African music is on my blood Back to my root Proud to be Africa,be your self #lets talk about African culture,tourism music ,life style, business,technology, money, fashion, Love, Marriage, Health, food, animals,and so on!!!!
Monday, December 24, 2012
Friday, December 14, 2012
Koffi olomide atua jijini Dar tayari kwa onesho lake la jumamosi
Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuwasili akiwa sambamba na skwadi lake zima la Quartier Latin kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),tayari kwa onesho lake litakalofanyika siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba,onesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Afrika Masharikia (EABL) kupitia kinywaji chake cha Tusker kiingilio chake kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= kwa kichwa kama tiketi ikinunuliwa mapema na shilingi 15,000/= getini.Pichani kushoto ni Mwenyeji wake kutoka kampuni ya Prime Time Promotions Ltd,Godfrey Kusaga
Watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV pichan shoto ni Millard Ayo na Ben Kinyaiya pichani kulia wakifanya mahojiano mafupi na Mwanamuziki Koffi Olomide mara baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),jijini Dar.Koffi alitanabaisha kuwa yeye amekuja nchini Tanzania kwa mara nyingine tena kuwaburudisha na kuwaonesha vipaji alivyo navyo sasa ndani ya kundi lake la Quartier Latin.
Tuesday, November 27, 2012
MUIGIZAJI SHARO MILLIONEA AFARIKI DUNIA KWA AJALI YA GARI, KUZIKWA KESHO JUMATANO KIJIJINI KWAO LUSANGA
Sharo Milionea katika moja ya pozi zake za Kimilionea enzi za uhai wake.
TANGA, Tanzania
Msiba wa Milionea unakuja siku chache tangu msanii mwingine John Maganga afariki siku tatu zilizopita. Aidha tasnia ya sanaa pia hivi karibuni imempoteza muigizaji kundi la Kaole Sanaa Group Mlopelo, wiki chache baada ya kifo cha mwimbaji mahiri wa taarabu nchini Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ wa TOT
NYOTA wa filamu za vichekesho na Muziki wa Kizazi Kipya nchini, Hussein Ramadhani Mkiety ‘aka’ Sharo Milionea amefariki dunia jana usiku kwa ajali ya gari, imethibitishwa.
Taarifa rasmi kutoka kwa ndugu wa karibu wa Sharo Milionea na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga Constatine Masawe, zimethibitisha kutokea kwa kifo cha Sharo, kilichosababishwa na ajali ya gari katika kijiji cha Lusanga, Muheza, mkoani Tanga ambako ndio nyumbani kwao.......
Taarifa zilizoifikia Habari Mseto kutoka kwa ndugu wa Sharo Milionea, aliyetambulika kwa jina la Snura Mushi, zimepasha kuwa, nyota huyo alikuwa safarini kuytoka SDar es Salaam kwenda kijijini kwao Lusaanga, Muheza mkoani Tanga, kwa ajili ya kusalimia wazazi, ndugu, jamaa na marafiki.
“Ni kweli Sharo Milionea amefariki dunia jana saa mbili usiku kwenye barabara ya Segera, Muheza. Alikuwa akiendesha gari aina ya Toyota Harrier lenye namba za usajili T 478 BVR, ambalo liliacha njia na kupinduka mara kadhaa na kusababisha kifo chake, ambapo mwili wake umehifadhiwa kwenye Hospitali Teule ya wilaya ya Muheza.”
Habari Mseto imezipokea taarifa za kifo cha Sharo Milionea kwa masikitiko makubwa, kutokana na mwangaza halisi alioanza kuupata nyota huyo katika tasnia ya filamu na muziki nchini, alikotamba na filamu kadhaa, na nyimbo kali za Bongo Flava ukiwamo wa Chuki Bure aliomshirikisha Dully Sykess.
Msiba wa Milionea unakuja siku chache tangu kufariki kwa msanii mwingine John Maganga, aliyefariki siku tatu zilizopita. Aidha tasnia ya sanaa hiyo pia hivi karibuni imempoteza muigizaji kundi la Kaole Sanaa Group Mlopelo, wiki chache baada ya kifo cha mwimbaji mahiri wa taarabu nchini Mariam Khamis ‘Paka Mapepe’ wa TOT.
