Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, October 14, 2015

KUMBUKUMBU YA KIFO CHA LUAMBO MAKIADI NA KUZINDULIWA KWA MNARA WAKE.

Aliyekuwa mwanamuziki wa rumba, Luambo luanzo Makiadi amejengewa mnara mkubwa mjini Kinshasa ambako waziri mkuu aliuzindua jana usiku wakati wa maadhimisho ya miaka 26 ya kumbukumbu ya kifo chake.


Mnara huo wa picha yake umejengwa kwenye eneo la wasanii, la PLace de la Victoire/Matonge katika mji mkuu wa Congo. 

Luambo ambaye jina lake kamili ni Francois Luambo Luanzo Makiadi, aliyezaliwa mwaka 1938 na kufariki dunia Oktoba 12 mwaka 1989 akiwa na umri wa miaka 51, alikuwa mtunzi, mpigaji gitaa na mwimbaji ambaye kundi lake la OK Jazz ligeuka kuwa bendi maarufu ba




rani Afrika na duniani kote.
 
 Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo imeahidi pia kuwajengea minara ya kumbukumbu wanamuziki wengine watatu, Joseph Kabasele," Grand Kalle,Tabu Ley Rochereau na Lutumba Simaro.

No comments:

Post a Comment