Ni wakati wa jioni wanaonekana Vijana zaidi ya Watano
wakisikiliza Redio, mara linasikika tangazo linalohamasisha upimaji wa afya zao,
wote wanapuuza na mmoja wao anabadilisha kabisa stesheni na kutafuta nyingine.
Baada ya wiki kupita mmoja wa Vijana hao ghafla hali ya
mwili wake inaanza kubadilika anahisi uchovu muda wote, na miguu yake kuvimba hivyo
wanalazimika kumkimbiza hospitali.
Kutokana na kutojenga utamaduni wa kupima afya zao, mara
baada ya vipimo anabainika kuwa na tatizo la figo lakini kibaya zaidi Daktari
anawajuza kuwa tatizo la rafiki yao ni kubwa zaidi kutokana na kuchelewa
kubainika.
Hali hiyo ndiyo inayoelezwa kuwakumba Wagonjwa wengi wanapelekwa
katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbi…
Tatizo la figo linaelezwa kuendelea kuwa kubwa nchini ambapo
kwa wiki katika Hospitali hiyo pekee wanapokea wagonjwa kuanzia 8 hadi 10.
Watoto, Vijana, watu wazima na hata Wazee wako hatarini
kukumbwa na tatizo hilo.
Kulingana na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO),
idadi ya vifo vitokanavyo na magonjwa ya figo nchini imefikia 4533 sawa na
asilimia1.03 ya vifo vyote, wakati
kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa figo kimeripotiwa kuwa asilimia 14 .
No comments:
Post a Comment