Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, November 9, 2015

RAIS DKT JOHN MAGUFILI AKIZUNGUMZA LEO WAKATI WA ZIARA YA GHAFLA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI

RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANI DKT JOHN POMBE MAGUFULI AMEFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MUHIMBILI .

KATIBU MKUU KIONGOZI OMBENI SEFUE AZUNGUMZIA ZIARA YA RAIS DKT JOHN MAGUFULI MUHIMBILI

BAADA YA KUFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA MUHIMBILI LEO,RAIS DKT MAGUFULI AMEVUNJA BODI YA UONGOZI WA HOSPITALI HIYO NA KUTEUA UONGOZI MPYA HABARI ZAIDI ZITAKUFIKIA.

Papaa WEMBA afanya Maajabu " KARIBU MUSIC FESTIVAL"


DSC_1032DSC_1032

Mwanamuziki nguli wa dansi kutoka DRC Congo, Papaa Wemba kushoto akiimba na kucheza sambamba na madansa wake jukwaani usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la muzuki la Karibu Music Festival msimu wa pili linaloendelea katika viwanja vya Mwanakalenge,mjini Bagamoyo. 

Na Andrew Chale

 Mwanamuziki kutoka Congo mwenye makazi yake nchini Ufaransa, Papaa Wemba, ameweza kuonyesha ukomavu wake kwenye muziki wa dansi licha ya kuwa na uri wa miaka 66, kwa kupiga shoo ya aina yake usiku wa kuamkia leo kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015 linaloendelea ndani ya viwanja vya Mwanakalenge, Bagamoyo-Tanzania.

Katika shoo hiyo, Papaa Wemba aliweza kupanda jukwaani akiwa na bendi yake na kupiga nyimbo zaidi ya tano zilizokonga nyoyo mashabiki lukuki waliofurika ndani ya viwanja hivyo vya Mwanakalenge mjini hapa.

Papaa Wemba ambaye anatamba kwa muda mrefu na wimbo wa “Show Me The Way” ameweza kuwa miongoni mwa wasanii wa muziki wa dansi kutoka DRC Congo kufika Tanzania kwa mara ya pili sasa kwa vipindi tofauti huku watanzania wengi wakionyesha kumkubali na kufuatilia muziki wake mara kwa mara.

Baada ya shoo hiyo Papaa Wemba aliwashukuru Watanzania kwa kujitokeza kwa wingi na kumuunga mkono katika muziki wake ambapo alieleza kuwa tamasha hilo la Karibu Music Festival licha ya kuwa change kwa kufanyika mwaka wa pili, huko linakoelekea litakuwa kubwa zaidi na kuwa maarufu.

Katika shoo hiyo, Papaa Wemba aliimba nyimbo zaidi ya nne huku akiimba pia vibao kadhaa vilivyowahi kutamba miaka ya nyuma pamoja na nyimbo mbalimbali zikiwemo mpya.

Tamasha hilo ambalo leo Novemba 8.2015, linatarajiwa kufikia tamati, linaratibiwa na Karibu Cultural Promotions Organization (KCPO) na Legendary Music Entertainment and Promotions Co. Ltd, T kwa kushirikiana na kampuni ya kinywaji cha Jebel Coconut. Wadhaminiwa wengine ni pamoja na Swiss Embassy, Precision Air, Coca Cola, Mwananchi Communication, Kaya fm, Magic fm, Focus Outdoor, Jovago, Kaymu na Time tickets.

DSC_1025
Papaa Wemba akiimba jukwaani kwenye tamasha la Karibu Music Festival 2015, usiku wa kuamkia leo kwenye viwanja vya Mwanakalenge, mjini Bagamoyo.

DSC_1083DSC_1099DSC_1030
Dansa akifanya yake jukwaani..

DSC_1063DSC_1080DSC_1090
Mwenyekiti wa tamasha la Karibu Music Festival, Amarido Charles (kushoto) akiwa pamoja na mwanamuziki kutoka Afrika Kusini, Bodenim 'Bo' katika viunga vya tamasha hilo viwanja vya Mwanakalenge..