Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, January 28, 2015

WANAFUNZI ZAIDI YA 200 WATUMIA DARASA MOJA WENGINE WASOMA CHINI YA MITI ILIYOKO KARIBU NA SHULE HIYO.



Hali ya Shule ya msingi SAKU iliyoko Manispaa ya Temeke Jijini Dar es salaam si ya kuridhisha baada ya kukabiliwa na uhaba wa miundombinu na kusababisha zaidi ya Wanafunzi 200 kusoma ndani ya chumba kimoja.

Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Mkondongwa NASORO RASHID anasema shule hiyo kwa sasa haina madawati ya kutosha, madarasa  hali inayosababisha wanafunzi wengi kusomea chini ya miti na wengine kujazana katika darasa moja.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo alipotakiwa kutoa ufafanuzi wa suala hilo hakuwa tayari kutoa ushirikiano kwa madai kuwa yeye si msemaji huku akifanya juhudi za kuwazuia waandishi wa Clouds kufuatilia tukio hilo.

Kitendo cha Mwalimu Mkuu kujaribu kuzuia Waandishi wa kituo hiki kufuatilia matatizo ya Shule hiyo kinamshangaza Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo ambae anasema kuwa haoni sababu ya Mwalimu kuchukua hatua hiyo wakati shule hiyo ikiwa na miundombinu ambayo hairidhishi.

Baadhi ya wazazi wameiambia Clouds fm kwamba matatizo yanayoikabili shule hiyo yanachangiwa pia na uongozi mbovu wa mwalimu mkuu huyo ambae hana ushirikiano na wazazi.

Swali la kujiuliza ni kwamba kama shule iliyoko jiji la Dar es salam inakuwa na wanafunzi wanaosomea chini kwenye sakafu na wengine kusoma chini ya miti, Je kwa shule za vijijini zitakuwa katika hali gani, ni vyema serikali ikalitazama hili kwa jicho la tatu.

No comments:

Post a Comment