Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, November 5, 2012

CHECK OUT:AFTER PARTY YA FETTY BAADA YA KUGRADUATE

                                                 Ilikua ni party flani ya kiaina tu, kusherehekea kumaliza kwa miaka yangu mitatu ya kutafuta na kufanikiwa kuipata elimu ya chuo kikuu. shukrani zote nazipeleka kwa Mungu kwa kuendelea kuniazima pumzi yake na kunielekeza vyema.
                              Pichani ni Washikaji wakipata msosi wa nguvu                       
 Nikki wa pili kwa mbaali namuona Dina Marios
  Antu Mandoza akipata msosi wa nguvu kabisa

My good friend's Uncle Shaa and his friend Calvin
                                                                        B Twelve na Faraja
                                                                          Shilole
                                                                     Warembo    
                                                                       Ncha kali
                                                                        Darasa
                                                                       B Dozen
 Muli B
                                                                          Sofia
                                                                       Darasa
                                                                        B dozen
                                                  Thats ma girl Shade

                                            Kulia,Faraja na kushoto kwangu ni Millard Ayo
                                                                     
                                                                          Nikki wa pili
Issa Wendo hahahaaaaa hatari sana huyu kaka
                                                                                  Jaffarai 
Ticha shiiipu hahahaaaa mshkaji wangu, kaka yangu, ndugu yangu, chizi mwenzangu thats him Evarist
Mgomvi wangu dunia nzima Tannisa aka Real tanny....
Mtu wa watu Chibebi
                                                                             Ncha kali
                                                                        Soudy Brown
                                                                    Cute couple Issa and Nurie
                                                               Muna mindu weeeeeee,  Burudani mwanzo mwisho
                                                       DeeAndy,Soudy Brown,Ncha kali 
                                                                       Tumetokelezea
kwa hisani ya dj fetty blog

MISS TANZANIA 2012-2013

 Brigette Alfred kutokea Kanda ya Kinondoni (Sinza).Akiwa amewabwaga wenzake 29 waliokuwa wakiwania taji hilo.Na kujipatia zawadi yake ya Gari aina ya Noah na pesa taslim Tsh ml 8.Hongera sanaaaaa!!

SERIKALI KUTOA DAWA ZA KUTIBU KISUKARI BURE KWA WATANZANIA WENYE TATIZO HILO.

Serikali imetangaza kutoa bure dawa za kutibu ugonjwa wa kisukari ili kuokoa maisha ya watanzania wanaokabiliwa na ugonjwa huo kutokana na kuwepo kwa ongezeko la wagonjwa wa kisukari kwa siku za karibuni.

Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii SEIF RASHID amesema hatua hiyo ya Serikali imefikiwa kutokana na kupatikana kwa gharama kubwa kwa dawa za ugonjwa wa kisukari na kuwa watu wanaokabiliwa na ugonjwa huo wanapaswa kutumia dawa hizo kwa maisha yao yote huku idadi kubwa wakiwa ni watoto.

Kauli hiyo ya Serikali imekuja kufuatia swali la Mbunge wa Viti Maalum SUSAN LYIMO ambaye ameiomba Serikali kutoa bure dawa za ugonjwa wa kisukari kama ilivyo kwa dawa za kutibu magonjwa mengine sugu ikiwemo UKIMWI

