Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, October 9, 2014

MAPISHI YA VIPAPATIO VYA KUKU NA PILIPILI MBOGA JARIBU NA WEWE.


Vipapatio vya kuku 20, pilipili mboga gramu 300, tangawizi gramu 150, vitunguu maji, gramu 5, pilipili manga gramu 5, unga wa pilipili
hoho kijiko kimoja, mchuzi wa sosi kijiko kimoja, chumvi vijiko vitatu.

NAMNA YA KUPIKA KWA UFUPI SANA 
 
1. kata kila kipapatio kiwe vipande vitatu, kata pilipili mboga iwe slesi, kata tangawizi, vitunguu maji viwe vipande 

2. washa moto tia mafuta kwenye sufuria, tia vipande vya vipapatio kwenye sufuria, korogakoroga tia vipande vya vitunguu maji na tangawizi, korogakoroga, tia pilipili manga na unga wa pilipili hoho kwenye sufuria, korogakoroga mimina mchuzi wa soya, tia pilipili mboga korogakoroga, tia chumvi korogakoroga. Ipakue mpaka hapo kitoweo hiki kiko tayari kuliwa kwa ugali au wali au chochote upendacho.

No comments:

Post a Comment