Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Tunapatikana Sinza kwa Remmy

Friday, August 24, 2012

British Airways kurejesha huduma zake Tanzania

Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya Ndege ya British Airways imeirejesha angani ndege yake iliyokuwa ikifanya safari zake za kusafirisha abiria kati ya Dar es Salaam na London, Uingereza.

Kurejeshwa kwa ndege hiyo aina ya BA 737 kutaiunganisha Afrika kwenye mtandao wa safari za ndege na nchi za Ulaya unaofanywa na kampuni hiyo ya Britisha Airways.
Akizungumza kupitia taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na shirika hilo, jana, Ofisa Uhusiano wa British Airways, Mary Barry alisema safari hizo zimerejea baada ya matengenezo ya kawaida ya ndege hiyo.
Alisema ndege hiyo imerejea tena baada ya matengenezo hayo na itakuwa ikifanya safari zake za Ulaya na Afrika katika kipindi cha majira ya joto baada ya kutoonekana kwa kipindi cha miaka 25.
“British Airways inajisikia furaha kukamilisha matengenezo ya ndege hii ambayo ni moja kati ya zile ndogo lakini tunaamini itakidhi haja za wasafiri wa Afrika,” alisema.
Kama ilivyo kwenye ndege zake, alisema abiria kwenye ndege yake watafurahia huduma za aina mbalimbali kama vile vyakula, vinywaji na vifaa vya kisasa vya elektroniki, kwa lengo la kuburudisha wateja.
Wakati huohuo, Shirika hilo limesema kuwa litatoa punguzo maalumu la nauli kwa abiria wa Tanzania watakaosafiri na ndege hiyo kwenda Ulaya na New York Marekani.
Alisema tayari huduma za tiketi kwa safari zake zinapatikana kwa maajenti mbalimbali nchini, wakiwemo BA Travel.
Chanzo: mwananchi.co.tz

No comments:

Post a Comment