Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tuesday, January 10, 2012

CHARLES BABA KUIBUKIA WAPI IJUMAA?, NENDA KASHUHUDIE BUSNESS CENTER KIJITONYAMA


Mratibu wa onyesho la bendi tatu litakaloshirikisha bendi za Mapacha Watatu, Mashujaa na Extra Bongo Bw. King Dodoo, akiongea na waandishi wa habari kwenye mgahawa wa Busness Kijitonyama leo, wakati mwanamuziki wa bendi ya Mapacha watatu Khalid Chokoraa alipotangaza onyesho maalum la pamoja la bendi hizo, kumtafuta na kumuibua mmjoa wa mapacha wanne Charles Baba ambaye hajulikani alikokimuziki kwa sasa, Charles Baba ameshiriki kuimba wimbo wa KUACHWA ulioshirikisha wanamuziki Khalidi Chokoraa Mwenyewe, Kalala Junior, Jose Mara na Charles Baba, ambaye kwa sasa ametangaza kujiweka kando kutoka bendi ya African Stars. Onyesho hilo litafanyika hapohapo Busness Center Kijitonyama siku ya ijumaa wiki hii na kiingilio kitakuwa shilingi elfu 7.000 kwa kila mtu mashabiki wa muziki wanakaribishwa kuja kuona mwanamuziki Charles Baba anaibukia wapi siku hiyo.
Mwanamuziki Khalid Chokoraa wa Mapacha watatu akizungumza katika mkutano huo wakati akielezea historia ya pacha mwenzao Charles Baba, kulia ni Rogat Hega wa Extra Bongo na katikati ni King Dodoo mratibu wa onyesho hilo.
Kutoka kulia ni Mulomba Shilumba wa Mashujaa Band, Kajo Lisungu- Dasia wa Mashujaa band na Rogat Hega kutoka Extra Bongo.
 
SHUKURANI ZA KIPEKEE KWA MZEE MWENYEWE WA FULL SHANGWE MH : BUKUKU