Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, June 18, 2012

EDDIE KADI ATUA BONGO HE IS THE BEST MALE COMEDIAN...


Miongoni mwa wachekeshaji mahiri sana London uingereza Eddie Kadi jana nilibahatika kukutana nae Live for the first time ndani ya Bongo ambapo Eddi ametua kwa shuhuli fulani fulani na atakaa kwa sikuchache .... Nikiwa pia miongoni mwa wapenzi wakubwa sana wa Stand Up Comed Eddie Kadi ni miongoni mwa wachekeshaji wanao nivutia sana kutokana na kazi zake. 
MIE NA EDDIE MAPEMA JANA


EDDIE KADI ni mzaliwa wa Kongo ila amekaa uingereza kwa muda mrefu sana Mbali na uigizaji Eddi pia Ni mtangazaji wa Choice Fm ya uingereza na amewahi pia kufanya kazi BBC london kama mtangazaji hakika nilifurahi sana kukutana nae kukaa nae kupata chakula cha usiku na kuzunguka baadhi ya maeneo kijana huyu hayuko Pekeyake ameambatana na  Manager wake anaejulikanakwa jina la  Ma mundele Maarufu kama Yasmin ambae pia ndie Manager wa Fally. picha zaidi na Mambo mengine nitakudondoshea soon.



EDDIE KADI AKIWA NA MANAGER WAKE YASMIN AKA MA MUNDELE.
MBALI NA EDDIE KADI MCHEKESHAJI MWINGINE ANAEISHI MAREANI ANAE NI VUTIA SANA NI EDDIE GRIFIN HUYO NAE NI NOMA NAZIPENDA KAZI ZAO LAKINI LEO HAPA MIMI LIVE NA EDDIE KADI


KWA UFUPI HAYO HAPO NI MAELEZO YA HISTORIA YAKE



- Best Male Comedian Nominee (Urban Comedy Awards '09)
- Top 5 UK Comedy Talent (Channel 4 Talent 2008)
- Best Male Comedian Nominee (BECA Awards 2008)
- Best Newcomer (BECA Comedy Awards 2006)
- Artist of the Year (Vine Awards 2006

Eddie Kadi was born in the DR Congo in 1983, and, moving to the UK at the age of 8, he grew up in Fulham, West London. A student at the Henry Compton secondary school (famously attended by British Athlete Linford Christie), he moved on to the William Morris Academy for Sixth Form. Head prefect and a popular student, Eddie threw himself into the performing arts, taking part in numerous school and church music groups.

He then went on to obtain a bachelor of science degree in Media Technology from Kingston University, where he was elected spokesman, and ultimately president, of the Kingston University African-Caribbean Society (ACS).

It was while at University that Eddie hosted his first show which further cemented that entertaining people seemed to come naturally - and he’s never looked back since!





HAPA NI BAADHI YA KAZI ZAKE AKIWA JUKWAANI EDDIE KADI BRAVO BRO.
HAPA KAZI ZAKE PIA UNAWEZA INGIA YOU TUBE UKAANGALIA EDDIE KADI KAZI ZAKE ZOTE UTAONA KWA WAPENZI WA COMEDY

EDDIE AKIWAJIBIKA

MASHABIKI WA EDDIE WAKIFURAHI

 EDDIE KADI ON STAGE
 MBALI NA UIGIZAJI EDDIE ANAPENDA SANA KUCHEZA SI UNAJUA TENA WAKONGO HAPO AKIWAFURAHISHA MASHABIKI WAKE
 KAZI NI KAZI EDDIE ON STAND UP COMEDY

KARIBU TANZANIA.

Friday, June 15, 2012

KAULI YA KWANZA YA DOGO JANJA BAADA YA KURUDISHWA KWAO NA MADEE.


