Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Thursday, June 27, 2013

ATI WAJAMENI JE UMRI NI KIGEZO? UNANAFASI GANI UMRI KATIKA RELATIONSHIP. MSAIDIENI DADA GETRUDA

Habari za leo dada Sofia?? kwa kweli jana nilipopita katika blog yako nilifurahishwa sana na topic ambazo kwa jana uliweka ili tuweze kuchangamsha akili na kusaidiana walau kupeana ufahamu wa hayo machache tulio nayo mie nina maswali kwako na kwa wadau wa blog hii yetu tena naomba nikupe jina Anti sophie nakumbuka sana jina hilo ulikuwa ulilitumia wakati tulipokuwa wadogo katika kipindi cha watoto huko Terrat Simanjiro kwakweli dada nisiseme mengi nakufaamu kwa uzuri tu na nafurahiswa na kazi zako .

Sasa basi langu lengo hapa ni kukuuliza wewe na wadau wa blog yetu kama nilivyo bainisha hapo awali kuwa Ati UMRI NI KIGEZO au UMRI UNANAFASI GANI KATIKA MAHUSIANO??. mie nimetokea kupendwa na kijana mmoja jina kapuni lakini kulingana na umri wangu mie na miaka 35 yeye ana miaka 28 naogopa mmno  ingawa kijana huyo na mpenda sana, ila hofu yangu ni ndugu na marafiki pengine wataniona kama nambemenda kijana wa watu, kwa kweli najitahidi sana kumkwepa ila naona kama naidhukumu nafsi yangu mie naomba ushauri wenu marafiki pamoja na dada Sofia je nifanyeje kwasababu nampenda mmno ila nahofia umri nisaidieni.. je umri unanafasi gani katika mahusiano je nimwache tu kwasababu mdogo kuliko mie au nifanyaje naidhulumu nafsi yangu jamani.

wenu rafiki Gatruda Nipo Arusha kaloleni.

HAYA MARAFIKI HIYO NI BARUA PEPE YA MDOGO WETU GETRUDA TUNAMSAIDIAJE HEBU TUZUNGUMZE KATIKA KURASA YETU HII PENGINE ATAPATA MUAFAKA WA KILE ANACHOFIKIRIA WENU ANTI SOPHIE

No comments:

Post a Comment