Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, August 24, 2012

WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII BALOZI KHAMIS KAGASHEKI AENDELEA NA MKUTANO WA TISA WA SULLIVAN, MALABO EQUATORIAL GUINEA



Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki (kulia) akiwa na Rais Mstaafu wa Ghana Bw. John Kufuor mjini Malabo, Equatorial Guinea (Picha na Pascal Shelutete)
 Waziri wa Maliasili na Utalii Balozi Khamis Kagasheki amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa Ghana, John Kufuor ambapo walizungumzia masuala mbalimbali ya kuimarisha Utawala Bora katika nchi za kiafrika. Aidha, Rais Mstaafu Kufuor alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Jakaya Kikwete aliyefika nchini Ghana kuhudhuria mazishi ya aliyekuwa Rais wa nchi hiyo John Atta Mills na kusema kuwa ni ishara ya uhusiano wa kidugu uliopo baina ya Tanzania na Ghana tangu enzi za waasisi wa mataifa haya Kwame Nkrumah na Mwalimu Julius Nyerere. (Habari Picha na Pascal Shelutete) 

Hatimaye Kalala arejea Twanga Pepeta na zawadi nono

Kalala Junior akizungumza na katika mkutano wa utambulisho kwenye ukumbi wa MangoGarden, kulia ni kiongoz msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza huku kushoto ni Msemaji wa ASET, Mohamed Pizaro na meneja wa ASET, Hassan Rehani.
Kalala Junior ( Katikati) akiweka hadharani vionjo vya wimbo wake mpya, Nyumbani ni Nyumbani kwenye mkutano na waandishi wa habari  akiwa na wanenguaji wa bendi hiyo, Frida Joseph aka Beckham, Sabrina Mathew na Mary Hamis aka Mary Kimwana wakionyesha staili yao mpya.
Na Mwandishi wetu
UONGOZI wa kampuni ya African Stars Entertainment Tanzania (ASET) umemtambulisha rasmi mwanamuziki mwenye vipaji vingi, Kalala Hamza Kalala maarufu kwa jina la Kalala Junior.
Kalala alitambulishwa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika kwenye ukumbi wa  Mango Garden ambapo mbali ya kusema kuwa amerejea kwa lengo la kuendeleza bendi yake hiyo aliyokuwa nayo kabla ya kujiunga na Mapacha Watatu.
Mwimbaji huyo maarufu alisema kwa  fumbo kuwa “Koti limembana akiwa na bendi yake ya Mapacha na kuamua kulivua na kuacha kuendelea kulivaa tena” na kujiunga na Twanga.
“Nimefurahi kujiunga na Twanga tena na nimekuja na zawadi za nyimbo mbili, wimbo wa kwanza unaitwa Nyumbani ni Nyumbani ambao  kwa sasa upo katika hatua ya mwisho na utatambulishwa rasmi wiki ijayo, ni wimbo ambao unazungumzia mambo mbali aliyokutana nayo katika muziki mpaka  kuamua kurejea Twanga,”  alisema Kalala.
Alisema kuwa  ujio wake wa Twanga siyo wa kulazimishwa, bali umetokana na mapenzi yake mwenyewe na hasa akikumbuka  fadhira za ASET ambapo ndipo alipata umaarufu mkubwa.
“Nawaomba  wadau wa Twanga wakae mkao wa kula, kwani nimerejea kivingine na watarajie kupata mambo mengi mazuri, nitafanya zaidi ya yale niliyoyafanya zamani, lengo ni kuendelea kushika hatamu katika muziki wa dansi,” alisema Kalala ambaye vionjo vyake ‘vimewashika’ mashabiki wengi wa muziki wa dansi.
Afisa Habari wa ASET, Mohamed Pizaro alisema kuwa ujio wa Kalala umetokana na mpango wao waliouanzisha ujulikano Amsha Amsha Twanga Pepeta Nyumbani ni Nyumbani .
Pizaro alisema kuwa mpango huo ni maalum kwa kuhimarisha bendi yao na hasa kwa wanamuziki ambao wameonyesha nidhamu nzuri wakiwa chini ya ASET na sasa wanatumikia bendi nyingine.
Kiongozi msaidizi wa Twanga Pepeta, Saleh Kupaza alimpokea kwa mikono miwili mwimbaji huyo na kusema kazi ya kujihimarisha zaidi imeanza.
“Karibu nyumbani, si unajua nyumbani ni nyumbani, tunaamini hata hao wengine wanajifanya vichwa ngumu, nao watarejea tu,” alisema Kupaza.
kwahisani ya full shangwe.

