NAOMBA MSAADA KWA RAISI, IGP MWEMA NA
WANANCHI WOTE NIPATE HAKI ZANGU NIKIWA KAMA MAMA NA MKE KUFAHAMU KUJUA MUME
WANGU ALIPO.
Baada ya kukaa kwa siku mbili bila kujua alipo mume
wangu, nimejitokeza mbele ya waandishi wa habari wapate kunisaidia kufikisha
ujumbe wangu wa kupata msaada ya kujua mume wangu alipo.
Hapa ni karibu
kabisa ya ukumbi wa habari maelezo ambapo niliwafuata waandishi wa habari ili
kupata muda wa kuongea nao, nikiwa nimewabeba wanangu Lincon na Linston.
Nina watoto wawili mkubwa ni wa miaka 2
na mdogo wake ni wa miezi 4, leo ni siku ya nne hawajamuona baba yao, baba yao
ni msaada mkubwa mno kwa familia yangu, Raisi Kikwete huko ulipo nakuomba usikie
kilio changu, IGP Said Mwema nahitaji msaada wako, Wanawake na Wote nahitaji
msaada wenu.
Hapa nikiendelea
kuelezea hali halisi ya jambo hili mpaka leo hii kuja hapa, na kubwa ni kutopewa
taarifa ya mume wangu alipo. Sina Amani kabisa naomba kupata taarifa kamili huko
aliko yuko salama? na hata kufahamu anakula nini?
Kubwa watanzania
wenzangu ni kunisaidia katika maombi ili huko aliko awe salama.
Kwa Urefu
zaid habari hii itaruka katika vyombo mbalimbali vya habari zikiwepo TV kama
Channel Ten, ITV, EATV, Star TV na Clouds, Radio kama Clouds, Radio One, na
magazeti kama Mwananchi, Nipashe , Mtanzania, Tanzania Daima , The Citizen,
Guardian, na vyombo vingine vya habari.
Nawashukuru waandishi wote ambao
walikuwepo hapa, pia na watanzania wote naamini mko pamoja na mimi. .
HABARI HII NI KWA HISANI YA JOYCE KIRIA WANAWAKE LIVE.