Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Sunday, October 26, 2014

#TOP10MostGameChangers DIAMOND PLATNUMZ AMETAJWA KWENYE ORODHA HYO

DIAMOND PLATNUMZ AMETAJWA KWENYE ORODHA YA WASANII KUMI WA AFRICA WALIOFANYA MABADILIKO

   Mkali wa Ngoma ya "Mdogo Mdogo" Diamond Platnumz ametajwa kwenye Orodha ya wasanii Kumi Afrika waliofanya Mabadiliko (Top10 Most Game Changers).


Orodha hiyo imetolewa week hii kwenye Kipindi cha Top10 Most kinachoendeshwa na Joketi Mwengelo na Ice Prince kutoka Nigeria, Diamond Platnumz ameshikilia namba 10 pamoja na Fally Ipupa. Hii ndio List nzima 
1. 2face Idiba 
2.Boom Shaka 
3.D banj  & Don Jazzy 
4.K'naan -
5.Banky W  & Psquare 
6.Dj Jimmyyat & Dj Waxxy
7.Tiwa savage  & Wizkid ayo 
8.Ice Prince - Nigeria & Naetoc 
9.Mafikizoro & Mr. Flavour
10.Diamond Platnumz & Fally Ipupa

Saturday, October 18, 2014

MWANAMUZIKI WA KIMATAIFA T I AMETUA BONGO TAYARI KWAAJILI YA SERENGETI FIESTA 2014 LEO USIKU SAMBAZA UPENDO


Fiesta 2014 ni Sheedah. Sambaza upendo.
Kwa mara ya kwanza Serengeti Fiesta inakupa urahisi wa kufika eneo la tukio na kusambaza upendo.
Uhitaji kuuliza ni wapi. Ni pale pale Leaders Club.
Sasa mpango mzima umekaa hivi: Serengeti Fiesta inakupa usafiri wa BUREEE wa mabasi ya UDA kwako mkazi wa Dar es salaam. Vituo vya usafiri ni kama hivi: Kariakoo Big Bon, Magomeni Hospitali na Mwenge Puma Petrol Station. Mabasi ya yatakuwepo kuanzia saa 12 Jioni na yatakuwa na mabango ya fiesta. Na usafiri huu utakuwa ni kwenda na kurudi.
Fiesta 2014 ni Sheedah.



Thursday, October 16, 2014

WANAMUZIKI WA KIMATAIFA WAANZA KUWASILI KWA AJILI YA TAMSASHA LA SEREGETI FIESTA 2014

Jana Ms Victoria Kimani alivyo wasili jijini dar na Ladyhaha akapata kumuhoji kidogo...jamaniiiiiiiiii fiesta hii si yakukosa.. #Nisheedah#Sambazaupendo#FiestaFever
Photo: Jana Ms Victoria Kimani alivyo wasili jijini dar na Ladyhaha akapata kumuhoji kidogo...jamaniiiiiiiiii fiesta hii si yakukosa.. #Nisheedah#Sambazaupendo#FiestaFever


WAJE from nigeria  tayari ameshawasili  stay tune kwa fiest 2014 jumamosi @ Lidaz Club 


Guess who's on his way _ it's Davidoooooooo
Photo: Guess who's on his way _ it's Davidoooooooo

Sikiliza live interview ya Waje na Victoria Kimani ndani ya Cloud TV, Clouds fm na Choice fm mida hii......#Fiesta2014 #Nisheedah #SambazaUpendo na usikose kudondoka Leaders Club Jumamosi hii kuwaona live ndani ya jukwaa moja na T.I





TI on the way now

Tuesday, October 14, 2014

HAKUNA BINTI ASIE IPENDA TUSIDANGANYANE HATA MIE NAIWAZA SASA LOL HA HA HA KAMA UPO NIPE SABABU NA KINA KAKA PIA KARIBU TUJADILI

Anaeichukia hii (PETE) aniambie @ kina dada wenzangu hivi ni kweli ati mnaichukia??? kweli wangapi hawaipendi?  na wangapi wanaipenda wanawaza kila kukicha lini wataipa.

Nakumbuka niliwahi kuambiwa na rafiki yangu (binti) kuwa ikifika wakati kama binti unaeishi pekeyako utaanza kujiona mpweke na kutamani kuwa na familia na itafaika wakati utaachana na baba yako na mama yako na kuambatana na mwenzi wako  je umewahi kujiuliza hisia ulizonazo za kutaka kuolewa ni za kweli? au unataka ufanye hivi kwasababu fulani na yeye alifanya hivyo? au unafanya kwasababu nyumbani wanakutania unazeeka na wadogo zako wote wameshafanya hayo lol  au unafanya hivi kwasababu marafiki wanakusukuma ufanye hivyo? au unafanya kumkomoa x wako ili ajue na wewe unaweza kuolewa??? au unaolewa fashion ?? je anaetaka kukuchumbia umeridhika nae nichaguo la kweli la moyo wako je uko tayari au hujielewi hebu tujadili waungwana maana .

jana nilikuwa mahali nikawa naongea na rafiki yangu mmoja tukawa tunajadili jinsi umri unavyokimbia na miaka inavyo enda na bado tupotupo tu tukajikuta na maswali mengi sana juu ya kufanya uamuzi sahihi kabla ya kuitwa mke wa fulani na mwisho wa siku nikaona hebu leo nijadili na wewe. 



unadhani ni wakati gani uko sahihi kwako kuolewa au kuchumbiwa?

