![](https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhnf7uL7FMKaqb3A2rzD7beYbyHC_kcJPapz1tJebM8454OYw1YAkDli9sr1tyWgkvm2JCjoOGFdYgitZvPOQUFzfYVvQfzJhGQPXyRiamT8ecwGM9T8rXpzXFGX-Cb_YU2k59eBj_3eXDp/s320/ma42.jpg)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua sanamu ya Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Mzee Nelson Mandela wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012. Pamoja naye ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali ambaye ndiye Mkuu wa Chuo hicho, WAZIRI wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa, Makamu Mkuu wa Chuo hicho Profesa Burton Mwamila, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Magessa Mulugo,
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali ambaye ndiye Mkuu wa Chuo hicho katika sherehe za uzinduzi wake rasmi Ijumaa Novemba 2, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya utafiti wa dawa asilia toka kwa Meneja Mauzo wa kampuni ya madawa asilia ya Moringa Natural Products Bi. Christina Ngoty wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo ya utafiti wa mitishamba toka Dkt Efrem Akilei Njau wakati wa uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Arumeru Mashariki Mhe Joshua Nassari wakati uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu wa zamani Mzee Edwin Mtei wakati uzinduzi rasmi wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
Wageni waalikwa wakimshamgilia Rais Kikwete baada ya kuzindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela jijini Arusha Ijumaa Novemba 2, 2012.
No comments:
Post a Comment