Mwanamuziki
mwenye asili ya Tanzania na Italia CHANTAL SAROLDI amesema muziki wa Tanzania unayo nafasi kubwa
kimataifa kutokana na Watu kutoka nje kupendelea sana nyimbo zenyeasili ya nchi
za Kiafrika.
Mwanamuziki
huyo amesema hayo wakati akiongea na waandishi wa habari kuhusiana na maonesho
atakayoifanya jijini kwa mualiko wa
ubalozi wa Itali nchini.
Amesema
muziki wa wanamuziki kutoka Afrika ikiwemo Tanzania wanapaswa kufanyaziara za
mara kwa mara nje ya nchi zao ili kuutangaza muziki wao huku akithibitisha kua
Raiya wa Italia wanapenda sana utamaduni hasa wa nyimbo kutoka barani Afrika.
Nae balozi
wa ITALI nchini Tanzania LUIGI SCOTTO amesma muziki ni moja ya njia za kukuza
ushirikiano hivyo ubalozi wake umeamua kumualika mwanamuziki huyo ambaye
mamayake ni raiya wa Tanzania huku babayake akiwa muitalia ili kuja kuonesha
jinsi Tanzania na Italii zilivyokuwa na urafiki wa karibu.
Kuhusiana na
ziara ya mwanamuziki huyo , msimamizi wa maonesho hayo SAMANTAR ABDINUR LUSUF
amesema ziara ya mwanamuziki huyo itamfikisha pia katika kisiwa cha Zanzibar.