Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, February 15, 2013

Mahakama ya juu kuamua kuhusu Kenyatta na Ruto



Mahakama kuu nchini Kenya imeeleza kwamba haiwezi kuamua iwapo Uhuru Kenyatta na William Ruto wanapaswa kugombea nyadhifa katika uchaguzi mkuu ujao.
Mahakama hiyo imeeleza kwamba ni mahakama ya juu nchini pamoja na tume huru ya mipaka na uchaguzi Kenya ndiyo zilizo katika nafasi ya kufikia uamuzi kuhusu hilo.

Ikiwa zimesalia wiki mbili tu kwa uchaguzi mkuu kufanyika Kenya, inaonekana kuwa wananchi ndiyo watakaoamua kupitia kura, iwapo Uhuru Kenyatta na William Ruto wanafaa au hawafai kuwa viongozi nchini.
Uhuru Kenyatta anawania urais katika uchaguzi mkuu unaowadia katika muda wa wiki mbili zijazo na naibu wake ni William Ruto.
Kesi hiyo iliwasilishwa na mashirika yasiyo ya serikali yaliyotaka kubainishiwa iwapo viongozi hao wawili wa muungano wa kisiasa, Jubilee, wana uwezo wa kuhudumu katika ofisi ya serikali wakati wanatuhumiwa kwa kesi za uhalifu.
Hali ambayo mashirika hayo yanaona ni kwenda kinyume na katiba ya nchi.

CHANZO CHA HABARI HII NI BBC SWAHILI .

No comments:

Post a Comment