Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, March 27, 2014

Rais Barrack Obama wa Marekani anakutana na na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis.


Rais Barrack Obama wa Marekani anakutana na na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, katika makao yake makuu huko Vatican.
Hii ni mara ya kwanza kwa Obama kukutana na papa Francis.
Rais Obama ameelezea furaha yake ya kukutana na papa mtu ambaye kulingana naye anaishi na kutenda kulingana na injili anayoihubiri.
Maswala mbali mbali yenye umuhimu wa kimataifa pamoja na kidini huenda yakajadiliwa katika mkutano huo.
Wawili hao wanatarajiwa kujadili namna ya kupunguza tofauti iliyopo kati yao katika maswala mengi mbali na kujaribu kuinua maisha ya watu maskini duniani.
source Bbc.

Thursday, November 28, 2013

UKITAKA KUOWA KWA WAZARAMO BASI ZINGATIA HAYA.


Kwanza kwa ufupi kabisa nikufahaishe kuwa Wazaramo ni kabila kutoka eneo baina ya Dar es Salaam na Bagamoyo, nchini Tanzania. Hawa  Wazaramo ni sehemu ya Wabantu. Mababu wanaamini kwamba waliingia katika eneo la Tanzania katika milenia ya kwanza,  inasema ya kwamba walihamia pwani katika mazingira ya Dar es Salaam kutoka Uluguru (Morogoro) katika karne ya 18.
Basi kama ujuavyo Tanzania watu hutoka mkoa mmoja kwenda kuchumbia mkoa mwingine au kabila fulani kwenda kuchumbia kabila jingine ni jambo la kawaida sana ingawa katika makabila hayo wana mila na tamaduni zao ambazo bado kila kabila huamini na kuzifanya wakati wa sherehe misiba au ndoa.
Sasa basi tunapokuja katika swala la ndoa  wewe kijana Ukitaka kuchumbia kwa Wazaramo basi tegemea kukutana na haya .
1.    Yahitajika uwe na Mshenga ambae  wewe muowaji atakuwakilisha, itaandikwa barua ya posa kwenda kwa wazazi wa Mwali ambae unataka kuowa,na barua hiyo itapelekwa na mshenga wako .

 2.  Baada ya barua kupelekwa  inapangwa siku maalum ambapo barua hiyo itasomwa kisha baadae utapewa jibu la NDIO au HAPANA . na kama basi utakuwa umekubalika kwa wakwe zako majibu utakayopewa utaambiwa kwamba Mtoto au huyo Mwali ataolewa kwa mahari ya kiasi Fulani  na mambo yanayo hitajika na nilazima uyatimize.

3.    Utakapo pokea majibu ya kukubaliwa unatakiwa huyo mshenga wako arudishe majibu ya shukurani kwa kukubaliwa pamoja na MAHARI uliyo pangiwa .

4.    KATIKA MAHARI kunakuwa na fedha ulizo ambiwa kama ni m 500 au 1,000 au hata milioni moja ni kile ulichoambiwa utapeleka  . KUNA MKAJA WA BIBI ( hili ni kama kapu la bibi wasemavyo sikuhizi  linakuwa na kila kitu ndani, kanga, nguo mafuta sabuni sukari na hata blanketi la bibi yani kila kitu ambacho bibi anapaswa kutumia)  kisha kuna SAMBUA LA NDEVU  hilo mwenzangu sasa utauliza zaidi lina mambo gani naambiwa hizo ni mbwembwe tu vikolezo vya kufanya mahari ipendeze . Kisha kuna KANYANGA LUBUGA . Kisha ukisha timiza hayo  basi unapanga tarehe ya kufanya ndoa.

5.    Kumbuka katika ndoa pia yasemekana kuwa hufungwa kulingana na nyota ya mhusika ndio maana yaweza fungwa mchana au asubuhi na hata usiku ili basi kuweka tu mikakati mizuri ili ndoa isije vunjika ndio maana pia wanazingatia muda wa kuowa.

6.    Mie nakomea hapo basi kama kula lolote zaidi juu ya wazaramo karibu sana na ruksa kabisa kuniongezea hapo  ili tujuzane mengi ndio maana ya mimi kuzungumza na wewe.
Nimshukuru sana kaka yangu Mbwiga wa Mbwiguke Mzaramo halisi kwa kunidokeza haya basi na mie nikaona vyema tujuzane pamoja.
sikunjema kwako .......

Wednesday, November 27, 2013

MONIE JOSEPH MWANA DADA ANAENIVUTIA KWA UCHAPAJI KAZI WAKE .


