Nilisema nitakwambia kwa nini wimbo huu unaitwa MBONI YANGU.Wimbo huu ni maalum kwa ndugu yetu msanii Sajuki ambae anahitaji mchango wako wako wa hali na mali kuokoa maisha yake.Kabla sikupenda kuweka picha yake hapa katika hali aliyonayo sasa ila imebidi ili upate picha kamili.Sajuki anasumbuliwa na uvimbe tumboni na mwezi huu anahitajika kusafiri kwenda nchini India kwa matibabu.Wimbo tuliokuwa tunaurekodi unatoka katika filamu aliyowahi kuifanya na mkwewe ya MBONI YANGU.Na wimbo huu upo ndani ya filamu hiyo aliuimba Wastara.Wimbo huu tumeurekodi kuhamasishana kuchangia na utaanza kusikika kesho hapa clouds fm na video ya tukio zima la kurekodi itaonekana clouds tv.Na kesho tutahakikisha tunakusanya angalau Tsh ml 12,000,000 hapa clouds fm.Nakuomba sana mtanzania mwenzangu tushirikiane katika hili.
Wimbo huu tuliurecord mpaka mishale ya saa tisa kasoro usiku,nilikuwa nasinzia ila mapema saa kumi nambili leo alfajiri nilikuwa macho tayari.Thanks kwa coordinator Ruge Mutahaba & Dina Marios
Director Mwasiti Almasi
Producer Tuddy Thomas
picha habari na matukio kwa hisani ya http://dinamarios.blogspot.com/ tembelea blog ya Dina pia kuona mengi.
KWA PAMOJA WATANZANIA TUMSAIDIE KIJANA MWENZETU SAJUKI KWA KUDOWNLOAD WIMBO HUO NA PIA KUMCHANGIA KIJANA MWENZETU AKATIBIWE.
No comments:
Post a Comment