Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, June 24, 2013

"NAOMBA MSAADA KWA RAISI WANGU WA NCHI, IGP SAID MWEMA, WANAWAKE WENZANGU NA WATANZANIA WOTE KWA UJUMLA". JOYCE KIRIA

 

NAOMBA MSAADA KWA RAISI, IGP MWEMA NA WANANCHI WOTE NIPATE HAKI ZANGU NIKIWA KAMA MAMA NA MKE KUFAHAMU KUJUA MUME WANGU ALIPO.



Baada ya kukaa kwa siku mbili bila kujua alipo mume wangu, nimejitokeza mbele ya waandishi wa habari wapate kunisaidia kufikisha ujumbe wangu wa kupata msaada ya kujua mume wangu alipo.


Hapa ni karibu kabisa ya ukumbi wa habari maelezo ambapo niliwafuata waandishi wa habari ili kupata muda wa kuongea nao, nikiwa nimewabeba wanangu Lincon na Linston.


Nina watoto wawili mkubwa ni wa miaka 2 na mdogo wake ni wa miezi 4, leo ni siku ya nne hawajamuona baba yao, baba yao ni msaada mkubwa mno kwa familia yangu, Raisi Kikwete huko ulipo nakuomba usikie kilio changu, IGP Said Mwema nahitaji msaada wako, Wanawake na Wote nahitaji msaada wenu.


Hapa nikiendelea kuelezea hali halisi ya jambo hili mpaka leo hii kuja hapa, na kubwa ni kutopewa taarifa ya mume wangu alipo. Sina Amani kabisa naomba kupata taarifa kamili huko aliko yuko salama? na hata kufahamu anakula nini?


Kubwa watanzania wenzangu ni kunisaidia katika maombi ili huko aliko awe salama.

Kwa Urefu zaid habari hii itaruka katika vyombo mbalimbali vya habari zikiwepo TV kama Channel Ten, ITV, EATV, Star TV na Clouds, Radio kama Clouds, Radio One, na magazeti kama Mwananchi, Nipashe , Mtanzania, Tanzania Daima , The Citizen, Guardian, na vyombo vingine vya habari.

Nawashukuru waandishi wote ambao walikuwepo hapa, pia na watanzania wote naamini mko pamoja na mimi. .
 
HABARI HII NI KWA HISANI YA JOYCE KIRIA WANAWAKE LIVE.

1 comment:

  1. Mh! kuna maelezo mengi hayajakamilika. Huyo Mumeo ni Nani? Mnaishi wapi? Anafanya kazi gani? Alitoka akaaga anaenda wapi? Umewasiliana na ndugu na rafiki zake wanasemaje? KUBWA KULIKO YOTE UMEWEKA PICHA YAKO BADALA YA PICHA YA MUMEO, AU KIKWETE AKIONA SURA YAKO TU ATAMJUA HUYO MUMEO?...AU LABDA NI STORI TU!

    ReplyDelete