Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Monday, February 25, 2013

MENO 18 YA TEMBO YAKAMATWA MOROGORO

Vipande 18 vya meno ya tembo vyenye thamani ya shilingi milioni ishirini na tisa laki saba sabini na sita elfu  vimekamatwa kwa ushirikiano wa jeshi la polisi mkoani Morogoro na hifadhi ya Udzungwa baada ya kupata taarifa kutoka kwa raia mwema huku wahusika waliokuwa wakisafirisha nyara hizo kutelekeza gari vilivyokuwamo vipande hivyo
            (picha kutoka maktaba)
Akizungumza na Clouds Fm kamanda wa jeshi la polisi mkoani Morogoro Faustine Shilogile amesema kuwa tukio hilo lilitokea  februari 23 mwaka huu majira ya saa saaa 11:00 jioni katika eneo la  la Mto Mwaya Mang’ula wilayani Kilombero ambapo askari polisi walipata taarifa ya kuwepo gari lenye namba T 557 AYR aina ya Toyota mark II yenye rangi ya kijivu ikiwa na watu wawili ndani iliposimamishwa watu hao walishuka kwenye gari na kukimbilia porini huku wakilitelekeza  gari hilo ambalo ndani yalikuwamo meno hayo.



Naye mhifadhi mkuu wa hifadhi ya Udzungwa Vitalis Uruka amesema kuwa vipande hivyo vya meno ya tembo vinadaiwa kupatikana maeneo ya Ifakara au Mahenge na  ni tukio la muda mrefu na kwamba wwatatumia gari hilo lililotelekezwa na watu hao kuwapata wahusika

No comments:

Post a Comment