Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, December 2, 2014

CELIN DION AKATISHA ZIARA YAKE KIMUZIKI NA KUREJEA KUANGALIA AFYA YAMUMEWE
 yaonekana kwa sasa mwana mama
Celine atarejea kwenye ulingo wake wa kazi baada ya kuonekana mafanikio mazuri baada ya mumewe kuweza kupata ahueni kutokana na kusumbumbuliwa kwa ugonjwa wa saratani.

ukijaribu kufuatilia baadi ya mitandao yenye kutoa taarifa juu ya  mwanamuziki huyo zinaonyesha kuwa hivi karibuni alisitisha ziara yake ya muziki iliokuwa ifanyike Las Vegas  na ile ya bara la Asia na kuamia kurejea nyumbani kwaajili ya kuwa karibu na mumewe ili kumsidia kupata matibabu na kuwa nae katika wakatu huu.

 Mumewe Celine mwenye umri wa miaka 72 hivi sasa alifanyiwa upasuaji mwezi december ya kuondoa uvumbe wa saratani iliokuwa inamkabili.

Mwanamuziki huyo alinukuliwa  kupitia kituo cha  ABC akisema " nataka kuweka nguvu zanguzote na uwezo wote wakati huu wa kumuuguza mume wangu ni muhimu sana kwangu mimi kutoa mudawangu wote huu kwake , kwa familia yangu, na watoto wangu ." Alisema " nataka pia kuomba samahani kwa mashabiki zangu wote popote walipo kwa kukwaza, lakini pia nawashukuru sana kwa upendo wao wanaonionyesha hasa katika kipindi hiki cha matatizo ya kiafya kwa mume wangu  na mie ambae nimekuwa na matatizo ya koo ambayo yalinifanya nishindwe kufanya show zangu kuanzia mwezi june nasema santeni sana." Alimaliza celin dion.

Sisi tunamtakia kila la heri afya njema kwake na mumewe ili aweze kurejea kwenye kazi yake mapema.