Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, amesema mipango inaandaliwa kuhakikisha akina baba wanapatia likizo ya uzazi, pindipo wake zao wanapojifungua.
Waziri huyo alisema msingi wa hatua hiyo utasaidia ulezi wa wazazi wawili baina ya mama na baba mara tu wanapojaaliwa kupata mtoto.
Mzee alieza hayo ofisini kwake alipokuwa akitoa taarifa ya Serikali ikiwa ni maadhimisho ya siku watu duniani. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Fedha na Mipango ya Maendeleo, Omar Yussuf Mzee, amesema mipango inaandaliwa kuhakikisha akina baba wanapatia likizo ya uzazi, pindipo wake zao wanapojifungua.
Waziri huyo alisema msingi wa hatua hiyo utasaidia ulezi wa wazazi wawili baina ya mama na baba mara tu wanapojaaliwa kupata mtoto.
Mzee alieza hayo ofisini kwake alipokuwa akitoa taarifa ya Serikali ikiwa ni maadhimisho ya siku watu duniani.
Kwa miaka kadhaa hivi sasa wafanyakazi wa kike katika Serikali ya Zanzibar wamekuwa wakifaidika na mpango wa likizo ya uzazi kwa kupata mapumziko ya kipindi cha mienzi mitatu mara tu wanapojifungua na kupewa muda wa saa nzima ya kwenda kumpatia mtoto maziwa ya mama.
Alisema katika kuimarisha huduma za uzazi wa mpango na malezi kwa watoto wataozaliwa na watumishi wa umma, Serikali inakusudia kuchukua hatua ya kuwapa likizo ya uzazi wanaume ili kumsaidia mama ulezi kwa mtoto aliyezaliwa.
Alisema hivi sasa utaratibu wa likizo ya uzazi upo kwa upande mmoja tu ambao wamekuwa akipewa mwanamke, lakini hata hivyo bado haujaweza kuleta tija kutokana na wanaume kujiona kama sio sehemu ya kuisaidia familia katika kipindi hicho. Kutokana na hali hiyo, Waziri huyo alisema Wizara hiyo kwa kushirikiana na Wizara ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar, tayari imeanza kuandaa kanuni ili akina baba nao wapatiwe likizo (siku tano za kazi) la uzazi ili kumsaidia mama na mtoto aliezaliwa.
“Hatua hii itasaidia kuondokana na ile dhana kwamba suala la afya ya uzazi linamhusu mama pekee. Llakini hatua hii inategemewa iwe chachu ya kuwashirikisha akina baba katika harakati zote za huduma ya afya ya uzazi na mtoto”, alisema Waziri huyo.