Habari zaidi zinapasha kuwa, baadhi ya wasanii waliokuwa nyumbani kwa marehemu Maganga, wakishamaliza kumzika nyota huyo, watasafiri kwa mabasi mawili maalum yaliyotolewa na mdhamini mmoja kuelekea Lusanga kwa ajili ya mazishi ya Sharo yanayotarajiwa kufanyika kesho.
Inna Lillah Wainna Ilaiyh Rajiuuuuun. Mungu ailaze roho ya marehemu Sharo Milionea mahali pema Peponi. Ameen.
Wednesday, November 21, 2012
A DAY TO REMEMBER # NAWASHUKURU SANA WAPIGA KURA WANGU KWA KUFANIKISHA YOTE.
karibu kuendekea kuona picha za matukio mbali mbali ambayo yalifanyika moshi katika chaguzi tofauti za ndani ya chama.
nikiwa miongoni mwa wagombea wa nafasi ya uwakilishi wa UWT kwenda vijana ambapo niliibuka mshindi kwa kishindo sina budi kuwapa shukurani za dhati na za kipekee wapiga kura woote ninacho ahidi ni kuwa nimeamua sasa kazi ni moja wataona kwa matendo na sio maneno.
POZI NIKIWA NA MH BETTY MACHANGU (MB)
KUJADILI NI MUHIMU SANA HASA KATIKA CHAGUZI MBALI MBALI
KIONGOZI WANGU
WAPIGA KURA WANGU
MMH NAMSHUKURU MUNGU KWA KILA HATUA
WAPIGA KURA WAKIJADILI
HAPO SASA
MAMA YANGU HAKUWA MBALI NA MIE KWA FURAHA KABISA ALINIUNGA MKONO
ASANTE SANA DADA NA KIONGOZI WANGU PIA KWENYE CHAMA DUME
WATU TULICHEZA IYENA IYENA WEWEEEE
MH BETI MACHANGU AKIJADILI JAMBO
KATIBU WANGU WA UWT DA YUSTA
MIE NA DADA YUSTER
KIONGOZI WANGU KATIKA POZI.
Tuesday, November 20, 2012
Picha: Aunt Ezekiel na mume wake kwenye harusi ya Dubai
Chanzo: Leo bongo 5
Friday, November 16, 2012
Ngisi wa kukaanga
Mahitaji Gramu 250 za ngisi waliolowekwa, gramu 500 za mafuta yaliyopikwa, vitunguu maji, tangawizi, vitungu saumu, chumvi, M.S.G., mvinyo wa kupikia, wanga wa maji na vipande vichache vya matango.
Njia 1. Osha ngisi waliokwishalowekwa, ondoa ngozi, wapasue vipande viwiliviwili kutoka kichwani hadi mkiani. Watandaze kifudifudi kwenye ubao wa kukatia mboga na uwakate katika umbo la fungu la ngano(acha upana wa mm.3 baina ya mikato, kina cha mkato kiwe 3/4 ya maki ya nyama, halafu kata mikato ya mshadhari), na mwisho wakate vipande vyenye urefu wa sm.4 na upana wa sm.2.
2. Pitisha vipande hivyo vya ngisi ndani ya maji yanayochemka na uvitoe kwa mkupuo mmoja ili viviringike.
3. Pasha moto mafuta mpaka yawe na joto la asilimia 80 hivi, tumbukiza vipande vya ngisi ndani ya mafuta na kuvitoa nje mara moja, la sivyo nyama itakuwa ngumu.
4. Tia mafuta kidogo ndani ya sufuria, kisha yapashe moto, mimina mchuzi wenye mchanganyiko wa vitunguu maji, tangawizi, vitunguu saumu, chumvi, M.S.G., mvinyo wa kupikia, wanga wa maji na matango, baada ya mchuzi kuchemka, tia vipande vya ngisi, iepue na iandae tayari kwa kuliwa.