Mie huwa napenda sana kuwa muwazi kwako hebu na wewe kuwa muwazi kwangu  lol # its a agirls talk kina kaka mnaweza kujadili na nyie ha ha ha ha ha ha uwiii 

Mlio olewa na wale single ladies wenzangu hebu tulonge.

Nawapenda wote

KAMWE USIUDANGANYE MOYO WAKO 

PICHA 5 ZA WILIAM RUTO AKIKABIDHI OFISI KWA RAIS UHURU KENYATA ALIPO ILI


















DAIMA TUTAKUKUMBUKA BABA YETU WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Mimi pamoja na watanzania wenzangu kote ulimwenguni hapa nyumbani Tanzania  hii leo tunaadhimisha miaka kumi na tano sasa (15)   tangu kifo cha baba wa taifa langu mwalimu Julius kambarege Nyerere alipoiaga dunia, baba wa taifa hili aliaga dunia tarehe 14 mwezi 10 mwaka 1999.

Wakati ikiwa nchinzima hii leo iko katika mapumziko , ni sikuambayo wananchi wanatafakari kwa kina mengi uliyoyafanya na kutuachia hapa nyumbani wviongozi wetu mbalimbali wa hama na wadini bado wanaendelea kuwahimiza watanzania wenzangu  kuendelea kuyaenzi yale mazuri  aliyoyaacha  hayati baba wa taifa ambaye wakati wa uhai wake alisisitiza suala la amani na Umoja miongozi mwa watanzania na bara la Afrika.

Watanzania wengi wanamkumbuka baba wa taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alifariki Octoba 14 mwaka 1999 ikiwa ni miaka 15 sasa.

 Watanzania wanamuenzi mwalimu kwa mengi lakini kuu ni ile falsafa yake ya umoja ambayo ilimpelekea kuunganisha Tanganyika na Zanzibar.
Mwalimu Nyerere anaheshimiwa na watanzania wengi kwa uadilifu na moyo wake wa kutumikia kuliko kutumikiwa.

Julius Nyerere alizaliwa mwaka 1922 katika eneo la mashariki mwa Ziwa Victoria na alieshi katika maisha ya kawaida, ambapo baba yake alikuwa kiongozi wa kabila ndogo.

Alianza shule katika umri wa miaka 12 na alisomea taaluma ya ualimu katika Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda. Baada ya kufundisha kwa miaka mitatu alipata ufadhili wa kusomeshwa katika Chuo Kikuu cha Edinburgh.

Alifundisha Kiingereza, Kiswahili, na historia katika chuo kikuu cha jijini Dar es Salaam, na kutokana na mwenendo wake aliochaguliwa kuwa mkuu wa shirika la Tanganyika African Association.

Baba wa taifa bado tunakumbuka mengi mazuri uliyoyafanya kwa nchi yetu tunakumbuka pia ucheshi wako upendo na tabasamu lako pumzika kwa Amani, kamwe pengo uliloliacha ni kubw amno haliwezi kuzibika.

Kumbukumbu hii tunaifanya wakati ambapo nchi yetu ya Tanzania ikiendelea kukabiliwa na changamoto nyingi za kimaendelea ikiwemo kupambana na umasikini, rushwa na kupinga ujinga.

Monday, October 13, 2014

HONGERA SANA STEVE R&B KWA KUPATA JIKO

PICHAKWA HISANI YA MILLARD AYO BLOG
Ni mwanamuziki wa bongofleva ambae ameweza kutikisa na nyimbo kama Tabasamu  aliyoshirikiswa na Mr Blue siku ya  October 11 mwaka  2014 ameamua kujinyakulia jiko na kufunga  ndoa takatifu katika kanisa la Word Alive Sinza Mori Dar es salaam….
 
 Steve na mke wake Easter. hawajaishana sana kiumri ambapo Steve ana umri wa miaka 28 na mke wake Easter ana umri wa miaka 25.
 yasemekana kuwa Wawili hawa walianza kuwa pamoja kwenye uhusiano wa kimapenzi toka wakiwa High School miaka nane iliyopita shuleni St. Mathew kisha walikwenda wote chuo IFM na kusoma pamoja.
pongezi nyingi kwenu kwa uamuzi mzuri na wabusara mliochukua kila la kheri Ester na Steve kwa kufunga ndoa daima mtangulizeni MUNGU kwa kila jambo mfanyalo.

