Ulaya kwa kutimiza miaka kadhaa ya kuzaliwa, mie mengi sina shoga ako nakuombea heri na mafanikio zaidi inshalah mungu akupe afya njema mpendwa.

MAVAZI YALIO NIVUTIA KWENYE EMMY AWARDS

unajua unapokuwa unafuatilia shows fulani basi kama mwanamke kuna vitu ambavo vinaweza kuwa vinakuvutia nilibahatika kuona Emmy Awards  ambazo zilijumuisha kina dada warembo sana huko majuu lakini kupitia DSTV nilivutiwa na muonekano wa mavazi haya ambayo yanaonekana kushika chart. 

sikuhizi bwana mtu anapokualika kwenye shuhuli yake basi kina dada wengi huwa tunajiuliza sana nivae nini ili tu ukabambe ndani ya Red Carpet si unajua tena na Bongo watu hawataki utani coz ladies wa Bongo Tz shiiiii*** wanajua kuvaa bwana .


No: 1

No: 2


                                                                          No: 3
No:4

No:5

No:6
Nilivutiwa na mavazi haya labda na wewe unaeza vutiwa na mmoja wapo  ukaweka oda then kwenye Red Carpet ukafunike unayoifikiria.

WOMEN IN BALANCE KPARTY GALA MWEZI HUU!!



Women in balance kitchen party gala kufanyika kwa mara nyingine tena.Safari hii ni ya mwisho kwa mwaka huu na ya aina yake. Itakuwa jumapili ya tarehe 21st october 2012.
Mahali:Diamond jubelee VIP hall
Muda:Kuanzia saa nane mchana mpaka saa nne usiku.
Kiingilio:Tsh 30,000
Ukitaka kubook meza ya watu kumi piga namba 0787583132,0716485666
Safarii hii ukiacha wasemaji kuna burudani ya kila aina ukizingatia ni ya mwisho kabisa kwa mwaka huu.Bila kusahau chakula,na vinywaji laini.
RANGI YA SIKU
Kwa muda kina dada/mama mmekuwa mkitoa maoni mnataka kushona nguo mtokelezee.
Basi rangi ya siku ni rangi ya chenza (tangerine tango)color of the year 2012.
Ishone utakavyotaka wewe iwe kitambaa cha kawaida,kitenge,kanga,batiki,au ukachanganya vyovyote ili mradi uzingatie rangi ya siku.

Kwa habari zaidi tembelea blogs zifuatazo
www.8020fashions.blogspot.com
www.dinamarios.blogspot.com
www.kajunason.blogspot.com
www.homezdeco.blogspot.com

 UJUMBE WA SAFARI HII
Mwanamke....kuwa mfano!

KUTAKUWA NA PRE LAUNCH  IJUMAA YA TAREHE  12 KATIKA BUSTANI YA SHEKINAH KWA MWALIKO MAALUM.UNATAKA MWALIKO NIPIGIE 0787 583132.

HAPPY BIRTHDAY ZAMARADI.. AND M BROTHER DR ISSAC



leo ni siku maalum sana kwenu rafiki na mfanya kazi mwenzangu Zamaradi mtekema pamoja na kaka yangu wa kufikia Dr Issac kwa kuweza kusherehekea kwa maranyingine tena mkiongeza miaka kadhaa ya kuzaliwa kwenu.


  mie sophie leo nachukua nafasi hii kuwapongeza sana na nawaombea mema Mwenyezi Mungu awajalie maisha marefu sana na mafanikio tele love you always Zama Nd My Bro Dr Issac.