Kama ulipitwa na hii stori ni kwamba msanii Madee wa TipTop Connection ambae ndio alikabidhiwa kumlea Dogo Janja na kumsimamia kwenye muziki alitangaza juzi kwamba amemrudisha Dogo Janja kwenye mikono ya wazazi wake baada ya kuona muelekeo wa Janja sio mzuri kitabia.Alisema kwanza Janja alikua mtoro wa shule na mara kadhaa hakwenda shule na alikua akimdanganya, aliwahi kumkuta anaogoelea Ubungo Plaza wakati wenzake wako shule, amekuta msg za matusi ambazo Dogo Janja aliwatumia watu wengine kuhusu Madee na makosa mengine kadhaa.Dogo Janja ambae sasa hivi karudi Arusha tayari amefunguka kila kitu katika Interview ya Dakika 40 Exclusive on millardayo.com na yafuatayo hapo chini ni baadhi ya mambo aliyoyazungumza.Amesema “kwanza napenda watanzania wajue kwamba mimi nilikua siishi na Madee nilikua naishi na rafiki yake ambae ni Abdallah Doka Kimara jirani na Madee, Madee alikua haniangalii kwa chochote na niliweka kikao juzi kati tu hapa nilikua nataka nirudi kwetu, kula ni Doka, kuvaa Doka, Hela ya Shule Doka…. ninavyoongea hapa Dogo Janja sijawahi kulipwa hela zaidi ya laki tatu kwenye show, Tanzania hii nimeshaizunguka ujue alafu sioni faida yake nakwenda kwenye show nikirudi napewa laki moja alafu ukiuliza mtu anaweza kukununia sasa nikawa zinanikera lakini nikawa nashindwa kuongea sababu ndio niko pale kwa ajili ninasoma


”KUHUSU ACCOUNT YANGU BANK:
Madee alininyang’anya mpaka kadi yangu ya ATM yani mimi narudi Arusha ni kama nakwenda kuanza maisha mapya hamna ambacho useme labda narudi Arusha ni kama vile nakwenda kuanza maisha mapya hamna ambacho useme labda naweza kurudi Arusha labda kwenye account sijui nina shilingi ngapi, kachukua hela zangu zote kwenye account yani, mi nilikua namuona mwema ananijali aliniambia nenda kafungue account na kiuaminifu pale unatakiwa kuandia namba zako mimi sikuandika zangu nikaandika za Madee, taarifa yoyote ya bank inakutana na Madee, mi siwezi kumtusi yule nitakua namkosea sana hata akinipa radhi inaweza kunipata mi naongea kilicho moyoni mwangu mpaka nimechukua hatua hii

KURUDISHWA KWANGU ADA SHULENI NA KIWANGO CHA PESA BANK:
Na jina lote hili Dogo Janja nilikua narudishwa ada nyumbani, nikachukua hatua nikaenda kufanya show ile hela yangu ya show baada ya kurudi nakumbuka alitoa laki mbili na 60, hela ilikua yangu akaniambia… Ahh Janja hapa sina hela nyingine nenda katoe kwenye account nitakurudishia.. ni brother alafu mi namuheshimu sana, kadi yangu ya bank yeye ndio alikua anaizuia lakini mwisho wa siku nakuja kuangalia account yangu, mbona account haisomi? na kadi yangu yeye ndio alikua nayo… Millard nakwambia ukweli wa mwenyenzi Mungu mimi account yangu haikuwahi kufikisha shilingi milioni moja na kila show ninayofanya nalipwa shilingi milioni moja, naongea mbele za mwenyenzi Mungu mimi mtoto wa kiislamu naitwa Abdulaziz


”KUHUSU SHOW YA MWISHO KUIFANYA KABLA YA YEYE KUNIPIGA:
Madee alinipigia simu jumapili akiwa Iringa ambapo jumanne wenzangu walikua wanaanza mtihani,nilimwambia niko na Hassan nyumbani kwa Tunda akasema ana kaka yake Kibaha alikua na show ya CCM alikua anamtaka lakini akaona hawezi na analove na bro akashindwa kukataa, roho ilikua inaniuma mimi hapa mimi nakwenda kufanya show kwa laki moja… alafu hapo niko na backup wangu nimempa elfu 20 mi nikabaki na elfu 80 alafu hiyo 80 anakupigia…. wee sikia elfu 50 hiyo kaweke bank, elfu 50 tumia…. mi nikafanya kipeace tu nikaenda kwenye show huyo brother wake kachelewa kuturudisha hapa saa saba usiku kwa sababu ujue mimi sina usafiri na yule jamaa alikua anasubiri mishe zake zote zikamilike alafu asubuhi nilikua natakiwa kuingia shule, kosa sio langu ni la huyo kaka yake Madee.. sikwenda shule jumatatu sababu nilichelewa.. hivi hata wewe Millard unaweza kulala saa saba ukaamka saa kumi??????! hiyo siku ndio nilitakiwa kwenda kuchukua namba ya mtihani nikapangwe la dawati langu ili jumanne nifanye mtihani, nilipoona nimechoka nilimpigia mwalimu wa Darasa nikamwambia siwezi kwenda shule jumatatu akaniambia hamna neno mi nikienda jumanne siku ya mtihani niende asubuhi nitapata

