Aliyekuwa
mwanamuziki wa rumba, Luambo luanzo Makiadi amejengewa mnara mkubwa mjini Kinshasa
ambako waziri mkuu aliuzindua jana usiku wakati wa maadhimisho ya miaka 26 ya
kumbukumbu ya kifo chake.
Mnara huo wa picha yake umejengwa kwenye eneo
la wasanii, la PLace de la Victoire/Matonge katika mji mkuu wa Congo.
Luambo ambaye jina lake kamili ni Francois
Luambo Luanzo Makiadi, aliyezaliwa mwaka 1938 na kufariki dunia Oktoba 12 mwaka
1989 akiwa na umri wa miaka 51, alikuwa mtunzi, mpigaji gitaa na mwimbaji
ambaye kundi lake la OK Jazz ligeuka kuwa bendi maarufu ba
rani Afrika na duniani kote.
Serikali
ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeahidi pia kuwajengea minara ya kumbukumbu
wanamuziki wengine watatu, Joseph Kabasele," Grand Kalle,Tabu Ley
Rochereau na Lutumba Simaro.
No comments:
Post a Comment