Kwa mara ya kwanza kifaa cha kujipima iwapo mtu ana virusi vinavyosababisha ukimwi kimeidhinishwa na wataalam wanaodhibiti sekta ya Afya nchini Marekani.
Kifaa hicho ambacho kitawezesha mtu kuchunguza hali yake mwenyewe nyumbani au kokote anakotaka kitaanza kuuzwa nchini Marekani mwezi Oktoba mwaka huu.
Serikali ya Marekani inatarajia kuwa kifaa hicho kitasaidia kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kwa kubadili tabia miongoni mwa watu wanaoishi na virusi bila kujua.
Inakadiriwa kuwa robo millioni ya Wamarekani wako katika kitengo hicho.
Utafiti wa kimatibabu unaoyesha kuwa majaribio ya matokeo ya uchunguzi wa kifaa hicho cha Oraquick yananaweza kuwa sahihi kwa asilimia tisini na mbili, miongoni mwa watu wanoishi na virusi vya ukimwi.
CHANZO CHA HABARI HIZI NI BBC
No comments:
Post a Comment