Winners ..
Represented well the Tanzania Business Community. With MH. Mohamed Dewji. (MP)

HAKIKISHA UNAFUATILIA NA KUSOMA HABARI MBALI MBALI ZA MAMSWALA YA BIASHARA KATIKA BLOG YAKE YA monfinance

KAMATA FURSA TWENDE ZETU



nikiwa na mh January Makamba naibu waziri wa mawasiliano sayansi na teknolojia katika semina ya Fursa iliofanyika katika umbumbi wa Diamond Jubilee hall hapa dar es Saalam.

pichani katika mahojiano na Nasib Abdul maarufu kwa jina la Diamond mmoja ya wanamuziki wa muziki wa kizazi kipya hapa nchini ambae ameiona Fursa akaitambua na kisha kuifanyia kazi.


picha ya pamoja kutoka kushoto ni Da Regina Mwalekwa Mh January Makamba  Jerome Risasi na mie sophia kessy.



Friday, June 28, 2013

ANANIPIGA SANA ILA NAMPENDA NAOGOPA KUMUACHA NIFANYEJE MWILI WOTE UNA MAJERAHA YA VIPISI VYA SIGARA

Ama kweli dunia ina mambo,unaambiwa tembea ujionyee yanayojiri duniani kweli MOYO UKIPENDA MACHO HAYAONI.Jana nilibahatika kwenda kutembelea maeneo Fulani hivi pande za mbezi, wakati nikiwa huko nikakutana na ma binti wawili wamekaa wanajipatia vilaji, mmoja wao alikuwa mwenye huzuni sana  bahati nzuri nawafahamu wakati naingia eneo la tukio mmoja wapo akaanza kunipa story, si unajua tena mambo ya wanawake tukikaa basi hatuishi kuteta hili mara lile, katika zungumza mwenzetu huyo akaanza kutusimulia jinsi anavyopata kipigo toka kwa mpenzi wake ambae kwa sasa wanamiaka 5 ya mahusiano, anakuambia tangu ameanza mahusiano jama ayake anawivu sana yani akimpigia simu dakika mbili isipopokelewa ni kosa akikutana nae ni kichapo. Akitoka hata kwenda sokoni asipomuarifu basi kichapo bidada ana makovu ile mbaya ya kipigo, si kwao wala si kwa marafiki wamemkataza na kumwambia hayo si mapenzi jamaa pengine hana nia nae njema atamtoa roho.

wiki chache zilizopita alienda kwenye kitchen part ya rafiki yake bahati mbaya hakuwa na usafiri hivyo alitegemea usafiri wa mashosti awahi kurudi home kwakwe, kwa bahati mbaya yule shoti mwenye gari akachelewa kurudi akarudi home kwenye saa 7 usiku, kumbe jamaa yake alishafika home tangu saa nne  na kumgoja bila kumuona, na unajua tena mambo ya mitandao simu ikawa kwa bahati mbaya haipatikani lol, wanasema siku ya kufa nyani miti yote huteleza .


Basi bwana bidada aliporudi home kesho yake  jama ayake akamuita eneo la kin'gori Arusha , binti hakuwa na hili wala lile wamekaa zao bar wanakula na kunywa mara jamaa akaanza kumhoji ilikuwaje ukachelewa binti wa watu akajielezea wee lakini wapi, unaambiwa bila haya jamaa akanyanyuka pale pale na kuanza kumpa kichapo mbele za watu tena bar .


Piga binti kisawa sawa mpaka akawa hoi ndio ikabidi watu waliokuwa bar wamuokoe jamaa kwa sifa akawa anasema TENA NAKUPIGA KISAWA SAWA NA KUKUACHA SIKUACHI. na ukitaka kashitaki popote sasa binti ndio ndugu zake kumuona na majeraha wakamtorosha na kumleta dar, binti anasema anampenda mpenzie na anataka kurudi kuleeee alilokuwa napata kichapo mmh ukimuangalia mwili mzima makovu ya hatari.


Nikajiuliza jamani Mapenzi gani haya loh ... JE UMEWAHI KUYAONA AU MWENZETU ANA TATIZO AU NDO MAPENZI YAMEKOLEA DUH .