YANAYOJIRI KATIKA AMSHA AMSHA YA FIESTA TANGA

Mkuu wa Wilaya ya Moshi Mjini Dr Msengia akiaga baada ya kuitembelea timu Serengeti Fiesta 2012 Mkoa wa Kilimanjaro jioni ya leo. Katikati ni Erick ambae ni Mzalishaji wa timu ya Fiesta mkoani humo..Fiesta 2012..Bhaaaaaaaas!!


Gossip Cop akipiga stories na Fan pande za Tanga katika Amsha Amsha za Fiesta 2012..Fiesta Itafanyika Jumapili 26/8/2012 ndani ya Mkwakwani Stadium..Fiesta 2012..Bhaaaaaaas!!

AD+ Baba Jonii akiwa na na wana wa Tanga 

Adam, Diva na Wana wa Tanga

Vijana wa Tanga wakionyesha How They Can do it..Elimisha Burudisha Through This We can Teach How We Do It..

Gossip Cop Soudy Brown na Diva Loveness Love 


BIBI VERONICA MPANGALA AIBUKA MSHINDI WA BIBI BOMBA


Fainali za bibi bomba zilikamilika usiku wa jana katika viwanja vya ofisi za Clouds Fm na Tv, ambapo kati ya mabibi nane waliokuwa wameingia fainali, hatimae walipatikana washindi wawili walioondoka na mkwanja mrefu. Bi Veronica Mpangala wengi wanamjua kama tukinaaaooo ambae alikuwa ni mmoja kati ya mabibi waliokuwa wakifurahisha sana kwenye mjengo kwa ucheshi wakendie aliekuwa mshindi namba moja na kuondoka na shilingi milion 5 akifatiwa na mshindi wa pili aliechukua shilingi milioni tatu








British Airways kurejesha huduma zake Tanzania

Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Ndege ya British Airways imeirejesha angani ndege yake iliyokuwa ikifanya safari zake za kusafirisha abiria kati ya Dar es Salaam na London, Uingereza.

Kurejeshwa kwa ndege hiyo aina ya BA 737 kutaiunganisha Afrika kwenye mtandao wa safari za ndege na nchi za Ulaya unaofanywa na kampuni hiyo ya Britisha Airways.
Akizungumza kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na shirika hilo, jana, Ofisa Uhusiano wa British Airways, Mary Barry alisema safari hizo zimerejea baada ya matengenezo ya kawaida ya ndege hiyo.
Alisema ndege hiyo imerejea tena baada ya matengenezo hayo na itakuwa ikifanya safari zake za Ulaya na Afrika katika kipindi cha majira ya joto baada ya kutoonekana kwa kipindi cha miaka 25.
“British Airways inajisikia furaha kukamilisha matengenezo ya ndege hii ambayo ni moja kati ya zile ndogo lakini tunaamini itakidhi haja za wasafiri wa Afrika,” alisema.
Kama ilivyo kwenye ndege zake, alisema abiria kwenye ndege yake watafurahia huduma za aina mbalimbali kama vile vyakula, vinywaji na vifaa vya kisasa vya elektroniki, kwa lengo la kuburudisha wateja.
Wakati huohuo, Shirika hilo limesema kuwa litatoa punguzo maalumu la nauli kwa abiria wa Tanzania watakaosafiri na ndege hiyo kwenda Ulaya na New York Marekani.
Alisema tayari huduma za tiketi kwa safari zake zinapatikana kwa maajenti mbalimbali nchini, wakiwemo BA Travel.
Chanzo: mwananchi.co.tz

Mramba azidi kumkandamiza Mkapa mahakamani



Waziri wa zamani Fedha, Basil Mramba (Kushoto), Waziri wa zamani wa Nishati, Daniel Yona (Katikati) na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Grey Mgonja wakiwa ndani ya chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana, wakisubiri kuendelea kwa kesi yao ambapo wote wanatuhumiwa kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh11.7 Bilioni wakati wa uongozi wao. Picha na Venance Nestory.
Tausi Ally
ALIYEKUWA Waziri wa Fedha Basil Mramba, jana aliendelea kumkandamiza aliyekuwa bosi wake na Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, akimhusisha moja kwa moja na kutolewa kwa msamaha wa kodi kwa kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers.