Sunday, October 12, 2014

BOKO HARAM YAWAACHIA MATEKA 27

Rais wa Cameroon amesema kuwa mateka 27 wakiwemo raia 10 wa Uchina wameachiliwa na kundi la wanamgambo wa Boko Haram.

Raia hao wa China walitekwa nyara mwezi mei wakati kampuni moja ya China ilipovamiwa karibu na mpaka wa Nigeria.

Wengine walioachiliwa ni pamoja na mke wa naibu waziri mkuu nchini Cameroon aliyetekwa nyara mwezi Julai.

DOLA BILIONI 4 ZAHITAJIKA KUIJENGA GAZA MPYA MKUTANO WA KUIKARABATI WAANZA MJINI CAIRO

Wafadhili wamekusanyika mjini Cairo, Misri ili kujadili misaada inayohitajika kwa ajili ya kukarabati Ukanda wa Gaza ulioharibiwa katika mashambulizi ya hivi karibuni kati ya utawala wa Kizayuni wa Israel.




Mamlaka ya Ndani ya Palestina imesema kuwa dola bilioni 4 zinahitajika kwa ajili ya kujenga tena Ukanda wa Gaza. 

UTAFITI WAONYESHA VIAGRA HUSABABISHA UPOFU

kwa mujibu wa utafiti uliofanyika  ni kwambaWatafiti nchini Australiawanasema  dawa inayotumiwa kuongeza nguvu za kiume VIAGRA inasababisha upofu (kutoona) mara baada ya matumizi ya muda mrefu.

kwamujibu wa Watafiti hao kutoka Australia, wanasema kuna chembechembe fulani katika dawa hiyoinayotumiwa an wanaume kuongeza nguvu za kiume hasa na wale wanaopatwa na matatizo ya kukosa nguvu za kiume, ya kuwa huathiri uwezo wa kuona miongoni mwa wanaume ambao wana ugonjwa wa macho.

katika ripoti ya gazeti la Nation nchini kenya, Madaktari nchini Australia wamebaini kwamba chembechembe hiyo ndani ya dawa inaweza kusababisha upofu miongoni mwa wanaume wenye tatizo la ugonjwa wa macho.

wameongeza kuwa dawa hiyo pia inaweza kuwaathiri watumiaji ambao wanaona vizuri.

Utafiti huo uliofanywa katika panya,ulibaini kwamba hata watu wasio na ugonjwa wa macho wanaweza kuathirika.

Friday, October 10, 2014

MALALA NA SATYARTHI WASHINDA TUZO YA AMANI YA NOBEL

Mwanaharakati mwenye umri mdogo kutoka nchini Pakistan,

Malala Yousafzai pamoja na mwanaharakati mwingine wa maswala ya watoto nchini Idnia Kailash Satyrathi, wameshinda tuzo ya amani ya Nobel.

Malala mwenye umri wa miaka 16, ni mshindi mdogo zaidi kuwahi kushinda tuzo hiyo katika historia yake.

Malala amekuwa akiendeleza harakati zake za kutaka watoto wa kike kuweza kupata elimu.

Alipigwa risasi kichwani na kundi la Taleban nchini Pakistan mwaka 2012 kwa kutetea wasichana kupata elimu.

MTAMBUE MWANADADA LAETITIA MELODY NAFASI KWA WANAWAKE WOTE AFRIKA WANAOIBUKIA KIMUZIKI




Muziki ni dawa muziki ni faraja burudani na kila kitu hebu farijika burudika na utibike na ngoma  mpya kutoka kwa binti wa afrika.

kila ijumaa kipengele chetu hiki kitaitwa nafasi kwa wanawake wote afrika wanoibukia kimuziki.


Mimi kama mimi Sophia huwa naamini kabisa kwamba muziki ni kila kitu ukiwa na mawazo ukiwa  maswahibu yako muziki ndio tulizo la moyo wako au sio sasa basi kama wakubaliana na mie, kwanza tukubaliane kuwa sikuhizi hakika muziki unabadilika sana na kina dada wengi wanajitosa kuimba sana tena ni mahodari mmo maana kina dada tumejaaliwa sautui tamu sana hasa ukijua kuitumia , si tu hapa nyumbani Tanzania ila kila nchi, kina dada naona wameamka na kutambua kumbe muziki nao unalipa na sikulipa tu unaburudisha, basi naomba kila wiki hasa kila ijuma,hapa hapa kwenye blog yetu hii niwe na kipengele cha kumtambulisha mwanamuziki mpya mwanamke toka Afrika ambae kwangu naona anastahili kutambulishwa kwa wadau kisha tumuunge mkono,  kwa kuanza tuanze kumtambua mwadada huyu.



Binti huyu amezaliwa Congo