Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, November 28, 2013

UKITAKA KUOWA KWA WAZARAMO BASI ZINGATIA HAYA.


Kwanza kwa ufupi kabisa nikufahaishe kuwa Wazaramo ni kabila kutoka eneo baina ya Dar es Salaam na Bagamoyo, nchini Tanzania. Hawa  Wazaramo ni sehemu ya Wabantu. Mababu wanaamini kwamba waliingia katika eneo la Tanzania katika milenia ya kwanza,  inasema ya kwamba walihamia pwani katika mazingira ya Dar es Salaam kutoka Uluguru (Morogoro) katika karne ya 18.
Basi kama ujuavyo Tanzania watu hutoka mkoa mmoja kwenda kuchumbia mkoa mwingine au kabila fulani kwenda kuchumbia kabila jingine ni jambo la kawaida sana ingawa katika makabila hayo wana mila na tamaduni zao ambazo bado kila kabila huamini na kuzifanya wakati wa sherehe misiba au ndoa.
Sasa basi tunapokuja katika swala la ndoa  wewe kijana Ukitaka kuchumbia kwa Wazaramo basi tegemea kukutana na haya .
1.    Yahitajika uwe na Mshenga ambae  wewe muowaji atakuwakilisha, itaandikwa barua ya posa kwenda kwa wazazi wa Mwali ambae unataka kuowa,na barua hiyo itapelekwa na mshenga wako .

 2.  Baada ya barua kupelekwa  inapangwa siku maalum ambapo barua hiyo itasomwa kisha baadae utapewa jibu la NDIO au HAPANA . na kama basi utakuwa umekubalika kwa wakwe zako majibu utakayopewa utaambiwa kwamba Mtoto au huyo Mwali ataolewa kwa mahari ya kiasi Fulani  na mambo yanayo hitajika na nilazima uyatimize.

3.    Utakapo pokea majibu ya kukubaliwa unatakiwa huyo mshenga wako arudishe majibu ya shukurani kwa kukubaliwa pamoja na MAHARI uliyo pangiwa .

4.    KATIKA MAHARI kunakuwa na fedha ulizo ambiwa kama ni m 500 au 1,000 au hata milioni moja ni kile ulichoambiwa utapeleka  . KUNA MKAJA WA BIBI ( hili ni kama kapu la bibi wasemavyo sikuhizi  linakuwa na kila kitu ndani, kanga, nguo mafuta sabuni sukari na hata blanketi la bibi yani kila kitu ambacho bibi anapaswa kutumia)  kisha kuna SAMBUA LA NDEVU  hilo mwenzangu sasa utauliza zaidi lina mambo gani naambiwa hizo ni mbwembwe tu vikolezo vya kufanya mahari ipendeze . Kisha kuna KANYANGA LUBUGA . Kisha ukisha timiza hayo  basi unapanga tarehe ya kufanya ndoa.

5.    Kumbuka katika ndoa pia yasemekana kuwa hufungwa kulingana na nyota ya mhusika ndio maana yaweza fungwa mchana au asubuhi na hata usiku ili basi kuweka tu mikakati mizuri ili ndoa isije vunjika ndio maana pia wanazingatia muda wa kuowa.

6.    Mie nakomea hapo basi kama kula lolote zaidi juu ya wazaramo karibu sana na ruksa kabisa kuniongezea hapo  ili tujuzane mengi ndio maana ya mimi kuzungumza na wewe.
Nimshukuru sana kaka yangu Mbwiga wa Mbwiguke Mzaramo halisi kwa kunidokeza haya basi na mie nikaona vyema tujuzane pamoja.
sikunjema kwako .......