Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, August 24, 2012

Baadhi ya Viongozi wa Dini ya Kislam kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu waliokuwa wakipinga zoezi la sense ya watu na makazi waungana na Watanzania wengine kushiriki zoezi hilo


Ikiwa imebaki Siku moja kuanza kwa zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kwa nchi nzima baadhi ya Viongozi wa Dini ya Kislam kutoka Jumuiya na Taasisi za Kiislamu waliokuwa wakipinga zoezi hilo wamejiengua katika Jumuiya na Taasisi hizo na kuungana na Watanzania wengine kushiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
Akizungumza Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Taasisi ya Islamic Peace Foundation, Sheikh SADIKI GODIGODI amevitaka Vyama vya siasa nchini kuacha tabia ya kuwatumia baadhi ya Viongozi wa dini kuanzisha migogoro na Serikali likiwemo suala la kuwashawishi waumini wa Dini ya kiislam kutoshiriki zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.
Katika hatua nyingine Sheikh GODIGODI ameeleza kusikitishwa kwake na baadhi ya Watu kusambaza ujumbe wa simu kwa Waumini wa Dini ya kiislam ukiwataka kutoshiri zoezi hilo na kuwataka Waislam kote nchini kupuuza ujumbe huo na kuwataka kushiriki ipasavyo katika Sensa ya Watu na Makazi kwani ni haki yao.
Kwa upande wake mmoja wa Wahadhiri aliyejiengua kutoka kwenye Jumuiya na Taasisi za kiislam ambao wanapingana na zoezi hilo, amesema kwamba amifikia uamuzi wa kujitoa katika Jumuiya hiyo kutokana na kutoona mantiki ya kupinga zoezi la Sensa ya Watu na Makazi kutokana na umuhimu wake katika utekelezaaji wa maendeleo nchini.

No comments:

Post a Comment