Mramba aliyaeleza hayo jana wakati akijitetea dhidi ya tuhuma zinazomkabili za matumizi mabaya ya ofisi za umma na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni na kwamba alitoa msamaha wa kodi kwa kampuni hiyo ili kutekeleza matakwa ya mkataba.
Alidai kuwa kifungu cha 4.3.1 kilichopo kwenye mkataba huo ulioingiwa kati ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Alex Stewart Government Business Assayers kinasema malipo yoyote yatakayolipwa na mkataba huo hayatotozwa kodi.
“Mimi nilichofanya ni kutekeleza matakwa ya mkataba huu kwa sababu Waziri wa Fedha pekee ndiye mwenye mamlaka ya kutekeleza mkataba huo,” alidai Mramba.

Mramba alikiri kuruhusu gavana wa BoT kuilipa kampuni ya Alex Stewart, Dola za Marekani 1 milioni kama malipo ya awali, kwa ajili ya kufanya maandalizi ya ukaguzi wa migodi ya madini, na kwamba fedha nyingine zingelipwa kwa awamu.
Mramba alisema aliruhusu malipo hayo kufanyika kutokana na kuwapo kwa barua ya Mei 13, 2003, kutoka kwa Katibu Mkuu wa Rais, Patrick Mombo kwenda kwa Katibu Mkuu wa Nishati na Madini kuhusu mkaguzi wa dhahabu ikisema “Rais amekubali Waziri wa Fedha na BoT watafute njia ya kuilipa kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers”.
“Maagizo yote mimi niliyachukulia kama ni ya Rais, alikuwa akiagiza watendaji wake kutekeleza majukumu yote,”alisema Mramba na kuongeza kuwa kwa kuzingatia makubaliano hayo alitafuta fedha hizo kupitia bungeni katika Bajeti ya Serikali ya 2003/04.

Kuhusu mkataba, Mramba alisema kuwa anachofahamu yeye sheria ya BoT inampa mamlaka Gavana kuingia mikataba na kuisaini na kwamba mikataba yote aliyoingia na watu wengine ni lazima kodi isamehewe.
Mramba aliiambia mahakama hiyo kuwa, kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers ilikuwa ikitaka malipo bila kodi na kwamba, wao walikubali kutomtoza kodi kutokana na ushauri kutoka kwa wataalamu akiwamo gavana kuwa wamsamehe kodi vinginevyo wangemlipa zaidi.
Hata hivyo, alisema mkataba baina ya BoT na kampuni hiyo haukuwahi kupitia katika kikao cha Baraza la Mawaziri. “Sikudhani kama angeweza kutiliana nao saini kwenye mkataba huo, bila Baraza la Mawaziri kuridhia,”alisema Mramba.
Ushauri wa TRA

Mramba alibainisha kuwa Bethar Soka ambaye alikuwa kwenye kamati iliyofanya mchakato wa kuitafuta kampuni hiyo ya ukaguzi wa dhahabu, aliomba kupata kauli ya TRA kama kampuni ya Alex Stewart Government Bussines Assayers isamehewe kodi ama la, Mei 26, 2003.
Alidai kuwa baada ya Soka kupeleka ombi hilo Mei 26, 2003, TRA katika majibu yao ya Juni 24, 2003 walisema kuwa hawapendekezi mkaguzi huyo wa dhahabu asamehewe kodi na kwamba barua hiyo ilipelekwa kwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha wakati BoT na kampuni ya Alex Stewart Government Business Assayers iliingia mkataba Juni 14, 2003.
“Inaonyesha barua hiyo ya TRA ilichelewa kwa siku 10, baada ya mkataba kusainiwa, hata hivyo, ushauri huu wa TRA hatukuuhitaji hata kama ungekuja haungekuwa na manufaa,” aliongeza kudai Mramba.
Baada ya maelezo hayo, mmoja wa wanaosikiliza kesi hiyo, Hakimu Saul Kinemela, alimuuliza Mramba, Wizara ya Fedha iliomba ushauri huo TRA kwa kazi gani?
Akijibu swali hilo, Mramba alisema, "Siyo Wizara ya Fedha iliomba ushauri TRA, bali Soka aliomba ushauri huo kama mwanakamati iliyokuwa ikifanya mchakato wa kutafuta kampuni hiyo na kwamba Soka yeye alikuwa ni mtumishi wa wizara yake.
Alibainisha kuwa Soka asingeweza kumshauri Waziri, anayeweza kumshauri ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu.
Mbali na Mramba, wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, Daniel Yona na Katibu Mkuu wa zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja.
Jaji John Utamwa aliiahirisha kesi hiyo hadi Oktoba 12, mwaka huu itakapoendelea na utetezi.
Utetezi wa awali