”JINSI MADEE ALIVYONIPIGA:
Nilikua nyumbani kwa Tunda Man na Hassan ambae aliniacha baada ya kutumwa, nimekaa kidogo natoka hivi nakutana na Madee geitinihajaniuliza chochote zaidi ya kuanza kunipig, kanichezeshea mikono kanipiga makofi alafu kanidhalilisha yani mtaa mzima umekusanyana pale kwa Tunda Man, t shirt ilichanika na akanikatalia kupanda kwenye gari… roho iliniuma palepale alafu alivyonikatalia kupanda kwenye gari huku akiniambia anikute nyumbani baada ya dakika tano, roho iliniuma nikasema haya yote nayapata kwa sababu mimi ndio nataka na napenda muziki na napenda baadae niwe na maisha bora, niliongea na wazazi wakaniambia nivumilie lakini kiukweli nikasema siwezi tena kuishi Dar es salaam na leo June 13 2012 ndio siku ya mwisho kuishi Dar es salaam hapa ninavyoongea, jioni niliitisha kikao nikampigia Doka, Madee, na kaka yangu huyu nikaulizwa labda kuna kitu Madee hanifanyii mi nikashindwa kuongea nikasema bwana mimi sitaki chochote mi nirudisheni kwetu ujue Millard mpaka mimi nachukua maamuzi haya kwamba naomba nirudishwe kwetu, nimeomba nirudi kiroho safi tu lakini nashangaa yeye anapokwenda kuongea mambo mengine kwenye media, mi namshangaa yule ni mtu mzima anajielewa ujue, sasa mimi sijui kwa nini amekua hivyo

”KUHUSU MADEE KUMUOMBA BABA YANGU ANIAMBIE NISIONGEE CHOCHOTE KWENYE MEDIA:

“Alimpigia simu baba ya kumuomba nisizungumze chochote kwenye media akidai kwamba itakua aibu kwangu na kwake, mimi niko hewani lakini hakunipigia.. baadae nikapata simu kutoka kwa bro akaniambia niongee na mama nilipoongea nae akaniambia Madee kasema nisiseme chochote kwenye radio, sasa imefika jioni nikashangaa nikamsikia sasa nikajiuliza kwa nini kaongea? na mimi siwezi kumpigia yule simu yani nimeshaapia kwa mwenyeenzi Mungu siwezi kumpigia simu.KUHUSU MIMI KUACHA MUZIKI: “Roho inaniuma kichizi nimeona hiviii, yani huu mziki huu kwa sababu haunisaidii chochote, mimi narudi Arusha ni kama narudi tena kuanza maisha mapya kwa hiyo mimi nimeona bora tu kama inawezekana huu muziki naweza kuacha na nitaishi kama zamani kwa sababu kwetu sijaua, nimeona bora nitulie nyumbani ujue mpaka Millard pale nimeomba kabisa jamani Eeehe nirudisheni nyumbani kwetu, nasema Inshallaah mwenyeenzi Mungu yupo na mimi na riziki hapangi Madee riziki anapanga Mungu”
KUHUSU KUSOMA DAR ES SALAAM:


“Sitaki kabisa kusoma Dar es salaam mimi nakwenda kusoma Arusha au mkoa wowote sitaki tena.
Chanzo:Millard Ayo.

ALI KIBA LIVE IN BRUXELLS

TODAY 15/06/2012 IS MY BABY GIRL AND DD FRIEND SHEILAS BIRTHDAY " HAPPY BIRTHDAY KIPENZI ,

MWINGINE HAKUNAGA" TODAY 15/06/2012 IS MY BABY GIRL AND DD FRIEND SHEILAS BIRTHDAY " HAPPY BIRTHDAY KIPENZI ,YANI SIKULALA USIKU MZIMA NIKITAFUTA HIZI PICHA ILI NIWEZE KUKUWISH NAZO HAPPY BIRTHDAY .KUDADADEKI HOW MUCH I LOVE YOU EHH" GOD BLESS YOU AND I WILL CALL YOU BAADAE !!"