Saturday, November 3, 2012

WEEKEND NJEMA NAKUACHA NA MAPISHI YA NYAMA YA NGOMBE NA MAHARAGWE

Mapishi ya nyama ya ng'ombe na maharagwe
Mahitaji Maharagwe gramu 350, nyama ya ng'ombe gramu 150, chumvi gramu 5, chembechembe za kukoleza ladha gramu 8, sukari gramu 5, pilipili hoho gramu 5, vipande vya vitunguu maji gramu 3, mchuzi wa sosi gramu 3. Njia 1. kata nyama iwe vipande, koroga nyama pamoja na wanga. 2. washa moto, mimina maji kwenye sufuria, baada ya kuchemka, tia maharagwe kwenye maji, korogakoroga, yapakue. Tia mafuta kwenye sufuria, halafu tia vipande vya nyama kwenye sufuria, korogakoroga vipakue. 3. washa moto tena, tia pilipili hoho korogakoroga, halafu tia maharagwe korogakoroga, halafu tia vipande vya nyama, tia chumvi, chembechembe za kukoleza ladha, mchuzi wa sosi, korogakoroga, tia sukari korogakoroga, halafu mimina maji ya wanga korogakoroga, ipakue, mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa.

Rais Kikwete azindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela - Arusha (NM-AIST)‏

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi  Hati ya Ardhi ya eneo la   Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali ambaye ndiye Mkuu wa Chuo hicho katika sherehe za uzinduzi wake rasmi  Ijumaa Novemba 2, 2012. Kulia ni Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Burton Mwamila.




 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi toka kwa Makamu Mkuu wa  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela Profesa Burton Mwamila  jijini Arusha. Kushoto ni  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali ambaye ndiye Mkuu wa Chuo hicho katika sherehe za uzinduzi wake rasmi  Ijumaa Novemba 2, 2012.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia wakati wa uzinduzi rasmi wa  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Ijumaa Novemba 2, 2012. 

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua sanamu ya Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela  wakati wa uzinduzi rasmi wa  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Ijumaa Novemba 2, 2012. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe  wakati wa uzinduzi rasmi wa  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Ijumaa Novemba 2, 2012. Pamoja naye ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali ambaye ndiye Mkuu wa Chuo hicho, WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Burton Mwamila, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulugo, 


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali ambaye ndiye Mkuu wa Chuo hicho katika sherehe za uzinduzi wake rasmi  Ijumaa Novemba 2, 2012.


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya utafiti wa dawa asilia toka kwa Meneja Mauzo wa kampuni ya madawa asilia ya Moringa Natural Products Bi. Christina Ngoty wakati wa  uzinduzi rasmi wa  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Ijumaa Novemba 2, 2012.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya utafiti wa mitishamba toka Dkt Efrem Akilei Njau wakati wa  uzinduzi rasmi wa  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Ijumaa Novemba 2, 2012.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari wakati   uzinduzi rasmi wa  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Ijumaa Novemba 2, 2012.
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu wa zamani Mzee Edwin Mtei  wakati   uzinduzi rasmi wa  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Ijumaa Novemba 2, 2012.
Wageni waalikwa wakimshamgilia Rais Kikwete baada ya kuzindua rasmi  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Ijumaa Novemba 2, 2012.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha za pamoja wakati wa  uzinduzi rasmi wa  Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Ijumaa Novemba 2, 2012.

FREEMAN MBOWE AMFAGILIA JK KWA JUHUDI ZA KUENDELEZA MIUNDOMBINU NCHINI‏

FREEMAN MBOWE AMFAGILIA JK KWA JUHUDI ZA KUENDELEZA MIUNDOMBINU NCHINI‏

Mbunge wa Jimbo la Hai ambaye pia ni Mwenyekiti wa CHADEMA na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni Mhe. Freeman Mbowe akizungumza wakati wa sherehe za uzinduzi wa ujenzi wa Barabara ya Kwa Sadala-Masama wilayani Hai mkoa wa Kilimanjaro Oktoba 31, 2012

Tumia link hii: kufaudu zaidi


MAJAMBAZI WAMVAMIA WAKILI: YAPORA NA KUMPIGA RISASI TUMBONI.‏


Siku 18 tangu lilipotokea tukio la mauaji ya aliyekuwa kamanda wa polisi mkoa wa mwanza liberatus barlow, usiku wa kuamkia leo majira ya saa 8:00 za usiku katika eneo la Nyegezi watu wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia makazi ya Wakili wa kujitegemea Elias Hezron na kumpigwa risasi  ya tumbo kisha kumpora kompyuta yake ya mkononi (laptop), simu tatu ikiwemo moja ya mkewe na kutokomea kusikojulikana.

