Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, March 12, 2015

TAASISI YA LISHE TANZANIA YASHITUSHWA NA UDUMAVU MKUBWA WA WATOTO SIMIYUTaasisi ya lishe tanzania imeshitushwa  na asilimia 42 za  takwimu
za udumavu  kwa watoto walio chini ya miaka mitano na hivyo ni sababu mojawapo inayochangia baadhi ya watahiniwa wa darasa la saba kutofanya vizuri katika  mtihani wa taifa mkoani simiyu.  

Akitoa elimu ya uhamasishaji ,kwa wawakilishi wa wakurugenzi wa halmashauri   ,maafisa mipango na waganga wakuu mkoani simiyu , afisa lishe wa mkoa wa iringa ambaye ni mwezeshaji mshauri kwa viongozi ngazi ya mikoa  na halmashauri mwita waibe amesema kuwa huu ni   mkakati wa kitaifa wa utoaji  elimu nchi nzima,ikiwa ni kutekeleza agizo la rais jakaya kikwete ambalo kimsingi alitoa agizo kuwa ,viongozi wote wapewe elimu ya lishe ili kuwajengea uelewa wa namna ya kusukuma masuala ya lishe ambayo yanaliathiri taifa ambapo   kati ya watu ,100,42 wamedumaa.

Katika mjadala huo wa lishe mganga mfawidhi wa hospitali ya halmashauri ya mji wa bariadi dr godfrey MPANGALE akazitupia lawama mamlaka ya chakula na dawa TFDA NA shirika la viwango Tanzania tbs kwa kushindwa kudhibiti bidhaa ambazo hazina na ubora na kuleta madhara kwa watumiaji bidhaa hizo.

Naye katibu tawala wa mkoa wa simiyu mwamvua jirumbi amewataka watendaji kuwajibikaji kwa kila mmoja kwa nafasi yake ili kuweza kulitokomeza tatizo la udumavu lililofikia asilimia 42 .