Wapo wanaomjua kama Drogba huku wengine wakimfahamu kama Mwananyika. Ni 
mdau wa Utalii ukanda wa Selous (Mloka) ambako yeye hujishughulisha na 
shughuli ya kusindikiza wageni kwenye safari za Matembezi maeneo ya 
pembezoni ya pori la akiba la Selous huko Mloka, Rufiji. Safari hii nae 
alielekea ukanda wa kaskazini na kuwakilisha utalii wa kanda ya Kusini 
kama anavyoonekana kwenye picha hizi.
Jina la Drogba amepewa sababu ya sura yake kuonekana kufanana na ya 
Mwafrika mwenzetu anayesakata kabumbu huko bara la Ulaya, Didier Drogba.
 Mwenyewe hupenda zaidi kutumia jina la Mwananyika, jina ambalo hulitaja
 pia kwenye nyimbo zake anazoziimba akiwa kwenye misafara yake na wageni
 kwenye mapori ya kijiji cha Mloka. Safari zake hujaa mafundisho mengi 
na mazuri kuhusu mahusiano baina ya wanyama pori, wanadamu na mazingira 
ambayo sote tunatumia pamoja.
KWA HISANI KUBWA KABISA YA TEMBEA TZ 


 
 
No comments:
Post a Comment