Thursday, November 15, 2012
WATU WAWILI WAFA KWA EBOLA NCHINI UGANDA.
Wizara ya afya nchini Uganda imesema kuwa watu wawili wameaga dunia kufuatia mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola.
Kwa mujibu wa shirika la madaktari wasio na mipaka la Medecins Sans Frontieres (MSF), hakuna maafa yoyote yaliyoripotiwa kuhusiana na ugonjwa huo hatari tangu mwezi Agosti.
Waziri huyo wa Afya ameliambia shirika la habari la AFP, kuwa uchunguzi uliofanywa umethibitisha kuwa watu hao waliaga dunia kutokana na ugonjwa huo wa Ebola katika eneo la Luwero, takriban kilomita sitini kutoka mki mkuu Kampala.
Lakini amesema mwanaume mmoja kutoka eneo hilo, pia aliaga dunia mwezi uliopita, kutokana na kile kilionekana kuwa dalili za ugonjwa huo, lakini hakuna uchunguzi uliofanyika kuhusiana na kifo hicho.
Watu watano ambao ni jamaa wa karibu wa walioaga dunia, wanaendelea kuchunguzwa na madaktari. Wawili kati yao wamelazwa katika chumba maalum katika hospital kuu ya kitaifa ya Mulago mjini Kampala.
Hakuna tiba maalum inayojulikana ambayo inaweza kutumika kutibu ugonjwa huo, lakini wagonjwa hupewa dawa za kawaida za kinga pamoja na zile za kupunguza maumivu na kutibu Malaria ili kuongeza kinga mwilini.
Asilimia Tisini ya watu wanaogunduliwa kuwa na virusi vinavyosababisha ugonjwa huo wa Ebola huaga dunia, na katika kipindi cha miaka Kumi na mbili iliyopita kumekuwa na visa kadhaa vya mkurupuko wa ugonjwa wa Ebola nchini Uganda.
Takriban asilimia 50 ya yatu 425 ambao walikuwa wameambukizwa virusi hivyo waliaga dunia mwaka wa 2000.
SOURCE BBC NEWS.
Tuesday, November 13, 2012
Punda 200 huchinjwa Nigeria kwa matumizi ya chakula na sasa Soko kuu la punda lafungwa
Muuzaji mkubwa wa Nyama katika soko kubwa la punda nchini Nigeria ametekwa nyara na watu waliokuwa wamejihami.
Polisi wanasema kuwa kutekwa nyara kwa Al-Haji Salisu Yunusa,kumesababisha kufungwa kwa soko hilo ambalo lilijengwa miaka themanini imepita,mjini Ezamgbo.Kwa mujibu wa msemaji wa polisi Sylvester Igbo anasema kuwa juhudi zinaendelea za kumtafuta bwana Yunusa.
Mwandishi wa BBC Abdussalam Ibrahim Ahmed, mjini Enugu, anasema kuwa anaelewa watekaji wanataka dola milioni moja nukta 9 kama kikombozi kabla ya kumwachilia mfanyabiashara huyo.
Soko hilo lilifungwa siku ya Jumatatu huku wauzaji wakiandamana kupinga kutekwa kwake.
Hata hivyo lilifunguliwa baadaye huku wauzaji wakihofia kuwa kufungwa kwake kungezua hali ya wasiwasi na kutatiza harakati za kuweza kuokolewa kwa bwana Yunusa.
Uuzaji na ununuzi wa punda na nyama ya punda kumenawiri kama biashara katika soko hilo tangu kufunguliwa kwake miaka themanini iliyopita.
Takriban malori 20 ya punda huletwa katika soko hilo, kila siku.
ISIKILIZE HAPA SEHEMU YA HOTUBA YA YUSUF MAKAMBA CCM DODOMA MUDA MFUPI ULIOPITA.
ASANTE SANA MILARD HAYO KWA KAZI NZURI.
