Taasisi ya lishe tanzania
imeshitushwa  na asilimia 42 za  takwimu 
za udumavu  kwa watoto
walio chini ya miaka mitano na hivyo ni sababu mojawapo inayochangia baadhi ya
watahiniwa wa darasa la saba kutofanya vizuri katika  mtihani wa taifa
mkoani simiyu.  
Akitoa elimu ya uhamasishaji ,kwa
wawakilishi wa wakurugenzi wa halmashauri   ,maafisa mipango na
waganga wakuu mkoani simiyu , afisa lishe wa mkoa wa iringa ambaye ni
mwezeshaji mshauri kwa viongozi ngazi ya mikoa  na halmashauri mwita waibe
amesema kuwa huu ni   mkakati wa kitaifa wa utoaji  elimu nchi
nzima,ikiwa ni kutekeleza agizo la rais jakaya kikwete ambalo kimsingi alitoa
agizo kuwa ,viongozi wote wapewe elimu ya lishe ili kuwajengea uelewa wa namna
ya kusukuma masuala ya lishe ambayo yanaliathiri taifa ambapo   kati
ya watu ,100,42 wamedumaa.
Katika mjadala huo wa lishe mganga
mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa bariadi dr godfrey MPANGALE
akazitupia lawama mamlaka ya chakula na dawa TFDA NA shirika la viwango
Tanzania tbs kwa kushindwa kudhibiti bidhaa ambazo hazina na ubora na kuleta
madhara kwa watumiaji bidhaa hizo.
Naye katibu tawala wa mkoa wa simiyu
mwamvua jirumbi amewataka watendaji kuwajibikaji kwa kila mmoja kwa nafasi yake
ili kuweza kulitokomeza tatizo la udumavu lililofikia asilimia 42 .
 

No comments:
Post a Comment