Warembo waloumbwa wakaumbika" LOVE YOU MY DD FRIENDS!!

for more stories pic and ........take a look on http://networkedblogs.com/yMRxc

Thursday, June 14, 2012

UMESHAWAONA P SQUARE NA RICK ROSS KWENYE VIDEO MOJA? KAMA BADO ICHEK HAPA.

Imekua ngumu kwa waafrika wengi kuamini kama P SQUARE wa Nigeria wangeweza kufanya kolabo na Rick Ross rapper ambae bado yuko juu sana kwenye hiphop sasa hivi, sijachukua muda sana kuwaza au kujiuliza maswali mengi baada ya kukumbuka kwamba Akon anafanya nao kazi na kuna uwezekano mkubwa akawa ndio kawaunganisha.

Ninavyofahamu ni kwamba kuna process ndefu kidogo za kufata kama unahitaji kolabo na watu wakubwa kama Ross manake hata Marekani yenyewe kuna wasanii wanataka nae kolabo na hawampati, nakumbuka wakati Mimms amekuja bongo hata T pain hawakuruhusu kabisa kupigwa picha za video hasa wakiwa na wasanii wa bongo, ila walikubali kupigwa pictures za kawaida tu.
Anyway Chek hiyo kolabo ya P Square na Rick Ross hapo chini alafu utoe comment ya ulichopata au kukiona..

DIVA SONG IS FINALLY OUT 'PIGA SIMU FT DIAMOND THE PLATNUMZ




Its finally out! Diva Loveness Love brand new single featuring Diamond Platnumz that goes by the name of PIGA SIMU. A lot has been said about this track produced by Lamar at FishCrab Studios even before it came out, sasa have your say and let us know what YOU think.
SOURCE:
www.bongo5.com
P.S
Massive thanks to bongo5,am honored
ukitaka usikiliza bonyeza
follow download it on my Page twitterwww.twitter.com/Divaakamimi

JACK WOLPER AWAPAGAWISHA WANAFUNZI



KATIKA hali ya kushangazwa na kuonyesha jinsi gani mwanadada nyota katika tasnia ya filamu Jacqueline Wolper ni kivutio, wanafunzi wa shule ya msingi Baracks ilipo maeneo ya Kilwa Road walitimkia nje kwa ajili ya kwenda kumwona Jack huku wengine wakimrukia mwilini mwake na kumfanya awe katika wakati mgumu hadi Polisi walipokuja na kuwaamuru wanafunzi hawa kurudi madarasani walikokuwa wamewakimbia walimu wao.Jack alifika katika maeneo hayo kwa ajili ya kukagua maeneo kwa ajili ya kurekodia filamu mpya ya Injinia iliyoandikwa na msanii wa filamu na vichekesho Issa Kipemba ‘Kipemba’ Jack alikuwa ni mmoja kati ya majaji waliofanya usaili katika usaili uliofanyika Kilwa Road sehemu ya Polisi Bendi.“Nimefurahia sana kwa kupokelewa na wanafunzi kwa hamasa kama hiyo pamoja kuwa walikuwa wanataka kunizidi nguvu lakini nimefurahi nao kwani hawa ndio wapenzi wetu wa kazi za filamu, tunafurahi tunavyoona wanatukubali katika maeneo tunayofanyia kazi ni ushindi katika tasnia ya filamu,”anasema Jack.
Pia msanii huyo ni mmoja kati ya wasanii watakaoshiriki katika filamu hiyo ya Injinia filamu inayotabiriwa kutengenezwa kitaalamu zaidi kufuatia mtunzi wa filamu hiyo kujikita katika utafiti na kutumia wanataluma katika masuala ya upelelezi, filamu hiyo itarekodiwa na kampuni ya Papa zi ya jijini Dar es Salaam..