NDANDAA KOSOVO ASEMA YEYE NI MKALI KULIKO FM ACADEMIA ILA WAO WAMEMZIDI KWA MKOROGO NA KUVAA WIGI
MWIMBAJI mwenye asili ya Kikongo mwenye wingi wa vituko, Ndandaa Kosovo amesema yeye ni msanii mkali kuliko yeyote yule ndani ya FM Academia na kwamba hata kimataifa bendi yake ya Watoto wa Tembo iko matawi juu kuliko Wazee wa Ngwasuma.
Akiongea na mtandao wa Salut Ndandaa alisema FM Academia ambayo ni bendi yake ya zamani imemzidi kwa vitu vitatu: Kujichubua, kuvaa wigi na kuiba majina ya wanamuziki maarufu.
habari kwa hisani ya salut
MWIMBAJI MELODY AFARIKI DUNIA
MWIMBAJI nyota wa miondoko ya Taarab, Mariam Khamis “Paka Mapepe” amefariki alfajiri ya leo katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili.
Mariam Khamis ambaye hadi anafariki alikuwa ni mwajiriwa wa TOT Taarab alipelekwa Muhimbili kwa ajili ya uzazi na inasemekana mtoto ametoka salama lakini yeye Mungu amempenda zaidii.
Mtu wa karibu sana na mwimbaji huyo, Thabit Abdul ameithibitishia kwa wana SALUT kuwa ni kweli Mariam Khamis amefariki dunia.
Aidha mwimbaji Isha Ramadhan “Mashauzi” naye akiongea na saluti5 kutoka Muhimbili nae alithibitisha kutokea kwa kifo hicho “Ni kweli Mariam amefariki na hivi tunavyoongea tayari tupo hapa Muhimbili” Alisema Isha.
Mariam Khamis alitamba sana na wimbo wa Mapaka Mapepe alouimba akiwa na Melody, kabla ya kujiunga na Zanzibar Stars, Five Stars na hatimae TOT.
Wimbo wake wa kwanza kurekodi na TOT ni Sidhuriki na lawama ambao unatamba sana hadi leo hii
MAZISHI ya mwimbaji Mariam Khamis aliyefariki leo alfajiri yatafanyika kesho, Magomeni jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Baba Mdogo wa marehemu aliyejitambulisha kwa jina moja la Sembuli, alisema wamefikia hatua hiyo baada ya kuombwa na Mkurugenzi wa TOT Kapten Komba kufanya hivyo ili wapate kuhudhuria mazishi ya mfanyakazi mwenzao.
TOT wako Dodoma kwa hivi sasa kwenye mkutano mkuu wa Chama cha Mapinduzi.
Msiba uko nyumbani kwa baba yake mkubwa Magomeni makuti mtaa wa Ndovu Bar.
Mariam Khamis alifariki kwa uzazi baada ya kupata kifafa cha uzazi muda mfupi baada ya kufanyiwa upasuaji. Mtoto ametoka salama.
Monday, November 12, 2012
UCHAGUZI WA MWENYEKITI NA MAKAMU KUFANYIKA KESHO
MATUKIO YA MKUTANO MKUU WA NANE WA CCM KATIKA PICHA
Asha Baraka akiwa ndani ya banda la gazeti la Uhuru kwenye viwanja vya Kizota Dodoma. |
Viwanja vya Kizota vikiwa vimefurika wajumbe na wanachama wa Chama Cha Mapinduzi |
Biashara za aina nyingi zikiwa zimetanda kila kona. |
Ukumbi ukiwa umefurika wananchama na wajumbe wa Chama. |
Waalikwa kutoka vyama vya upinzani. |
Wajasiriamali hawakuwa nyuma kuuza bidhaa zao, Mkutano Mkuu wa nane wa CCM ulioanza leo umefungua fursa pekee kwa wafanyabiashara wadogo wadogo. |
Huduma za vyakula vya aina zote zinapatikana Kizota,eneo ambalo CCM inafanya Mkutano Mkuu wa nane. |
Wajumbe kutoka Mbeya wakionyesha ukakamavu wao kwenye ukumbi wa Mkutano Kizota leo. |