Rais wa China anayemaliza muda wake Hu Jintao, ameonya kuwa rushwa inatishia mustakabali wa chama tawala cha kikomunisti na taifa hilo kwa ujumla, huku akiahidi mageuzi wakati akifungua mkutano mkuu wa chama hicho.
Mkutano huo wa wiki nzima na unaotizamiwa kutetua viongozi wapya wa chama na taifa, unahudhuriwa na wajumbe elfu mbili waliyokusanyika katika ukumbi wa Cavernous mjini Beijing, na unafanyika huku kukiwa na machafuko ya kijamii na hasira za umma dhidi ya kuongezeka kwa vitendo vya rushwa, na pengo linalozidi kupanuka kati ya walicho nacho na wasiyo nacho.
"Kama tutashindwa kushughulikia suala larushwa vizuri, linaweza kkusababisha kuanguka kwa chama na taifa kwa ujumla. Mageuzi ya mifumo ya kisiasa ya chama ni muhimu kama sehemu ya mageuzi ya ujumla ya China. Laazima tuendelee kufanya juhudi za maksudi kugeuza mfumo wa kisiasa, na kupanua demokrasia kwa vitendo," alisema rais Hu.
habari kwa hisani ya DW

No comments:
Post a Comment