habari kwa hisani ya http://pro-24.blogspot.com/

CHEGE "SINA MPANGO WA KUFUNGA NDOA HIVI KARIBUNI, ILA NIMEKAMILISHA NYUMBA YANGU NA MTAA UTAPEWA JINA LA CHEGE STREET

Mwanamuziki na Mmoja kati ya wanamuziki  wa kundi la tmk wanaume faimly ambaye kwa sasa anatamba na ngoma yake mwanayumba, mtoto wa Mama Saidi Chege Chigunda amedai kuwa yeye bado yupo yupo sana,na  hana mpango wa kuchukua jiko kwa kile alichodai ndoa zina matatizo,ameongeza kwa kusema jamaa zake wa karibu kama  Mh.Temba hawamshauri kufanya hivyo, zaidi ya kumwonya kuwa asifanye hivyo..  Chege mwenye mtoto mmoja ambae anaishi na mama yake, na mwingine alifariki Dunia hivi karibuni, siku chache baada ya kuzaliwa pia aliongeza kwa kusema  kuwa amekamilisha mjengo wake ambao bado hajaamia.. na wakazi wa mtaa wake wapo kwenye process za kuuita mtaa huo kwa jina la chege.

habari kwa hisani ya http://pro-24.blogspot.com/

Thursday, June 7, 2012

Mapigano zaidi yazuka Mashariki mwa DRC

Raia wanaotoroka Mapigano DRC
Raia wanaotoroka Mapigano DRC
Mapigano makali yamezuka tena Mashariki mwa Jamhuri ya Kideomkrasi ya Congo DRC kati ya jeshi la serikali na wanamgambo wa M23 wanaomuunga mkono mbabe wa kivita Bosco Ntaganda.
Habari zinasema kuwa kundi lingine la wanamgambo kwa jina la Maji maji linalodai kuwatetea raia limejiunga katika mapigano hayo.
Raia wanazidi kuyakimbia makaazi yao hususan katika wilaya ya Masisi katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini.
Mwandishi wa BBC wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kideokrasi ya Congo, Jonathan Kachelewa, amesema wanajeshi wa serikali walirusha mabomu upande wa M23 huku wapiganaji hao wa M23 na wale wa Maji Maji nao wakarusha mabomu kujibu mashambulio ya wanajeshi yaliyofanywa na wanajeshi wa Serikali.
Bosco Ntaganda
Bosco Ntaganda
Makabiliano hayo yalidumu kwa saa kadhaa na idadi ya watu waliouawa au kujeruhiwa bado haijajulikana.
Kulingana na mwandishi huyo makundi mapya tayari yamejiunga na mapigano hayo nchini humo.
Katika Mkoa wa Kivu Kaskazini, Wilaya ya Masisi, kuna mapigano kati ya wapiganaji wa Maji Maji wanaojiita "raia Mutomboki" na wapiganaji wa FDLR kutoka Rwanda.
Watu kadhaa walioshuhudia mapigano hayo wanasema kuwa tayari raia wameanza kutoroka makaazi yao na kuongeza idadi ya wakimbizi wa ndani na wale wanaotorokea mataifa jirani.

Wednesday, June 6, 2012

DON'T MISS IT .....KITCHEN PART GALA 3



CHAMA CHA MADAKTARI WANAWAKE WATAKUWEPO PIA.
Ukifika mapema saa saba utapata huduma ya kupimwa saratani ya matiti bure na pia kupewa elimu ya kujipima mwenyewe mara kwa mara ili kujua afya yako.Kama unavyojua moja ya maradhi yanayowasumbua wanawake wengi na kupelekea kifo mojawapo ni saratani ya matiti.Ukigundulika mapema inatibika wahi siku hiyo upate huduma hii kabla ya shughuli kuanza.
TICKETS
Vituo vya ticket ni Shear Illusion mliman city,maduka ya casandra sinza,mikocheni na mjini,Born to shine boutiq mwenge na 8020 fashions Sinza.Kwa walio town piga namba 0716485666 ulizia Jajos.Ukitaka SPECIAL MEZA ya kukaa na mashoga zako(watu 10) piga 0787 583132 na 0657442255.



DONT MISS IT

HII NI YA PILI ILIOPITA. MAMA VICTOR AKITOA SOMO KWA UFUPI.

Afya ya Mubarak yadhoofika vibaya gerezani

Hali ya kiafya ya rais wa zamani wa Misri Hosni Mubarak imedhoofika vibaya katika siku ya nne tangu afungwe kwenye gereza la Torah, baada ya mahakama ya nchi hiyo kumhukumu adhabu ya kifungo cha maisha.