Mramba (71) alianza kujitetea, Agosti 22, mwaka huu ambapo alidai kuwa Serikali iliiteua BoT ifanye kazi ya kutafuta kampuni inayoweza kufanya kazi hiyo hivyo ikaingia mkataba na kampuni iliyochaguliwa ya Alex Stewart Government Bussines Assayers.
Waziri huyo wa zamani aliongeza kudai kuwa aliyeagiza BOT kufanya kazi hiyo ya kumtafuta mkaguzi wa dhahabu ni Rais wa Awamu ya Tatu, Mkapa na kwamba wakati huo yeye akiwa Waziri wa Wizara ya Fedha alipewa jukumu la kuhakikisha gharama za kumlipa mkaguzi huyo zinapatikana ndani ya Serikali au BoT ama pengine popote.
Alifafanua kuwa kati yake yeye na gavana hakuna aliyekuwa na mamlaka juu ya mwingine na kwamba gavana alikuwa na wajibu wa kufanya mchakato wa kumtafuta mkaguzi wa dhahabu.
Mramba alisisitiza kudai kuwa yeye hakuhusika kwenye mchakato huo kwa kumtafuta wala kumleta hapa nchini wala kumtuma mwakilishi yeyote kumwakilisha kwenye kamati iliyoteuliwa kufanya mchakato huo bali alipewa agizo la kumlipa.
“Mimi kama waziri sikuwa na mtu wangu kwenye ile kamati, lakini Wizara ilituma mwakilishi, ambaye alikuwa mwanasheria Bethar Soka wakati wa kuhoji kampuni mbili ili wachague na kwenye kujadili vipengele vya mkataba,”alisema.
Inadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na Juni 14, mwaka 2004, jijini Dar es Salaam, washtakiwa wakiwa watumishi wa umma, walitumia vibaya madaraka yao na kuisababishia Serikali hasara ya Sh11.7 bilioni.
Ilidaiwa kuwa washtakiwa hao waliipatia msamaha wa kodi isivyo halali, Kampuni ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.
Chanzo: mwananchi.co.tz

Dkt. Harisson Mwakyembe amsimamisha kazi Mkuu wa Bandari

Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe
Waziri wa Uchukuzi Dkt. Harisson Mwakyembe amemsimamisha kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari-TPA-Ndugu Ephrahim Mgawe pamoja na wasaidizi wake wawili ili kupisha uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili.
Wengine waliosimamishwa ni Meneja wa Mafuta ya Ndege Kurasini, Meneja wa JET na Meneja wa Oil Terminal kutokana na tuhuma za kupotea kwa mafuta na kuidanganya serikali kuhusu mafuta masafi na machafu.
 
Kutokana na kuwasimamisha kazi Wakurugenzi hao Dkt. Harisson Mwakyembe amemteua Injinia Madeni Kipange kukaimu nafasi ya Mkurugenzi Mkuu wa TPA.
 
Kufuatia tuhuma hizo zinazofanywa Bandarini Dkt. Mwakyembe ameunda Tume wa ya watu saba kufanya uchunguzi kwa wiki mbili na kumpelekea taarifa ofisini kwake ili kubaini ukweli wa tuhuma hizo zikiwemo za wizi.
 
Pia ameagiaza kufikia Septemba Mosi mwaka huu malipo yote yafanyike benki ili kuondoa rushwa na wizi unaofanyika ndani ya Mamlaka hiyo.
 
