Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, February 15, 2013

Oscar Pistorius afikishwa mahakamani


Nyumba ya mwanariadha huyo iliyo katika eneo la kifahari mjini Pretoria.

Mwanariadha mlemavu wa Afrika Kusini na nyota wa Olimpiki,Oscar Pistorius, amefikishwa mahakamani akikabiliwa kwa madai ya kumuua mchumba wake baada ya kupigwa risasi akiwa nyumbani kwa Pistorius mjini Pretoria.
Pistorius alikesha katika kituo cha polisi na uamuzi utaafikiwa ikiwa ataruhisiwa kupewa dhamana.
Wendesha mashtaka wanataka Pistorius aendelee kuzuiliwa na polisi.
Mwandishi wa BBC Andrew Harding,mjini Pretoria, anasema kuwa maelezo fulani, ya kesi hiyo dhidi ya Pistorius mwenye umri wa miaka 26 na upande wa utetezi yatatolewa baadaye leo.

Anasifika kama mkimbiaji wa vyuma, namaradhikatika miguu yake yalisababisha miguu yake kukatwa kabla ya kufikisha mwaka mmoja.
Wataalamu wa uchunguzi, wanatarajiwa kuendelea na uchunguzi wao katika nyumba ya Pistorius ambako mchumba wake Steenkamp, aliuawa.
Duru zinasema kukamatwa kwa Pistorous kumewashangaza wengi sana Afrika Kusini ambako anatazamiwa kama shujaa.
Pistorius alikuwa mkimbiaji wa kwanza mlemavu kuruhusiwa na shirika la kimataifa la riadha kuweza kushindana na wanaridha wengine wasio na ulemavu wowote.
Awali duru zilisema kuwa Pistorius huenda alimuua Reeva Steenkamp kimakosa kwa kudhania kuwa ni mwizi aliyekuwa amemvamia, ingawa polisi walipuuza madai hayo.
Polisi walisema kuwa kumekuwa na visa kadhaa vilivyoriptiwa kutokea nyumbani kwa Pistorius na kutajwa kuwa ugomvi wa kinyumbani.
Pistorius anasifika kama mwanaridha wa kwanza mlemavu kushiriki michezo ya Olimpiki. Habari za mauaji ya mpenzi wake Pistorius zimewashangaza wengi Afrika Kusini kwani anasifika kama mwanaridha anayeiletea nchi hiyo sifa.

Afrika Kusini ni moja ya nchi zenye visa vingi vya uhalifu duniani na watu wengi wanamiliki silaha za kujilinda.

CHANZO CHA HABARI BBC SWAHILI NEWS.

No comments:

Post a Comment