Siku alipelekwa gerezani, Bw Mubarak mwenye umri wa miaka 84 aliomba aambatane na madaktari wawili kutoka kituo cha afya cha kimataifa ambacho alikuwa akishikiliwa kabla ya kuhukumiwa, lakini wakuu wa gereza walimkatalia. Wakati huohuo msaidizi wa waziri wa mambo ya ndani wa Misri Bw Mohamed Naguib, jana aliamua kumhamisha mtoto wa Mubarak Gamal kutoka gereza la Molhak Mazraa na kumpeleka katika gereza la Mazraa ambayo ni sehemu ya gereza la Torah ili aweze kuwa pamoja na baba yake. Uamuzi huo umefikiwa baada ya watoto hao Gamal na Alaa kuomba wafungwe gereza moja na baba yao, chini ya kifungu cha sheria ya gereza ya "kuungana pamoja", hata hivyo ombi la Gamal lilikubaliwa lakini la Alaa bado halijaamuliwa.
 

 
Hukumu iliyotolewa jumamosi na mahakama ya uhalifu wa jinai ya Cairo ilithibitisha kuwa watoto hao wawili wa Mubarak hawana hatia, lakini bado wanakabiliwa na shtaka moja kuhusu kupata faida zisizo halali katika biashara ya faragha ya hisa za benki ya taifa ya Misri.

Tuesday, June 5, 2012

VICTORIA FOUNDATION YATOA MSAADA WA BAISKELI KWA WALEMAVU MKOANI GEITA KATA YA BUSANDA

Mwenyekiti wa Victoria Foundation,ambaye pia ni mbunge wa Viti Maalum Vicky Kamata ametoa msaada wa baiskeli kwa walemavu 30 katika wilaya za Nyakamwaga na Bukoli zilizopo mkoani Geita,











RAIS KIKWETE AKUTANA NA WABUNGE WA TANZANIA KATIKA BUNGE LA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI.

 Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza  na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya kukutana nao Juni 4, 2012 katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge jijini Arusha.Wabunge hao wapo Arusha tayari kwa kikao chao cha kwanza na wenzao wa Kenya, Uganda, Rwanda na Burundi Leo ambapo wanatarajiwa kuchagua Spika wa Bunge hilo pamoja na kuapishwa tayari kuanza majukumu yao.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Dkt  Jakaya Mrisho kikwete,  jana Juni 4, 2012 amekutana na Wabunge wa Tanzania katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki jijini Arusha.
Mhe. Rais, ambaye aliwakaribisha Wabunge hao kwa chakula cha mchana katika hoteli ya Ngurdoto Mountain Lodge, aliwapongeza kwa kuchaguliwa kwao kuiwakilisha Tanzania katika Bunge hilo la Jumuiya, na kuwataka wasimamie na kutetea maslahi ya nchi wakiwa huko.

Pia Rais amewataka Wabunge hao kuwa karibu na Serikali katika kushauriana namna ya kukabiliana na changamoto zitazojitokeza katika kazi zao, na kuwakumbusha kwamba majukumu ya Bunge hilo la Jumuiya ni kusimamia makubaliano  (treaty) yaliyoorodheshwa  katika kuundwa kwake na kuendeshwa.

Alisema: “Msome vyema na kuyaelewa makubaliano (treaty) hayo yote na vipengele vyake na msaidie kuiendeleza Jumuiya ambayo wanachama wote watanufaika nayo, na siyo upande mmoja.

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na Wabunge wa Tanzania Katika Bunge la Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Monday, June 4, 2012

nimeipenda hii style sana # NANASI


 MOI
 MMH NANASI WEEEE
 KWENYE MNUSO NA NANASI LANGU LOH

 BAADA YA MSUSI KUFANYA KWELI
 MIE NA AUNTI KWENYE MNUSO

ni style ya muda mrefu ila haiishi ladha hakina inavutia sana nimeipenda leo nimetoka hivyo mieeeh!!

KAMA UMEIPENDA NAMBIE NIKUELEKEZE UKAPATE NANASI NA WEYE KIZURI KULA NA NDUGU YAKO< RAFIKI AU JAMAA YAKO.

MY INTERVIEW NA DEO FILIKUNJOMBE,MP WA LUDEWA TALKING ABOUT HIS LOVE LIFE,WABUNGE SINGLE WAKIKE WANAVYOWAVUTIA AND ET CETERA