African music is on my blood Back to my root Proud to be Africa,be your self #lets talk about African culture,tourism music ,life style, business,technology, money, fashion, Love, Marriage, Health, food, animals,and so on!!!!
Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, November 7, 2012
KUKAMATWA KWA WATUHUMIWA ZAIDI WA MAUAJI YA BARLOW HATIMAYE RADIO CALL, FUNGUO ZA GARI ALILOKUWA NALO MAREHEMU VYAPATIKANA
Radio call (simu ya upepo) iliyokuwa ikitumiwa na aliyekuwa kamanda wa jeshi la polisi Mwanza marehemu Liberatus Barlow hatimaye imenaswa ikiwa imefichwa kwenye shimo la maji taka (septic tank) kwenye moja ya nyumba eneo la Nyashana jijini Mwanza.
Kunaswa kwa Radio call hiyo kumekuja kufuatia kukamatwa kwa watu wengine watatu zaidi wakituhumiwa kuhusika na mauaji hayo.
Watu hao waliokamatwa mara baada ya kutajwa na washirika wenzao watano ambao tayari wako mahabusu ni pamoja na Abdalah Petro Ndayi (32) mkazi wa Mjimwema jijini Mwanza, Abdalahman Ismail (28) mkazi wa Mkudi Ghana, na Lyoba Matiku anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 46-50 akiwa ni mkazi wa Nyakabungo jijini Mwanza huyu anatajwa kuwa ndiye mfadhili wa kundi hilo la ujambazi na mipango yote ya uvamizi hufanyika kwake.
Msikilize kwa kubofya play Mkuu wa kitengo cha upelelezi wa makosa ya Jinai wa Jeshi la polisi mkoani Mwanza, Joseph Konyo anafafanua zaidi...
Vielelezo vingine vilivyokamatwa nyumbani kwa mtuhumiwa Abdalah Petro Ndayi ni pamoja na Ufunguo mmoja wa gari alilokuwa akiendesha Kamanda Liberatus Barlow siku ya tukio, sim card za mitandao mbalimbali, simu nne za mkononi kila moja ikiwa na laini yake, kofia mbili aina ya barreti kati ya hizo moja ni ya polisi na nyingine ni ya kampuni ya ulinzi.
Vielelezo vingine ni sare moja (suruali na shati) ya rangi ya blue yenye mstari mweupe ya moja ya makampuni ya ulinzi jijini Mwanza, suruali moja ya kaki inayofanana na sare za mgambo wa jiji la Mwanza ikiwa na masalia ya damu kwenye pindo la suruali kwa nyuma, kipande cha nondo, bisibisi na sare inayotumiwa na askari wa polisi kikosi cha kutuliza ghasia FFU...
|
PICHA NA HABARI ZA TUKIO NI KW AHISANI YA ALBAT G SENGO WA MWANZA
BENDI YA MSONDO KUZINDUA VYOMBO VIPYA LIDAZ CLUB IJUMAA
BENDI Kongwe ya mziki wa dansi nchini Tanzania Msondo Music inatarajia kuzindua vyombo vyake vipya kabisa walivyokabidhiwa hivi karibuni na Kampuni ya KONYAGI akizungumza na waandishi wa habari msemaji wa bendi hiyo Rajabu Mhamila 'Super D' amesema tumeshapewa vyombo na Konyagi ambavyo tutavizindua mbele ya mashabiki wetu siku ya Ijumaa pale LIDAZ CLUB siku ya Ijumaa hivyo wapenzi wote wa bendi ya Msondo mnaombwa kuhudhuria kwa wingi ili kuona vyombo vipya
Pamoja na kupata burudani za bendi hiyo zikiwemo nyimbo za zamani na za sasa kwa ajili ya kuanza wik end Super D aliongeza kwa kusema wapenzi watakaokuja siku hiyo watapata burudani za radha tofauti tofauti kwani wamepanga kukonga nyoyo za mashabiki wao kwa kutumia vyombo vyao vipya
Bendi hiyo siku ya Jumapili itamaliza burudani za wik end katika ukumbi wa Max Bar Ilala bungoni
Mkurugenzi wa Bendi hiyo Muhidini Maalimu Gulumo ataongoza kundi zima la wana msondo ngoma akiwemo Said Mabera, Shabani Dede, Romani Mn'gande, Eddo Sanga, Juma Katundu, Hassani Moshi na wendine kibao kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki.
ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI LA SHINYANGA AFARIKI DUNIA
![]() |
Padri KUBEJA amesema kuwa mipango ya mazishi inafanyika jimboni shinyanga na kuwataka waumini wa kanisa hilo kuwa watulivu... Msikilize kwa kubofya Play |
TANZIA
JOPO LA WASHAURI WA ASKOFU JIMBO KATOLIKI SHINYANGA KWA NIABA YA MAPADRE, WATAWA, WALEI NA WATU WOTE WENYE MAPENZI MEMA JIMBO KATOLIKI SHINYANGA.WANASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA MHASHAMU ASKOFU ALOISIUS BALINA ASKOFU WA JIMBO KATOLIKI SHINYANGA KILICHOTOKEA LEO TARAHE 6 NOVEMBER 2012 SAA 5:00 ASUBUHI KATIKA HOSPITALI YA RUFAA BUGANDO.
HABARI ZIWAFIKIE MAASKOFU, MAPADRE, WATAWA NA WAUMINI WOTE POPOTE WALIPO.
MIPANGO YA MAZISHI INAANDALIWA JIMBONI SHINYANGA.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIHIMIDIWE.
IMETOLEWA NA
MKURUGENZI WA HABARI
JIMBO KUU LA MWANZA
PADRE CHRISTOPHER KUBEJA
OBAMA ASHINDA KUIONGOZA MAREKANI KWA MIAKA 4
Ni miaka minne mingine kwa rais Barack Obama. Rais huyo wa kwanza mweusi kuliongoza taifa kubwa zaidi duniani ametangazwa asubuhi ya leo kuwa mshindi katika mchuano mkali na wa aina yake.
Ilikuwa ni kama ndoto iliyozimika katika makao makuu ya kampeni ya Mitt Romney mjini Alabama wakati matokeo yakianza kumiminika hasa kutoka katika majimbo yenye maamuzi ambayo yote yalikuwa yanaelekea kwa rais Obama. Wakati kimya kikitanda katika kambi ya Romney na wafuasi wake wakionekana kutoamini kilichotokea, jimboni Chicagohali ilikuwa ya nderemo na vifijo.
Wafuasi wa chama cha Democrats wakishangalia wakati matokeo yakiendelea kutolewa.
Mitt Romney ameshinda kura ya umma kwa asilimia 50 lakini mfumo wa Marekani unazingatia kura za majimbo kupata mshindi. Obama ameshinda licha ya rekodi mbaya ya uchumi na ukosefu mkubwa wa ajira. Hakuna raia aliyewahi kupata muhula wa pili tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia, kukiwa na ukosefu wa ajira wa zaidi ya asilimia 7.2. Kiwango cha sasa ni asilimia 7.9.
Matokeo yalianza kwa kutangazwa ushindi wa Rais Obama katika jimbo la Vermont, yakifuatia majimbo ya Delaware, Maryland, Michigan, Pennyslivania, Wisconsin na New Hampshire . Kwa na mpinzani wake Mitt Romney alinyakua ushindi wa mikoa inayofahamika kuegemea upande wa chama chake cha Republican, ikiwa ni pamoja na Kentucky, Tennese, South Carolina, West Virginia na Indiana.Tuesday, November 6, 2012
Uchaguzi waanza Marekani
Uchaguzi waanza Marekani
Wapiga kura nchini Marekani wameanza zoezi la kumchagua rais atakaeiongoza nchi yao kwa miaka minne ijayo. Hadi siku ya mwisho ya kampeni, kura za maoni ziliwaonyesha wagombea wawili wa wadhifa huo, Rais Barack Obama na mpinzani wake wa chama cha Republican Mitt Romney wakiwa nguvu sawa, ingawa Obama anaonekana kuongoza kwa kiwango kidogo.