TUZUNGUMZE JAMANI

Thursday, June 27, 2013

ATI WAJAMENI JE UMRI NI KIGEZO? UNANAFASI GANI UMRI KATIKA RELATIONSHIP. MSAIDIENI DADA GETRUDA

Habari za leo dada Sofia?? kwa kweli jana nilipopita katika blog yako nilifurahishwa sana na topic ambazo kwa jana uliweka ili tuweze kuchangamsha akili na kusaidiana walau kupeana ufahamu wa hayo machache tulio nayo mie nina maswali kwako na kwa wadau wa blog hii yetu tena naomba nikupe jina Anti sophie nakumbuka sana jina hilo ulikuwa ulilitumia wakati tulipokuwa wadogo katika kipindi cha watoto huko Terrat Simanjiro kwakweli dada nisiseme mengi nakufaamu kwa uzuri tu na nafurahiswa na kazi zako .

Sasa basi langu lengo hapa ni kukuuliza wewe na wadau wa blog yetu kama nilivyo bainisha hapo awali kuwa Ati UMRI NI KIGEZO au UMRI UNANAFASI GANI KATIKA MAHUSIANO??. mie nimetokea kupendwa na kijana mmoja jina kapuni lakini kulingana na umri wangu mie na miaka 35 yeye ana miaka 28 naogopa mmno  ingawa kijana huyo na mpenda sana, ila hofu yangu ni ndugu na marafiki pengine wataniona kama nambemenda kijana wa watu, kwa kweli najitahidi sana kumkwepa ila naona kama naidhukumu nafsi yangu mie naomba ushauri wenu marafiki pamoja na dada Sofia je nifanyeje kwasababu nampenda mmno ila nahofia umri nisaidieni.. je umri unanafasi gani katika mahusiano je nimwache tu kwasababu mdogo kuliko mie au nifanyaje naidhulumu nafsi yangu jamani.

wenu rafiki Gatruda Nipo Arusha kaloleni.

HAYA MARAFIKI HIYO NI BARUA PEPE YA MDOGO WETU GETRUDA TUNAMSAIDIAJE HEBU TUZUNGUMZE KATIKA KURASA YETU HII PENGINE ATAPATA MUAFAKA WA KILE ANACHOFIKIRIA WENU ANTI SOPHIE

Wednesday, June 26, 2013

Nakaribisha barua pepe, na lolote lile ambalo ungetaka lijadiliwe kuhusu mapenzi, mavazi, urembo, ndoa , maradhi, afya, maisha , nk

karibu sana marafiki nimeona nibadili mwelikeo wa blog yetu kwasababu najua jamii inayotuzunguka ina mambo megi sana ya kuzungumza badala ya kuonyesha tu picha za matukio ya hapa na pale ngoja niwe na mwelekeo wangu.


sisi wenyewe kwa wenyeje tukajijenga na tukapena upeo au maujuzi ya mambo mbali mbali kama ,Elimu, maisha, vyakula, mapenzi, ndoa , maradhi, afya na mengineo.


basi tafadhali maswahibu hutukuta sote kina dada na kina kaka kina baba na akina mama so huu ni ukurasa wetu kujadili na kuzungumza pamoja.

kuhusu yale mambo yetu ya habari matukio na burudani  na mengineyo yake tutayasoma katika website yetu ya www.sophiakessy.com ila kwa  haya ya kawada ambayo twatakiwa tujadili basi tuzungumze nayo hapa hapa kwenye blog yako .

niandikie nitachapisha kasha kwa pamoja tutajadili tuma barua pepe yako kupitia

Email: sophia80tz@yahoo.com 
karibu sana nawajali na nawapenda mmno nategemea support yenu.




 

WANAPOPISHANA WASICHANA KWA WAVULANA @ HUGEUKA KUANGALIA NINI???

vitu vingine huwa ni vya kujiuliza tu hivi umewahi kujiuliza sikumoja labda umekatiza mitaa Fulani Fulani mkakutana na wasichana kwa wavulana labda katika pitapita zenu au hata kama uko pekeyako umewahi kufahamu ni kwanini vijana hugeuka hata kama umesimama ukasalimiana nae bado ukiondoka mkipishana tu lazima ageuge .

kama huja experience basi jaribu sikumoja mie huwa najiuliza huwa wangeuka kuangalia nini hasa???... ha ha ha ha lol dunia ina mambo ....

@ kina kaka hebu tuzungumze # girls talk...

