African music is on my blood Back to my root Proud to be Africa,be your self #lets talk about African culture,tourism music ,life style, business,technology, money, fashion, Love, Marriage, Health, food, animals,and so on!!!!
Tunapatikana Sinza kwa Remmy
Sunday, March 15, 2015
TUBURUDIKE NA WIMBO WA LOKUA KANZA AKIWA NA FALLY IPUPA
SHABIKI NAMBA MOJA WA KOFII OLOMIDE MWANAMAMA KISI NDJORA WAKATI ALIPOACHIWA HURU.
Hatimae KISI NDJORA yuu huru baada yakupewa msaada kutoka kwa mawakili wa koffi olomide.
JB MPIANA ndie aliekua wakwanza kumfungulia mashitaka kisi ndjora kwakosa la kumpakazia mambo yasiokua na ukweli wowote, baada ya kutafakari, jb mpiana kupitia mawakili wake, kaiomba mahakama jijini kinshasa imfutie kisi ndjora kesi.
Wakati akiachiwa huru kutokana na kesi ya JB MPIANA, fally ipupa kwaupande wake, kaja pia kumfungulia mashitaka kisi ndjora,kashutumiwa kosa la kumtukana , kumtishia maisha fally ipupa…
Ingawa kisi ndjora anao muonekano wakiume, bali ni mwanamke na anaishi na mwanaume, ana watoto hadi wajukuu!!!
Kwa hisani ya sport na starehe. By Pius
ASANTE KWA MIAKA 10 YA UTUMISHI # AMBULANCE ALIYOITOA MBUNGE ZITTO KABWE MARCH 14 JIMBONI KWAKE.
Mbunge
wa Jimbo la Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe leo March 14 ametoa gari mpya
ya kubebea wagonjwa (Ambulance)kama moja ya ahadi zake alipokuwa kwenye
kampeni ambapo aliahidi kabla ya kumaliza kipindi cha uongozi wake
atatoa gari hiyo.
Wakipokea msaada huo Michael Mwandezi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kigoma pamoja na Hamis Said Betese ambaye naye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambapo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Nyarubanda ambao ndio msaada huo wamemshukuru sana Mbunge Zitto Kabwe.
Hata hivyo kabla ya kuelekea kukabidhi Gari hiyo ya kubebea wagonjwa,Zitto Kabwe aliwatembelea Wanachama wa Chama cha Ushirika Rumaco ambao wanajishughulisha na kilimo cha Kahawa kutoka kijiji cha Matyazo Kigoma Kaskazini.
PICHA NA HABARI KW AHISANI YA MILLARD AYO BLOG.
Wakipokea msaada huo Michael Mwandezi ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Kigoma pamoja na Hamis Said Betese ambaye naye ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kigoma ambapo kwa niaba ya wananchi wa kata ya Nyarubanda ambao ndio msaada huo wamemshukuru sana Mbunge Zitto Kabwe.
Hata hivyo kabla ya kuelekea kukabidhi Gari hiyo ya kubebea wagonjwa,Zitto Kabwe aliwatembelea Wanachama wa Chama cha Ushirika Rumaco ambao wanajishughulisha na kilimo cha Kahawa kutoka kijiji cha Matyazo Kigoma Kaskazini.
PICHA NA HABARI KW AHISANI YA MILLARD AYO BLOG.
Thursday, March 12, 2015
WATOTO, VIJANA, WATU WAZIMA NA HATA WAZEE WAKO HATARINI KUKUMBWA NA TATIZO LA FIGO
Ni wakati wa jioni wanaonekana Vijana zaidi ya Watano
wakisikiliza Redio, mara linasikika tangazo linalohamasisha upimaji wa afya zao,
wote wanapuuza na mmoja wao anabadilisha kabisa stesheni na kutafuta nyingine.
Baada ya wiki kupita mmoja wa Vijana hao ghafla hali ya
mwili wake inaanza kubadilika anahisi uchovu muda wote, na miguu yake kuvimba hivyo
wanalazimika kumkimbiza hospitali.
Kutokana na kutojenga utamaduni wa kupima afya zao, mara
baada ya vipimo anabainika kuwa na tatizo la figo lakini kibaya zaidi Daktari
anawajuza kuwa tatizo la rafiki yao ni kubwa zaidi kutokana na kuchelewa
kubainika.
Hali hiyo ndiyo inayoelezwa kuwakumba Wagonjwa wengi wanapelekwa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi…
Tatizo la figo linaelezwa kuendelea kuwa kubwa nchini ambapo
kwa wiki katika Hospitali hiyo pekee wanapokea wagonjwa kuanzia 8 hadi 10.
Watoto, Vijana, watu wazima na hata Wazee wako hatarini
kukumbwa na tatizo hilo.
Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO),
idadi ya vifo vitokanavyo na magonjwa ya figo nchini imefikia 4533 sawa na
asilimia1.03 ya vifo vyote, wakati
kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa figo kimeripotiwa kuwa asilimia 14 .
TAASISI YA LISHE TANZANIA YASHITUSHWA NA UDUMAVU MKUBWA WA WATOTO SIMIYU
Taasisi ya lishe tanzania
imeshitushwa na asilimia 42 za takwimu
za udumavu kwa watoto
walio chini ya miaka mitano na hivyo ni sababu mojawapo inayochangia baadhi ya
watahiniwa wa darasa la saba kutofanya vizuri katika mtihani wa taifa
mkoani simiyu.
Akitoa elimu ya uhamasishaji ,kwa
wawakilishi wa wakurugenzi wa halmashauri ,maafisa mipango na
waganga wakuu mkoani simiyu , afisa lishe wa mkoa wa iringa ambaye ni
mwezeshaji mshauri kwa viongozi ngazi ya mikoa na halmashauri mwita waibe
amesema kuwa huu ni mkakati wa kitaifa wa utoaji elimu nchi
nzima,ikiwa ni kutekeleza agizo la rais jakaya kikwete ambalo kimsingi alitoa
agizo kuwa ,viongozi wote wapewe elimu ya lishe ili kuwajengea uelewa wa namna
ya kusukuma masuala ya lishe ambayo yanaliathiri taifa ambapo kati
ya watu ,100,42 wamedumaa.
Katika mjadala huo wa lishe mganga
mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa bariadi dr godfrey MPANGALE
akazitupia lawama mamlaka ya chakula na dawa TFDA NA shirika la viwango
Tanzania tbs kwa kushindwa kudhibiti bidhaa ambazo hazina na ubora na kuleta
madhara kwa watumiaji bidhaa hizo.
Naye katibu tawala wa mkoa wa simiyu
mwamvua jirumbi amewataka watendaji kuwajibikaji kwa kila mmoja kwa nafasi yake
ili kuweza kulitokomeza tatizo la udumavu lililofikia asilimia 42 .
Subscribe to:
Posts (Atom)