Waziri Mwakyembe anachukua hatua hizo kutokana na wadau wengi sasa hawaitumii Bandari ya Dar es salaam kupitisha mizigo yao kutokana na kutokuwa na inami na watumishi wake hatua inayoifanya serikali kukosa mapato.
 
Pia ameagiza kusimamishwa mara moja kwa Kampuni ya Singilimo ambayo inajihusisha na kazi ya kubeba mafuta machafu na badala yake itafutwe Kampuni nyingine

Wednesday, August 22, 2012

ANATAFUTWA AMEPOTEA MSAADA JAMANI ATAKAE MUONA.





CYNTHIA KIMASHA Mkazi wa kijichi Jijini Dar es Salaam, amepotelewa na kaka yake anayefahamika kwa jina la ERICK KIMASHA anayesumbuliwa na maradhi ya akili ametokea Kilimanjaro na mara ya mwisho aliondoka nyumbani akiwa amevaa tracksuit ya brown na T-shirt la njano.

ERICK KIMASHA,  anaumri wa miaka 28, kwa muonekano ni mrefu Mweusi na nimwembamba, Erick alikuja jijini Dar es salaam kwa ajili ya matibabu ya maradhi ya akili katika Hospitali ya Muhimbili ambako alikuwa akiendelea na matibabu yake.


ERICK  alitoweka nyumbani saa tatu usiku, Ijumaa  August 17 Mwaka huu na kwenda  kusikojulikana. Dada wa ERICK, CYNTHIA KIMASHA anawaomba wasamaria wema  kwa  atakaye muona anaomba kutoa taarifa kituo chochote cha polisi kilichopo karibu nae au kuwasiliana kupitia namba 0657 655555 au  0714 533166.   
= = = =

Rais wa Liberia amsimamisha kazi mwanae

Rais wa Liberia Ellen Johnson Sirleaf, amemsimamisha kazi mmoja wa watoto wake wa kiume kutoka ngazi ya unaibu gavana wa benki kuu ya nchi hiyo kwa kushindwa kuorodhesha mali zake katika tume ya kuzuia rushwa nchini humo.
Ellen Johnson Sirleaf anashutumiwa kwa kuendeleza upendeleo wa kindugu

Charles Sirleaf, ni miongoni mwa maafisa 46 waliosimamishwa kazi kwa kosa hilo.

Ni mmoja wa watoto wake watatu wa kiume aliowateua kushika vyeo vya juu kabisa baada ya kushinda muhula wa pili wa uchaguzi mwaka jana.

Wapinzani wa Bi Sirleaf wanamshutumu kwa kuendeleza upendeleo wa kindugu.
Rais huyo amemteua mtoto wake wa kiume Fumba kuwa mkuu idara ya usalama wa taifa, na kijana mwingine Robert kuwa mshauri mkuu na mwenyekiti wa kampuni ya mafuta inayomilikiwa na serikali-NOCAL

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI ;


Chama Cha Mapinduzi kimetafakari hukumu ya kesi ya uchaguzi iliyotolewa jana Agosti 21, 2012 na Mahakama Kuu kanda ya Tabora.
Kimejiridhisha na kufanya uamuzi wa kukata rufaa dhidi ya hukumu ya kesi ya uchaguzi, dhidi ya Mbunge wa jimbo la Igunga mkoani Tabora Dokta Dalaly Peter Kafumu.
Kusudio hilo linatokana na kutorishwa na hukumu hiyo.
Imetolewa na;-
Nape Nnauye
KATIBU WA HALMASHAURI KUU YA CCM
WA
ITIKADI NA UENEZI
22/08/2012

NAOMBA RADHI KWA KUTOKUWA NAWE HEWANI KWA MUD AMREFU





JAMANI NAOMBA RADHI KWA KUTOKUWA NAWE HEWAN KWAMUDA MREFU NI KUTOKANA NA MAJUKUMU KUWAMENGI INGAWA WALAU NAAMINI MARA CHACHE TUMEKUWA TUKIKUTANA KATIKA OFFICIAL WEBSITE YANGU AMBAYO NI WWW.SOPHIAKESSY.COM ASANTENI KWA SUPORT NIMERUDI NIKIWANA NGUVU MPYA NA TUTAKUWA PAMOJA KUPEANA MENGI SANA KARIBU WADAU NAWAPENDA WOTE. UKIWANA LOLOTE BASI USISITE KUNIHABARISHA KUPITIA SOPHIA80TZ@YAHOO.COM,

Friday, July 13, 2012

WANAUME ZANZIBAR KUPEWA LIKIZO YA UZAZI.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, amesema mipango inaandaliwa kuhakikisha akina baba wanapatia likizo ya uzazi, pindipo wake zao wanapojifungua.
Waziri huyo alisema msingi wa hatua hiyo utasaidia ulezi wa wazazi wawili baina ya mama na baba mara tu wanapojaaliwa kupata mtoto.