RAFIKI YAKO UNAVYO MJALI NA KUMPENDA YEYE ANAFANYA UFANYAVYO??? ... ZUNGUMZA NA MIE SOPHIA KESSY



Kichaga huwa tunasema shimbonyi lanye??/  ( habari jamani)
Mambo zenyuuuuuuuuu? Ninatumai kuwa wote ni wazima wa afya  mie sijambo kabisa namshukuru Allah kwa nguvu zake I am doing very well…...


leo wakati naingia ofisini nikawa natafakari mambo mengi sana miongoni mwayo ni Marafiki…. Hivi umewahi kujiuliza una marafiki wa namna gani?? Sote kama wakina dada au hata vijana tuna wale ambao huwa tunawaita close friends … Wengine sikuhizi utasikia tunaambiana BFF (Best Friend Forever) hivi hii ni kweli huwa inatoka moyoni au tunadanganya kusukuma siku  ilihali nyuma ya migongo tukitakiana mabaya.... Mbuta nanga....
 


Inakuwaje pale Yule unaemjali na kumpa kipaumbele kama rafiki yako wa karibu anakutosa au kukusaliti na wakati mwingine anakuwa na wivu au chuki na wewe kwa yale ufanyao ilimradi tu hataki kuona ukifanikiwa na mwisho wa siku bado unamkubatia na kumwita rafiki wa ukweli???


Jamani au mie ndio sielewi maana ya rafiki hebu tuzungumze rafiki yako unamuonaje na unamchukuliaje je unavyomjali na kumpenda divyo anavyofanya kwao.

 


That’s it....zungumza na mie Sophia kessy kila wakati hapa hapa usisite kuacha comment zako tafadhali msicharurane huku mkatajana majina ha ha ha mie sitakuwemo lol nataka kina dada tujifunze na tutafakari …..
rafiki yako umtendeayo je ndio akutendeavyo ????? nangoja kusikia kutoka kwako best yangu..

Tuesday, June 25, 2013

Desperate HousegirlsDesperate Housegirls NI FILAMU ILIYOANDIKWA NA KUANDALIWA na muandaaji Uduak Isong Oguamanam. filamuhii pia imeongozwa na Desmond Elliot, na kuna mastar mbalimbali ka vile Ini Edo, Desmond Elliot, Kenneth Okolie, Tamara Eteimo, Mary Lazarus, pamoja na  Benjamin Tuitu.  movie hii inazinduliwa rasmi  July 26, 2013.
 
KWA UFUPI KUHUSU HADHITHI HUSIKA KATIKA MOVIE, 
wasichana wamakamo warembo na wenye upeo mzuri sana ambao wameishi kwa muda mrefu maisha yao ya kigeto geto . kwa kuwa wameyachoka baada ya kukaa kwa muda mrefu wanaamua kuwa house girls kwenye familia za kitajiri .lengo lao hasa likiwa ni kuwa matajiri kwa haraka au wafe wakiwa wanajaribu kutajirika sasa fuatilia zaidi movie hiyo uone moto wake hakika wameicheza viziri na wamejipanga .
 
 

The Tinsel 1000 Celebration

MSEMA CHOHOTO MAARUFU TOKA NIGERIA NA AMBAE PIA NI MTANGAZAJI WA REALITY SHOW KILA JUMAPILI KWENYE MAMBO YA EVECTION UNAKUTANA NAE NI IK OSAKIOUDUWA ALISHEREHESHA PAMOJA NA MWANA DADA OSAS IGHODARO.

Tinsel 1000 Party (1) - IK Osakioduwa and Osas Ighodaro
IK Osakioduwa and Osas Ighodaro


M-Net Africa, last Thursday (May 23), held an event to celebrate the 1000th episode of it’s soap opera, Tinsel. The event was held at the Eko Hotels and Suites, Victoria Island, Lagos.  eeeh hiyo ndo habari ya wanaija shuhuli ilifana vipi na watu walitoka vipi basi  fuatilia zaidi kwa picha hizo za matukio .

Biola Alabi
Biola Alabi
Keppy Bassey Ekpenyong
Keppy Bassey Ekpenyong
Omoni Oboli
Omoni Oboli
Susan Peters
Susan Peters
Funmi Holder
Funmi Holder
Linda Ejiofor
Linda Ejiofor
Tomi Odunsi
Tomi Odunsi
Osas Ighodaro
Osas Ighodaro
Yvonne Ekwere
Yvonne Ekwere
Uti Nwachukwu
Uti Nwachukwu
Julius Agwu
Julius Agwu
Tom Ogbeiwi
Tom Ogbeiwi
Taiwo Ajai-Lycett
Taiwo Ajai-Lycett
Fred Amata and Joke Silva
Fred Amata and Joke Silva
Segun Arinze and Oge Okoye
Segun Arinze and Oge Okoye
Gideon Okeke and Linda Ejiofor

Gideon Okeke and Linda Ejiofor
Praiz performing
Praiz performing
Tinsel 1000 Party (20)