Akitoa rai ya mwisho kwa wapiga kura, Mitt Romney alisema mlango uko wazi kwa ushindi.
Rais Obama alitoa rai sawa na hiyo kwa wanaomuunga mkono jimboni Ohio. Kwa upande mwengine Warepublican wamelalmika juu ya kimbunga kilichoikumba Marekani wiki iliyompita kwamba kumepunguza kasi ya mgombea wao.
Akitoa rai ya mwisho kwa wapiga kura, Mitt Romney alisema mlango uko wazi kwa ushindi.
Rais Obama alitoa rai sawa na hiyo kwa wanaomuunga mkono jimboni Ohio. Kwa upande mwengine Warepublican wamelalmika juu ya kimbunga kilichoikumba Marekani wiki iliyompita kwamba kumepunguza kasi ya mgombea wao.
Monday, November 5, 2012
Arusha Artists na track "Arusha Kilele"
CHECK OUT:AFTER PARTY YA FETTY BAADA YA KUGRADUATE
Pichani ni Washikaji wakipata msosi wa nguvu
Nikki wa pili kwa mbaali namuona Dina Marios
Antu Mandoza akipata msosi wa nguvu kabisa
B Twelve na Faraja
Shilole
Warembo
Ncha kali
Darasa
B Dozen
Muli B
Sofia
Darasa
B dozen
Thats ma girl Shade
Kulia,Faraja na kushoto kwangu ni Millard Ayo
Soudy Brown
Cute couple Issa and Nurie
Muna mindu weeeeeee, Burudani mwanzo mwisho
DeeAndy,Soudy Brown,Ncha kali
Tumetokelezeakwa hisani ya dj fetty blog
SERIKALI KUTOA DAWA ZA KUTIBU KISUKARI BURE KWA WATANZANIA WENYE TATIZO HILO.
Serikali imetangaza kutoa bure dawa za kutibu ugonjwa wa kisukari ili kuokoa maisha ya watanzania wanaokabiliwa na ugonjwa huo kutokana na kuwepo kwa ongezeko la wagonjwa wa kisukari kwa siku za karibuni.
Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii SEIF RASHID amesema hatua hiyo ya Serikali imefikiwa kutokana na kupatikana kwa gharama kubwa kwa dawa za ugonjwa wa kisukari na kuwa watu wanaokabiliwa na ugonjwa huo wanapaswa kutumia dawa hizo kwa maisha yao yote huku idadi kubwa wakiwa ni watoto.
Kauli hiyo ya Serikali imekuja kufuatia swali la Mbunge wa Viti Maalum SUSAN LYIMO ambaye ameiomba Serikali kutoa bure dawa za ugonjwa wa kisukari kama ilivyo kwa dawa za kutibu magonjwa mengine sugu ikiwemo UKIMWI
Saturday, November 3, 2012
WEEKEND NJEMA NAKUACHA NA MAPISHI YA NYAMA YA NGOMBE NA MAHARAGWE
Mapishi ya nyama ya ng'ombe na maharagwe
Mahitaji |
Rais Kikwete azindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela - Arusha (NM-AIST)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua sanamu ya Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012. Pamoja naye ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali ambaye ndiye Mkuu wa Chuo hicho, WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Burton Mwamila, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulugo,
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali ambaye ndiye Mkuu wa Chuo hicho katika sherehe za uzinduzi wake rasmi Ijumaa Novemba 2, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya utafiti wa dawa asilia toka kwa Meneja Mauzo wa kampuni ya madawa asilia ya Moringa Natural Products Bi. Christina Ngoty wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya utafiti wa mitishamba toka Dkt Efrem Akilei Njau wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari wakati uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu wa zamani Mzee Edwin Mtei wakati uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Wageni waalikwa wakimshamgilia Rais Kikwete baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Subscribe to:
Posts (Atom)