Tukio hili naweza sema hufanyika Mara moja tu kwa mwaka ambapo wana familia wengi tunakutana kujumuika na kufanya mambo mbali mbali ya kifamili kwa kuwa kwa mwaka mzima huwa tunakuwa katika mikoa mbali mbali wenzetu wa mjini hutania wachaga wakidai kuwa tumeenda kuhesabiwa, Sensa ya kufunga mwaka ha ha ha ha Basi na mie mwaka huu nikajichangana na wachaga wenzangu haya ndio nilioyaona na kujikumbusha mengi ambayo niliyakosa kwa muda mrefu jumuika nami
Marangu moja hiyoo Gree Land
kichumi kina kuwa kisafiii, kwa wachaga wanelewa nikisema kichumi namaanisha ni kale kanjia ka kuingilia Nyumbani ni utamaduni kwa wachaga wengi huwa hawakosi kanjia hako hicho ndio kichumi na nilazima kifagiliwe kila siku saa 12 alfajiri inapendeza sana
unapofika kijijini kwa wachaga wa marangu basi utapokelewa na kitochi ( mbege ) ni pombe ya asili ambayo hupikwa kwa ndizi mbivu na ulezi nili enjoy sana maana ni muda mrefu sikuwa nimeipata
Marangau kuna vivutio vingi sana kuanzia mazingira tu kwa usafi na mengine mengi
Maji ya chemichemi ambayo ni masafi kuliko kawaida
wazee wa familia wanapokutana kujadili mambo
straw Bell mjini huuzwa bei mbaya sana ila kwetumarangu zimejaa kibao wenyewe wanita MAWERO bureee wala hununui.
bro akiwa kapozi na yeye kwenye jumba lake la la joto ha ha ha ha
mauwa mazuri ambayo ukija mjini utauziwa kwa bei ya gali kule yapo yamejiotea tu na unapochuma hata wenyeji hukushangaa kuwa unapeleka wapi yapo tuuuu.
majimbi na mboga aina ya salad mboga mboga hiyo ndogoo iliyo tambaa kwenye Maji ya majani ambayo huota katika maji marangu zipo kibao hizo
PICHA ZAIDI ZINAKUJA NA MATUKIO MEEENGI
haika sana monookika...nongikumbura mndenyi naiyo ngilenyo wari mrasa ngawarima na kanyi mleu
ReplyDeleteeh nimefurahi sana kuona home na kujifunza Mengi sophia endelea kutupa uhondo tuko pamoja i love what ur doing mamaaaa
ReplyDeletenimeipenda ma dear Sophy, hata mie nilikuwa uchagani pia
ReplyDelete