Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Wednesday, August 22, 2012

ANATAFUTWA AMEPOTEA MSAADA JAMANI ATAKAE MUONA.





CYNTHIA KIMASHA Mkazi wa kijichi Jijini Dar es Salaam, amepotelewa na kaka yake anayefahamika kwa jina la ERICK KIMASHA anayesumbuliwa na maradhi ya akili ametokea Kilimanjaro na mara ya mwisho aliondoka nyumbani akiwa amevaa tracksuit ya brown na T-shirt la njano.

ERICK KIMASHA,  anaumri wa miaka 28, kwa muonekano ni mrefu Mweusi na nimwembamba, Erick alikuja jijini Dar es salaam kwa ajili ya matibabu ya maradhi ya akili katika Hospitali ya Muhimbili ambako alikuwa akiendelea na matibabu yake.


ERICK  alitoweka nyumbani saa tatu usiku, Ijumaa  August 17 Mwaka huu na kwenda  kusikojulikana. Dada wa ERICK, CYNTHIA KIMASHA anawaomba wasamaria wema  kwa  atakaye muona anaomba kutoa taarifa kituo chochote cha polisi kilichopo karibu nae au kuwasiliana kupitia namba 0657 655555 au  0714 533166.   
= = = =

No comments:

Post a Comment