Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, January 6, 2012

Charles Baba aihama African Stars (Twanga pepeta)

Msanii wa Muziki wa Dansi nchini,Charles Gabriel a.k.a Charles Baba akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar es Salaam leo wakati akizungumzia nia yake wa kujitoa rasmi katika Bendi yake ya awali ya African Stars (Twanga Pepeta) kwenye mgahawa wa Hadee's uliopo katikati ya Jiji.Charles Baba pamoja na kutangaza nia yake hiyo,pia amemtangaza Meneja wake Mpya,Bw. Bernard Msekwa ambaye atasimamia shughuli zake zote za Kimuziki ikiwa ni pamoja na kuingia mikatana na Bendi yeyote itakayomuhitaji.
Meneja Mpya wa Msanii wa Muziki wa Dansi nchini,Charles Baba ,Bw. Bernard Msekwa akisisitiza Jambo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusiana na msanii wake huyo leo kwenye mgahawa wa Hadd's uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam leo.
MWIMBAJI wa kutumainiwa wa bendi ya muziki wa dansi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’ Charles Gabriel ‘Chaz Baba’ ametangaza kujitoa katika bendi hiyo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, msanii huyo alisema kujitoa kwake kumetokana na mambo mengi mojawapo ni kutokuwa na mkataba wa kazi.
Alisema tangu ajiunge na bendi hiyo mwaka 2005 hajawahi kupewa mkataba wowote wa kazi zaidi ya kulipwa mshahara tu kitu ambacho amekiona kama ni kinyume na utaratibu wa kazi.
Chaz aliongeza kuwa baada ya kujitoa ndani ya bendi hiyo kwa sasa atakuwa akisimamiwa na meneja wake aliyemtaja kwa jina la Benard Msekwa.
“Kwa sasa nitakuwa nasimamiwa na meneja wangu mpa (Msekwa) hivyo kila kitu kuhusiana na masuala yangu ya kisanii kitakuwa chini yake, kama ni onyesho ama kuhamia bendi nyingine yote ni juu yake,”Alisema.
Aidha, nyota huyo aliongeza kuwa baada ya kujitoa Twanga Pepeta huku akisubiri mambo mengine, ataelekeza nguvu zake katika kuandaa albamu yake binafsi itakayoundwa na nyimbo nane.
“Mpaka sasa nimeshakamilisha vibao kama sita hivi hivyo katika miezi ya karibuni nadhani itakamilika, nyimbo hizo ni pamoja na Nusu Chizi niliowashirikisha Mapacha Watatu, Blandina, Papa Fred, Mayasa na Ninaelekea wapi,”Alisema.
Naye meneja wa msanii huyo, Msekwa alisema kuwa wamekamisha taratibu zinazostahili juu ya kumng’oa Baba Twanga Pepeta ikiwemo kulipa mshahara wa mwezi mmoja.
Kuondoka kwa Charlz Baba kumethibitisha taarifa za kutaka kujiengua kwake, hivyo kufanya bendi hiyo kuendelea kuwa na pengo kutokana na wasanii kadhaa kuondoka katika siku za hivi karibuni.
HABARI NA PICHA KWA HISANI YA JOHN BUBUKU WA FULL SHANGWE BLOG
THANK YOU SO MUCH KAKA KWA HABARI HIZO.