Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, March 27, 2014

Rais Barrack Obama wa Marekani anakutana na na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis.


Rais Barrack Obama wa Marekani anakutana na na kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis, katika makao yake makuu huko Vatican.
Hii ni mara ya kwanza kwa Obama kukutana na papa Francis.
Rais Obama ameelezea furaha yake ya kukutana na papa mtu ambaye kulingana naye anaishi na kutenda kulingana na injili anayoihubiri.
Maswala mbali mbali yenye umuhimu wa kimataifa pamoja na kidini huenda yakajadiliwa katika mkutano huo.
Wawili hao wanatarajiwa kujadili namna ya kupunguza tofauti iliyopo kati yao katika maswala mengi mbali na kujaribu kuinua maisha ya watu maskini duniani.
source Bbc.