Mnyama Simba akikosa nyama wakati mwingine hulazimika
kula hata nyasi ilimradi tu adhibiti njaa inayomkabili na maisha yaende.
Ndivyo ilivyo kwa Wasichana na akimama wengi maeneo ya
Vijijini ambao hulazimika kutumia kanga na vitenge kama mbadala wa Taulo Maalum
za kike maarufu kama pedi.
Changamoto ya ukosefu wa taulo maalum za kike inatajwa
kuhatarisha Afya za Wasichana na Wanawake wengi Vijijini kutokana na kutumia
vifaa ambavyo si salama kwa afya zao pindi wanapoingia kwenye hedhi.
Meneja Mradi uliojikita kuwasaidia Wanafunzi wa Kike
Mashuleni kutoka Shirika la Maendeleo la Uholanzi, (SNV), ROZALIA MUSHI,
anatumia Siku ya hedhi Duniani kufafanua zaidi ukubwa wa tatizo hilo katika
maeneo ya Vijijini.
Kila anaetoa chozi anasababu inayopelekea chozi hilo
kulazimika kumtoka, Wakati Wasichana wa Vijijini wakikumbwa na tatizo la
ukosefu wa taulo za kike na kulazimika kutumia njia mbadala, wale wa maeneo ya
Mijini na wao wana kilio chao.
Kila jambo lina chanzo chake
na hapa ROZALIA MUSHI anabainisha
kilichochangia Dunia kulazimika kuiadhimisha Siku hii.
Camera na kipaza sauti cha
Clouds Tv hakikuishia hapo kinaelekezwa katika moja ya maduka yanayofanya
biashara ya Mataulo maalum ya kike ili kubaini hali ya biashara hiyo na
upatikanaji wake.
Lakini je hali ya
miundombinu kwenye Shule mbalimbali nchini pindi Mwanafunzi anapoingia kwenye
Siku zake akiwa yupo maeneo ya Shule ipoje..? MADINA KEMILEMBE ni Afisa Elimu
Mkuu, Kutoka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi anaeleza azidi.
Siku ya hedhi Duniani imeambatana
na kauli mbiu isemayo “ Usisite kuzungumzia hedhi’’ kauli hii inatokana na
kitendo cha Wanajamii wengi kuhofia kuzungumzia Siku hiyo.
No comments:
Post a Comment