Mfululizo wa vipindi vifupi vya televisheni kuhusu maisha ya Nelson Mandela viko njiani kutayarishwa huku kati ya waandaaji yuko mjukuu wa Rais huyo wa zamani.
Waandishi walio katika mradi huo ni pamoja na Nigel Williams, aliyeandika vipindi vya Helen Mirren mwaka 2005, Elizabeth I.
Mjukuu wake Kweku Mandela alisema mwitikio wa babu yake alipoelezwa kuhusu mpango huo ulikuwa: "Nitalipwa kiasi gani?"
Upigaji picha utaanza Afrika Kusini baadaye mwaka huu.


Vitabu viwili vya Nelson Mandela vitatumika kama vyanzo vikuu vya taarifa – chenye rekodi binafsi cha ‘Conversations With Myself’ na kile chenye nukuu ya matamshi yake ‘Nelson Mandela By Himself.’
Kazi hii imepewa jina la Madiba, jina la ukoo la Mandela ambalo linafahamika Afrika Kusini.
Kweku Mandela alisema mfululizo huo hautampamba babu yake kama ‘Mtakatifu Mandela’ lakini utatafuta ‘kumwonyesha Mandela kama mtu.’

Itafuatiwa na maisha yake kama kiongozi wa zamani kuanzia mwanzo,uhusiano wake na mama yake, kujihusisha kwake na siasa, maisha yake jela na hatimaye kuchaguliwa kwake kama Rais wa Afrika Kusini.
Mradi huu umetayarishwa kwa pamoja na kampuni tatu duniani -Left Bank Pictures ya Uingereza, Blue Ice Films ya Canada Out of Africa Entertainment ya Afrika Kusini.

Left Bank Pictures ndio kampuni iliyotengeneza filamu kama tamthilia ya mpira wa miguu ya The Damned United, kazi nyingine za televisheni zikiwa ni pamoja na Wallander, nyota wake akiwa Kenneth Branagh.
Nyota wa kuigiza kama Mandela katika mfululizo wa vipindi hivi vifupi vya maisha ya Mandela hajatangazwa bado.