Mzee alieza hayo ofisini kwake alipokuwa akitoa taarifa ya Serikali ikiwa ni maadhimisho ya siku watu duniani. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, amesema mipango inaandaliwa kuhakikisha akina baba wanapatia likizo ya uzazi, pindipo wake zao wanapojifungua.
Waziri huyo alisema msingi wa hatua hiyo utasaidia ulezi wa wazazi wawili baina ya mama na baba mara tu wanapojaaliwa kupata mtoto.
Mzee alieza hayo ofisini kwake alipokuwa akitoa taarifa ya Serikali ikiwa ni maadhimisho ya siku watu duniani.

Kwa miaka kadhaa hivi sasa wafanyakazi wa kike katika Serikali ya Zanzibar wamekuwa wakifaidika na mpango wa likizo ya uzazi kwa kupata mapumziko ya kipindi cha mienzi mitatu mara tu wanapojifungua na kupewa muda wa saa nzima ya kwenda kumpatia mtoto maziwa ya mama.
Alisema katika kuimarisha huduma za uzazi wa mpango na malezi kwa watoto wataozaliwa na watumishi wa umma, Serikali inakusudia kuchukua hatua ya kuwapa likizo ya uzazi wanaume ili kumsaidia mama ulezi kwa mtoto aliyezaliwa.

Alisema hivi sasa utaratibu wa likizo ya uzazi upo kwa upande mmoja tu ambao wamekuwa akipewa mwanamke, lakini hata hivyo bado haujaweza kuleta tija kutokana na wanaume kujiona kama sio sehemu ya kuisaidia familia katika kipindi hicho. Kutokana na hali hiyo, Waziri huyo alisema Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar, tayari imeanza kuandaa kanuni ili akina baba nao wapatiwe likizo (siku tano za kazi) la uzazi ili kumsaidia mama na mtoto aliezaliwa.
“Hatua hii itasaidia kuondokana na ile dhana kwamba suala la afya ya uzazi linamhusu mama pekee. Llakini hatua hii inategemewa iwe chachu ya kuwashirikisha akina baba katika harakati zote za huduma ya afya ya uzazi na mtoto”, alisema Waziri huyo.

Tuesday, July 10, 2012

NI KWA ODA MAALUM TU PENDEZA MWANA DADA NENDA NA WAKATI INATUMIA WIKI MOJA TU KUPATA MZIGO WAKO SHOP WITH SK: COLLECTION MALI MPYA FROM USA DRESS LIKE A HOLYWOOD STARS.

usikubali kupitwa SK: Collection kwa kushirikiana na Emmy Collection ya USA wanakupa njia rahisi ya kupendeza na kwenda na wakati  kama wafanyavyo Holywood Stars wa Marekani kwa kununua na kupendeza online kwa Oder Maalum baada ya kuona bdidhaa husika na kufikishiwa ulipo ndani ya wiki 1 mpaka 2 . kuanzia  shoes, Hand Bag, accessories, Dress, perfumes,
its for Reasonable Price
Select your choice and make a call  +255717331444 for more details.

SHOE
KILING SHOE AKA UNYAYOO $1,700



 BLUE SHOE $75

 ORAGLE SHOE IS FROM  $69




BLACK SHOE  NI $60

DRESS
MAGAUI YOTE UNAEZA PATA KWA BEI KUANZIA $ 60 MPAKA 80 MAKE A CHOICE AND GIVE ME A CALL PLZ







HAND BAG FROM $50 TO 95 $ TAKE A LOOK AND MAKE A CHOICE BABY











                                                          ACCESORIES
               bangili 40 per pc.










KARIBUNI SANA SANAAA