Wakili Elias Hezron wa kampuni ya uwakili ya JURISTIC LAW CHAMBER inayo milikiwa na Hon. Justice Nchalla, Outa & Hezron, Partiner Advocate ya jijini Mwanza ambaye amelazwa katika hospitali ya rufaa ya Bugando chumba cha wagonjwa mahututi (ICU) ambapo hali yake inadaiwa kuwa mbaya hivyo madaktari wanaendelea kumpatia tiba ili kuokoa maisha yake.

Akizungumza na Clouds kwa njia ya simu kaka wa wakili huyo George Hezron ameeleza kuwa tukio hilo lilitokea usiku wa Novemba 2 mwaka huu majira ya usiku baada ya muda mfupi kukatika kwa umeme ambapo wakili huyo akiwa na mkewe walisikia kishindo cha kuvunjwa geti na hatimaye mlango kisha watu wawili wasiotambulika sura zao waliingia ndani  huku wengine wakionekana nje ya nyumba na kumtaka Bw. Elias kuwapatia kompyuta yake ya mkononi, simu zake zote naye kukaidi agizo la watu hao.

"Baada ya kumuamuru na yeye kukataa  kutii kuwapatia kompyuta ndipo mmoja wa watu hao aliamua kumpiga na kitu kizito (nondo) kichwani naye kumkaba mwenzake hali iliyopelekea purukushani na kumzidia nguvu jambazi ndipo mwenzake alipoamua kutoa silaha na kumfyatulia risasi tumboni kisha kupora vitu walivyohitaji na kumwamuru mke wa wakili huyo pia kuwapatia simu yake ya mkononi na kisha wakatokomea kusikojulikana" Alieleza kwa masikitiko kaka wa wakili huyo.

Bw. George amefanua kuwa baada ya kupora kompyuta hiyo na simu hizo watu hao walitokomea bila kuchukuwa kitu kingine huku kompyuta iliyochukuliwa ikionekana kuwa na kumbukumbu na nyaraka za kesi mbalimbali ambazo wakili huyo amekuwa akizisimamia kwenye mahakama za mkoa wa Mwanza na mikoa ya jirani hali inayoonyesha kuwa watu hao walikuwa wamekusudia kupora nyaraka hizo.

Kaimu kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Mwanza Bi. Lilian Matola amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari polisi wanaendelea na uchunguzi wa kina na chanzo cha tukio ikiwa ni pamoja na kuwasaka kwa udi na uvumba watu walio husika 

UZINDUZI WA JIJI LA ARUSHA ULIVYOFANA.

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika shamrashamra za kulizindua rasmi jiji la Arusha Novemba 1, 2012 ambapo maelfu ya wakaazi wa jiji hilo walijitokeza kumlaki na kumshangilia katika hafla hiyo iliyoambatana pia na uzinduzi wa ujenzi wa barabara za jiji hilo. Sherehe hizo za kihistoria zilifanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid

 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea  ufunguo wa kuwa mkaazi wa heshima wa Arusha toka kwa  Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Gaeudence Lytimo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji

: Rais Jakaya Mrisho Kikwete akionesha ufunguo aliokabidhiwa na Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Gaeudence Lytimo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji
 

 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi hati rasmi ya kuuzindua mji wa Arusha kuwa jiji Meya wa Jiji la Arusha Mstahiki Gaeudence Lytimo mbele ya maelfu ya wakazi wa jiji la Arusha katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid 

 Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari akiwa ameketi bega kwa bega na Mama Mary Chatanda katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid wakati wa sherehe za kihistoria za kuuzindua rasmi mji huo wa kitalii kuwa jiji


PICHA NA IKULU