Picha hizi nilipewa na rafiki yangu wa huku Majuu ambae Mbwa wake alikuwa na ujauzito kishaa akaugua hali ambayo ilikuwa imehatarisha maisha ya watoto aliokuwa kawabeba tumboni basi bwana kwa kuwa wenzetu wanathamini sana wanyama wakaona ni vyema kuokoa maisha ya watoto hao kwa kuwa mama Mbwa mwenyewe alikuwa katika hali mbaya sana na haikuweza kujulikana kama atapona au la basi inasemekana wakampeleka mbwa wao katika Hospitali ya wanyama husika akafanyiwa upasuaji na kuzalishwa watoto hao wa mbwa unao waona pichani chini baadae walipata matunzo mazuri kama uonavyo katika picha wakiwa na afya njema mpaka sasa wanadunda na wanatamaniwa na kila mtu huko makwao. Mweeeeee ingekuwa bongo??? najiuliza tu Labda mbwa angekufa na wanae hao pia wangekufa.
dactari wa wanyama akiokoa maisha ya watoto wa mbwa mgonjwa.
watoto wa mbwa wakiwa tayari wamezalishwa kaba siku hazijatimia ambapo mama yao alikuw amgonjwa na mwenye hali mbaya sana.
Baada ya upasuaji huo nadahani umeona watoto hao na sasa picha zifuatazo ni za watoto hao walivyo sasa wamekuwa hatari duh
mtoto wa Rafiki Yangu akiwa Amelala na Mbwa hao baada ya kukua
Hao hapo sasa wanavyopendeza
huyu nae katia pozi wazungu dah wana mambo
anatamani Chai duh
wakiwa wame lala vizuri na kwa furaha pasipo mapenzi ya mama yao
anawaza nini huyu??
Habari ndio hiyo jamani Mie Hoi.