Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, February 20, 2013

IDHAA YA KISWAHILI YA DW YATIMIZA MIAKA 50 TANGU KUANZISHWA KWAKE.


Idhaa ya Kiswahili ya Deutsche Welle leo inaadhimisha miaka 50 tangu ilipoanzishwa na kuanza kurusha matangazo yake  tarehe 1 Februari 1963 na kusikika katika maeneo ya Afrika Mashariki na Kati.


 (Nikiwa pamoja na Adrea Schmidt ambae ni mkuu wa idhaa ya kiswahili wa Radio (DW) Deutshche Welle mara baada ya mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo 20/2/2013 katika ukumbi wa umoja house hapa jijini Dar es saalam. )

Deutsche Welle inaadhimisha miaka 50 ya idhaa yake ya Kiswahili
chini ya maudhui ya “Maarifa na Mwamko“ katika hafla maalumu itakayofanyika jijini Dar es Salaam.
Kwa nusu karne, Deutsche Welle (DW) imekuwa ikitangaza taarifa na habari
za uhakika kwa lugha ya Kiswahili kwa ajili ya wasikilizaji kwenye maeneo ya
Mashariki mwa Afrika na eneo la Maziwa Makuu.

Tarehe 22 Februari, saa 9.oo mchana katika jengo la Makumbusho ya Taifa, DW itasherehekea
maadhimisho haya kwa hafla maalumu jijini Dar es Salaam, Tanzania, ikiwaleta
pamoja wachambuzi wanaoheshimika katika mjadala wenye maudhui ya
“ Maarifa na Mwamko kupitia Vyombo vya Habari“.




Hotuba maalumu zitatolewa kwa lugha ya Kiingereza na Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Klaus-Peter Brandes, na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya DW, Andrea Schmidt.

“Idadi kubwa ya wasikilizaji wanaoishi hapa Tanzania, kwa hivyo lilikuwa chaguo la uhakika kwa ajili ya sherehe zetu,“ alisema Andrea
Schmidt. “Kwa miaka 50 iliyopita, DW imejitolea katika utoaji wa habari
zenye uwiano na taarifa za uhakika, ikiwapa watu wa Afrika ya Mashariki
habari na uchambuzi wa kina juu ya masuala yenye uzito mkubwa.“

Uchambuzi utafanywa na jopo la majadiliano lililotayarishwa kwa msaada
wa Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) ofisi ya Dar es Salaam na
utafanywa kwa lugha ya Kiswahili. Mohammed Khelef wa DW ataongoza
majadiliano hayo akiwa na wataalamu wa vyombo vya habari wanaoheshimika
nchini Tanzania, akiwemo Assah Andrew Mwambene (Mkurugenzi

waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali tulijumuika nao pamoja  
 nikifuatilia kwa umakini kabisa mkutano huo







No comments:

Post a Comment