Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, February 28, 2013

‘MAPACHA WATATU’ KUZINDUA ALBAM YARABI NAFSI

Waimbaji wa bendi ya Mapacha wa tatu Khalidi Chokolaa (kushoto) na Jose Mara wakiwa wameshika CD ya albam yao mpya  jijini Dar es salaam jana 27/2/2013 watakayoizindua March 2 / 2013 katika ukumbi wa bussines park.

 

Msanii wa bendi ya mapacha watatu Catherine Fidelic ' Cindy' akiimba mbele ya wana habari


Mmoja wa wanamuziki wa kundi la mapacha watatu Kambi Seif akiimba moja ya wimbo wa bendi hiyo.

Picha kwa hisani ya michuzi .

TUZINDUE NA MAPACHA JAMANI WATOTO WA NYUMBANI NYUMBANI NI NYUMBANI

HII SI YA KUKOSA WAJAMENI

Monday, February 25, 2013

MENO 18 YA TEMBO YAKAMATWA MOROGORO

Vipande 18 vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi milioni ishirini na tisa laki saba sabini na sita elfu  vimekamatwa kwa ushirikiano wa jeshi la polisi mkoani Morogoro na hifadhi ya Udzungwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia mwema huku wahusika waliokuwa wakisafirisha nyara hizo kutelekeza gari vilivyokuwamo vipande hivyo
            (picha kutoka maktaba)
Akizungumza na Clouds Fm kamanda wa jeshi la polisi mkoani Morogoro Faustine Shilogile amesema kuwa tukio hilo lilitokea  februari 23 mwaka huu majira ya saa saaa 11:00 jioni katika eneo la  la Mto Mwaya Mang’ula wilayani Kilombero ambapo askari polisi walipata taarifa ya kuwepo gari lenye namba T 557 AYR aina ya Toyota mark II yenye rangi ya kijivu ikiwa na watu wawili ndani iliposimamishwa watu hao walishuka kwenye gari na kukimbilia porini huku wakilitelekeza  gari hilo ambalo ndani yalikuwamo meno hayo.



Naye mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Udzungwa Vitalis Uruka amesema kuwa vipande hivyo vya meno ya tembo vinadaiwa kupatikana maeneo ya Ifakara au Mahenge na  ni tukio la muda mrefu na kwamba wwatatumia gari hilo lililotelekezwa na watu hao kuwapata wahusika

PICHA ZA MSIBA WA GOLDIE, MUME WAKE NA WENGINE WALIOHUDHURIA.

.
Andrew Harvey mume wa Goldie.
.
Dada wa Goldie akiwa na marafiki
.
.
Wa pili kutoka kushoto ni mtangazaji wa Channel O Denrele Edun ambae alikua rafiki mkubwa wa Goldie na ndioGoldie alifia mikononi mwake akiwa amembeba, huu msiba ulihudhuriwa na watu wachache walioalikwa tu huko Ikoyi Lagos Nigeria.
.
.
.
.
.
.
.
Mwimbaji Tiwa Savage na mchumba wake.
.
Gazeti la Daily Post liliripoti leo asubuhi kwamba msanii Goldie ambae aliiwakilisha Nigeria kwenye jumba la Big Brother 2012 anazikwa leo, baada ya muda kupita ndio nimezipata hizi picha za msiba wa Goldie ambae alifariki siku ya Valentine feb 14 2013.
Imeripotiwa kwamba manenoya mwisho ya Goldie yalikua ni kumuomba baba yake amuombee apone maumivu makali ya kichwa aliyokua nayo ambapo Daily Post wameripoti tena kwamba staa huyo alifariki akiwa njiani kupelekwa hospitali, foleni ya magari siku hiyo ya wapendanao ilichangia kuchelewa kufika hospitali.
Chanzo mojawapo cha kifo chake ni shinikizo la damu na maradhi ya moyo.

HABARI HII KWA HISANI YA MILARD AYO BLOG.

Wednesday, February 20, 2013

IDHAA YA KISWAHILI YA DW YATIMIZA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWAKE.


Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle leo inaadhimisha miaka 50 tangu ilipoanzishwa na kuanza kurusha matangazo yake  tarehe 1 Februari 1963 na kusikika katika maeneo ya Afrika Mashariki na Kati.


