Ni miaka minne mingine kwa rais Barack Obama. Rais huyo wa kwanza mweusi kuliongoza taifa kubwa zaidi duniani ametangazwa asubuhi ya leo kuwa mshindi katika mchuano mkali na wa aina yake.
Ilikuwa ni kama ndoto iliyozimika katika makao makuu ya kampeni ya Mitt Romney mjini Alabama wakati matokeo yakianza kumiminika hasa kutoka katika majimbo yenye maamuzi ambayo yote yalikuwa yanaelekea kwa rais Obama. Wakati kimya kikitanda katika kambi ya Romney na wafuasi wake wakionekana kutoamini kilichotokea, jimboni Chicagohali ilikuwa ya nderemo na vifijo.
Wafuasi wa chama cha Democrats wakishangalia wakati matokeo yakiendelea kutolewa.
Mitt Romney ameshinda kura ya umma kwa asilimia 50 lakini mfumo wa Marekani unazingatia kura za majimbo kupata mshindi. Obama ameshinda licha ya rekodi mbaya ya uchumi na ukosefu mkubwa wa ajira. Hakuna raia aliyewahi kupata muhula wa pili tangu kumalizika kwa vita vikuu vya pili vya dunia, kukiwa na ukosefu wa ajira wa zaidi ya asilimia 7.2. Kiwango cha sasa ni asilimia 7.9.
Matokeo yalianza kwa kutangazwa ushindi wa Rais Obama katika jimbo la Vermont, yakifuatia majimbo ya Delaware, Maryland, Michigan, Pennyslivania, Wisconsin na New Hampshire . Kwa na mpinzani wake Mitt Romney alinyakua ushindi wa mikoa inayofahamika kuegemea upande wa chama chake cha Republican, ikiwa ni pamoja na Kentucky, Tennese, South Carolina, West Virginia na Indiana.
No comments:
Post a Comment