Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, June 28, 2013

ANANIPIGA SANA ILA NAMPENDA NAOGOPA KUMUACHA NIFANYEJE MWILI WOTE UNA MAJERAHA YA VIPISI VYA SIGARA

Ama kweli dunia ina mambo,unaambiwa tembea ujionyee yanayojiri duniani kweli MOYO UKIPENDA MACHO HAYAONI.Jana nilibahatika kwenda kutembelea maeneo Fulani hivi pande za mbezi, wakati nikiwa huko nikakutana na ma binti wawili wamekaa wanajipatia vilaji, mmoja wao alikuwa mwenye huzuni sana  bahati nzuri nawafahamu wakati naingia eneo la tukio mmoja wapo akaanza kunipa story, si unajua tena mambo ya wanawake tukikaa basi hatuishi kuteta hili mara lile, katika zungumza mwenzetu huyo akaanza kutusimulia jinsi anavyopata kipigo toka kwa mpenzi wake ambae kwa sasa wanamiaka 5 ya mahusiano, anakuambia tangu ameanza mahusiano jama ayake anawivu sana yani akimpigia simu dakika mbili isipopokelewa ni kosa akikutana nae ni kichapo. Akitoka hata kwenda sokoni asipomuarifu basi kichapo bidada ana makovu ile mbaya ya kipigo, si kwao wala si kwa marafiki wamemkataza na kumwambia hayo si mapenzi jamaa pengine hana nia nae njema atamtoa roho.

wiki chache zilizopita alienda kwenye kitchen part ya rafiki yake bahati mbaya hakuwa na usafiri hivyo alitegemea usafiri wa mashosti awahi kurudi home kwakwe, kwa bahati mbaya yule shoti mwenye gari akachelewa kurudi akarudi home kwenye saa 7 usiku, kumbe jamaa yake alishafika home tangu saa nne  na kumgoja bila kumuona, na unajua tena mambo ya mitandao simu ikawa kwa bahati mbaya haipatikani lol, wanasema siku ya kufa nyani miti yote huteleza .


Basi bwana bidada aliporudi home kesho yake  jama ayake akamuita eneo la kin'gori Arusha , binti hakuwa na hili wala lile wamekaa zao bar wanakula na kunywa mara jamaa akaanza kumhoji ilikuwaje ukachelewa binti wa watu akajielezea wee lakini wapi, unaambiwa bila haya jamaa akanyanyuka pale pale na kuanza kumpa kichapo mbele za watu tena bar .


Piga binti kisawa sawa mpaka akawa hoi ndio ikabidi watu waliokuwa bar wamuokoe jamaa kwa sifa akawa anasema TENA NAKUPIGA KISAWA SAWA NA KUKUACHA SIKUACHI. na ukitaka kashitaki popote sasa binti ndio ndugu zake kumuona na majeraha wakamtorosha na kumleta dar, binti anasema anampenda mpenzie na anataka kurudi kuleeee alilokuwa napata kichapo mmh ukimuangalia mwili mzima makovu ya hatari.


Nikajiuliza jamani Mapenzi gani haya loh ... JE UMEWAHI KUYAONA AU MWENZETU ANA TATIZO AU NDO MAPENZI YAMEKOLEA DUH .

TUZUNGUMZE JAMANI