 (Nikiwa pamoja na Adrea Schmidt ambae ni mkuu wa idhaa ya kiswahili wa Radio (DW) Deutshche Welle mara baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo 20/2/2013 katika ukumbi wa umoja house hapa jijini Dar es saalam. )

Deutsche Welle inaadhimisha miaka 50 ya idhaa yake ya Kiswahili
chini ya maudhui ya “Maarifa na Mwamko“ katika hafla maalumu itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Kwa nusu karne, Deutsche Welle (DW) imekuwa ikitangaza taarifa na habari
za uhakika kwa lugha ya Kiswahili kwa ajili ya wasikilizaji kwenye maeneo ya
Mashariki mwa Afrika na eneo la Maziwa Makuu.

Tarehe 22 Februari, saa 9.oo mchana katika jengo la Makumbusho ya Taifa, DW itasherehekea
maadhimisho haya kwa hafla maalumu jijini Dar es Salaam, Tanzania, ikiwaleta
pamoja wachambuzi wanaoheshimika katika mjadala wenye maudhui ya
“ Maarifa na Mwamko kupitia Vyombo vya Habari“.




Hotuba maalumu zitatolewa kwa lugha ya Kiingereza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter Brandes, na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt.

“Idadi kubwa ya wasikilizaji wanaoishi hapa Tanzania, kwa hivyo lilikuwa chaguo la uhakika kwa ajili ya sherehe zetu,“ alisema Andrea
Schmidt. “Kwa miaka 50 iliyopita, DW imejitolea katika utoaji wa habari
zenye uwiano na taarifa za uhakika, ikiwapa watu wa Afrika ya Mashariki
habari na uchambuzi wa kina juu ya masuala yenye uzito mkubwa.“

Uchambuzi utafanywa na jopo la majadiliano lililotayarishwa kwa msaada
wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) ofisi ya Dar es Salaam na
utafanywa kwa lugha ya Kiswahili. Mohammed Khelef wa DW ataongoza
majadiliano hayo akiwa na wataalamu wa vyombo vya habari wanaoheshimika
nchini Tanzania, akiwemo Assah Andrew Mwambene (Mkurugenzi

waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali tulijumuika nao pamoja  
 nikifuatilia kwa umakini kabisa mkutano huo







Tuesday, February 19, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WANACHAMA WA SIMIYU COMMUNITY BANK LEO IKULU‏


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam, kumwelezea mipango ya kufungua benki hiyo itayoshirikisha jamii katika mkoa huo mpya na ya jirani katika azma ya kumkomboa mjasiriamali na mkulima
mdogo.

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na  na ujumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam



Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana  na wajumbe wa Benki ya Jamii ya Simiyu (Simiyu Community Bank) uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam

KANISA LA CHOMWA MOTO VIZIWANI ZANZIBAR

 
SIKU TATU TU ZIMEPITA BAADA YA PADRE KUUWAWA -'KANISA JINGINE LA POOL OF SILOAM LACHOMWA MOTO VISIWANI ZANZIBAR' ( TUNAELEKEA WAPI? AMANI IPO WAPI? WATU WANAOGOPA HATA KUSALI MAKANISANI SIKU HIZI UNAPOTOKA HUNA UHAKIKA WA KURUDI NYUMBANI UKIWA SALAMA EEH MWENYEZI MUNGU TUSAIDIE WAJA WAKO.)

Monday, February 18, 2013

SAFARI YA KISIWANI MBUDYA ILIVYOKUWA

SORRY FRIENDS I HAVE BEEN SO BUSY WITH STUDIES AND WORK NDIO MAANA NACHELEWA KUWEKA PICHA ZA MATUKIO KISIWANI MBUDYA PLZ NAOMBA MNIVUMILIE WHEN I GET TIME SOON WILL PUT MORE PICS NA HABARI ZAIDI LOVE YOU ALL ENJOY.


 taratibu tukaanza kusogea
 dogo langu merry kessy na yeye alijumuika na ma single girls kuenjoy kisiwani mbudya
 hapa tukielekea kufuata boti kubwa inayoonekana pichani chini


 baba jonii hakukosekana Adam Mchomvu na yeye yumo
 misosi pia ilikuwepo
 aah mie nikapozi kupata upepo
 kimodo nae muoga ndani ya life jacket

 waliobaki wali lala kisiwani humo 
 raha jipe mwenyewe ukisubiri kupewa utazeeka bila kuzipata

 sitii neno hapo kilaji

 kisiwa cha ukweli
 mtu na dada yake




PICHA ZAIDI NIKIPATA TU TIME NITAZIWEKA THANKX